Libertatem Pugnator
JF-Expert Member
- Aug 24, 2017
- 1,006
- 1,377
Usijitingishe mkuu. Mama anaponya nchi. Magufuli aliiharibu sana nchi hii 😂😂😂Tanzania ni mali ya Watanzania wote,wenye itikadi ya vyama vya kisiasa na wasio na vyama pia.
CCM imejijengea imani kuwa ina hati miliki ya Tanzania,ndo maana mambo yanakwenda kama mnavyoona.
Leo hii kg ya nyama ya ng'ombe Dar ni Tsh 10,000 na vijjini ni Tsh 7,000 hadi 8,000,.
Tanzania ni Taifa la pili Africa Baada ya Ethiopia kwa kuwa na idadi kubwa ya ng'ombe.
Hebu jiulizeni nchi inakwenda wapi hii? Mwaka 2012 kipande cha sabuni kiliuzwa Tsh 200, na nyama kg moja ilikuwa Tsh 4,00.
Sasa hivi kuna mfumuko mkubwa mno wa Bei kuwahi kutokea utadhani Taifa lilikuwa vitani.
Kwa sababu CCM inajivunia Dola kubakia madarakani,siye tujivunie Mungu kuitoa madarakani,nawahakikishia Tukiungana tukafanya maombi ya Rehema juu ya Tanzania, CCM itatoweka na ukatili wake hamtaamini.
Ni mpumbavu pekee mwenye kuweza kupuuza Maombi.
Daudi alimshinda Goaliathi kwa kumtegemea MUNGU.
Na sisi tukifanya hivyo Tutaishinda CCM.
Maisha hayaeleweki ,mara Tozo,sijui mara nini.
Mungu yupo,naye husimama na wenye haki.