I always wonder,hivi mhando na trupu lake la tanesco wakiamua kugoma na kuzima mitambo mtera itakuwaje? Dawasco nao wakigoma na kuzima mitambo ruvu chini itakuwaje? Na staff wa huduma za anga wakizima mitambo kisa haina quality itakuwaje? Na zima moto waki down tools kisa magari mazee je? For that matter hata wazoa taka darisalama waki down tools je?
This reminds me story ya Anus iliyogoma kupitisha choo eti inadharauliwa matokeo yake ikawa ni head ache na mwili mzima kuwa dysifunctional.
Ndugu zangu hakuna taaluma iliyo bora kuliko nyingine,hata Invisible na taaluma yake ya IT ana mchango mkubwa tu katika jamii.
Nawasilisha,
Bishanga Abashaija.
Muhimbili is the crime scene
Kuwa makini na toa taarifa sahihi ct scan mnh ni lak 1.7 na ni mbovu mda mrefu , mashine moja inahudumia nchi nzima haifanyiwi service itadumu vipi???
kama madaktari wana fight juu ya hali ngumu na mazingira magumu ya kufanyia kazi basi wangeweza kueleweka zaid kama wangewajumuisha na manesi ambao wanafanya nao kazi kwa karibu. tena wangelifanya hivi wangepata mass sapoti kubwa sana ila jinsi ilivyo its like wao hawajui wanataka nini na watawin vip majority ya watu. japo dr anampasua mtu na kumuandikia dawa ila anayesafisha na kufunga vidonda ni nesi anayempa dawa ni nesi yeye anaandika tu sasa huwa najiuliza hivi manesi wakisema hawazitoi hizi dawa kwa wagonjwa hata kama dr kaandika ingekuwaje? mbona kama madaktari wanasahau uhalisia wanabebwa na hisia za kuwa watu bora kuliko wengine?
kibaya zaid ni pale unapokwenda hosp ukataka kuongea na dr juu ya ugonjwa wako omba Mungu usiwe na knowledge ya kile kitu ila kama wengine ambao ni multi professional huwa tunakoma manake ukimwmbia unachokijua jamani anaona kama unaundermine ujuzi wake wakati nafikiri ndio njia nzuri ya kufikia maamuzi juu ya swala lako. to me sipend jinsi wanavyo act.
kila profession ina chama chake cha kitaaluma na kuhitaji kutetea mahitaji na mapenndekzo ya taaluma hiyo..mfano Madaktari, Wafamasia, Wauguzi, Watu wa maabara n.k.
-si kila madai huusisha taaluma zote wakati wote
- kuna dai katika madai pendekezwa inayojumuisha taaluma zote
kuhusu kuwa na uelewa..ni vizuri, mara nyingi nafurahi napokutana na wagonjwa wenye uelewa na kusoma angalau ugonjwa kupitia na aina za matibabu. Kwa mfn nilikutana na mgonjwa wa saratani ya ngozi(Malignant melanoma) iliyokuwa katika mguu mmoja, tuliposhauriana kufanya vipimo kuhusu kuona ni jinsi gani imesambaa mwilini(kwa kutumia Ct- scan, Ultrasound sonography, na X-ray) kwa mgonjwa huyu ilikuwa ni shida madai yake ni kuwa tatizo liko ktk mguu, kwa nini tusikate mguu na kuhangaika na mengine..lakini kwa kulazimisha ilibidi nilazimishe vipimo! saratani ya ngozi kwa mfano haikuchukui hata miaka miwili) sasa kama kwa mfano ningelazimisha kufata tu maelezo ya mgonjwa aliyoyasoma ktk mtandao(ambao kila mtu anaweza kuandika kwa maoni yake) mgonjwa huyu alikuwa anapotea.
Ushauri wangu ni vema kusoma katika mitandao ya kidaktari au ule wa Shirika la afya duniani(WHO) kuona ni njia gani za vipimo,matibabu mgonjwa anaweza kupata, lakini zaidi ya yote kujua ni njia zipi zilizo hapa nchini.
Sina tabia ya kufungua nyuzi jukwaa la siasa (JLS), anga zangu ni mmu na chi chat.
Lakini katika hili la hospitali ya muhimbili kwa kuwa naijua vyema naomba niseme haya yafuatayo:
1.MRI ( magetic resonance imaging):
Mashine hii muhimbili ipo,gharama za kipimo ni sh 120,000.-
Ukienda agha khan,regency na hindu mandal unapigwa sh 540,000.- kwa kipimo.
2.CT scanning:
Muhimbili tsh 80,000.-
Ukienda agha khan,regency na hindu mandal unapigwa sh 360,000.-
3. Kidney dialysis:
Hiyo ndo usiseme.
In short,vipimo hivi day in day out ukienda muhimbili unaambiwa vimekufa, nenda agha khan,hindu mandal na regency,same doctors hao hao wa muhimbili wana handle vifaa hivi private hospitals na kutoa majibu kwa gharama kubwa,mnyonge inabidi augulie tu cant afford.
Kila kukicha technians from Phillips company Uholanzi wanakuja TZ kurekekibisha mashine hizi muhimbili na zinakuwa ok,wakitoka tu zinakufilia mbali, patients wanaendelea wenda private hospitals,doctors wanalalamika vifaa duni.
Tutafika kweli?????
Wasi wasi wangu ni nini hasa kinasababisha mashine za dialysis,ct scanner na MRI kila kukicha muhimbili zimekufa , opearators kwa maana ya technicians , wasoma majibu kwa maana ya doctors ambao wanasimamia mashine hizi za muhimbili ndo more or less unawakuta hao hao regency,agha khan na hindu mandal wanapiga mzigo?
Mkuu unataka tutajane kwa majina hapa? Twajuana ati.
chit chat na mmu oyeeee
huku sitii neno maana walishaninyoa sasa naoopa kunyolewa ngozi.
Kuna kipimo cha figo pale ocean road kimekufa, mgonjwa anaambiwa aende Bugando, nauli, mahali ya kuishi, gharama ya kipimo chenyewe, wanyonge bora turudi kwenye maombi tu.
unapigwaje maswali ya Abbot wakati wewe pua ngwini?
He he he, hongera, umeikomboa chit chat na mmu lol