Watanzania wengi wanaamini Rushwa ni kikwazo cha Haki na inachangia kutokuwepo kwa Usawa

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
MTAZAMO WA RUSHWA TANZANIA.jpg


Rushwa ni tatizo kubwa nchini Tanzania na inaathiri maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta ya umma, miundombinu, afya, elimu, na biashara. Hali ya rushwa nchini inaweza kuelezewa kama changamoto inayosababisha ukosefu wa uwazi, upendeleo, na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Rushwa inapunguza ufanisi wa huduma za umma, inakwamisha ukuaji wa uchumi, na inasababisha pengo la kutokuwepo kwa usawa. Sekta muhimu kama afya na elimu hupata athari kubwa, kwani rasilimali zinapotumiwa vibaya au kutowasilishwa kwa uwazi, huduma muhimu kwa wananchi hupungua na ubora wake hushuka.

Pamoja na Serikali kuchukua hatua za kupambana na rushwa, kama kuanzisha vyombo vya kupambana na rushwa na kuweka sheria. Hata hivyo, jitihada hizo zinahitaji kuimarishwa zaidi ili kukabiliana na changamoto zinazohusiana na rushwa, ikiwa ni pamoja na ufisadi wa ngazi za juu, kutokujali kwa utawala bora, na ukosefu wa uwajibikaji.

Mtazamo wa Watanzania kuhusu rushwa ni tofauti na inaweza kutofautiana kati ya watu binafsi na makundi mbalimbali. Hata hivyo, rushwa inachukuliwa kuwa tatizo kubwa na lenye athari mbaya kwa maendeleo ya nchi.

Wengi wa Watanzania wanahisi kuwa rushwa inaathiri vibaya ufanisi wa huduma za umma, kama vile afya, elimu, na miundombinu. Wananchi wanaolazimika kutoa hongo au rushwa ili kupata huduma zinazostahili wanahisi kudharauliwa na kujisikia kukosa haki.

Kikwazo Cha Haki

Kwa mujibu ripoti ya Haki za Binadamu ya 2022 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), rushwa ilibainishwa kuwa kikwazo kikubwa katika kupata haki mwaka 2022. Wanajamii waliotoa majibu kwenye utafiti wa ripoti hiyo iliyozinduliwa mapema mwaka huu 2023 pia walikuwa wameulizwa ni kwa kiasi gani rushwa ni tatizo katika kupata haki.

Asilimia kubwa ya wanachi waliotoa majibu katika ripoti hiyo (42.5%) walisema ni tatizo kubwa, ikifuatiwa na zaidi ya theluthi moja, ambao walisema ni tatizo. Ni chini ya robo tu ya waliojibu (22.5%) wanaamini kuwa rushwa ni tatizo la wastani, tatizo dogo, au sio tatizo kabisa.

MTAZAMO WA WATANZANIA KUHUSU RUSHWA.jpg

Kwa upande wa tofauti za kikanda, asilimia ya washiriki ambao waliona rushwa kuwa ni tatizo kubwa na tatizo lilikuwa kubwa zaidi Kigoma (92%), ikifuatiwa na Pwani (91%), Mbeya (90%), Mtwara (88%), na Kagera (87%). Asilimia ilikuwa ndogo zaidi Morogoro (51%), ikifuatiwa na Katavi (53%), Iringa (53%), Dodoma (63%), na Rukwa (67%).

Mikoa mingine ilikuwa na asilimia kati ya 67% na 87%, ikiwemo Tabora (79%), Singida (81%), Tanga (81%), Kilimanjaro (78%), Arusha (77%), Njombe (73%), na Mwanza (85%). Hii inaonesha kuwa wengi wa wanajamii katika mikoa karibu yote waliona rushwa kuwa ni suala kubwa katika mfumo wa haki.

Ripoti hiyo ambayo hutolewa kila mwaka kuangazia hali ya haki mbalimbali ikiwemo za kisiasa na kijamii pia inaonesha kuwa data ya kina iliyopatikana katika mikoa iliyofanyiwa utafiti pia inaonyesha ukubwa wa tatizo. Kwa mfano, mkoani Singida, baadhi ya washiriki wa jamii waliohojiwa walidai kuwa rushwa ni jambo lililoenea katika mahakama za mwanzo, mahakama za wilaya, na kuwalaumu watu wenye uwezo wa kifedha kwa kuwahonga watoa haki kama polisi na maafisa wa mahakama ili kuvuruga haki.

Mapambano Ni Muhimu

Hata hivyo, Watanzania wana imani na matumaini kuwa kupambana na rushwa ni jambo la muhimu na wanathamini juhudi za serikali na vyombo vya kupambana na rushwa katika kushughulikia tatizo hilo. Kuna mwamko unaonekana miongoni mwa wananchi na taasisi za kiraia katika kuelimisha na kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa.

Watanzania wengi wanakubaliana kuwa rushwa inachangia pengo la kutokuwepo kwa usawa kwa kuwafaidisha wachache wenye uwezo na kuacha wengi bila kupata fursa na huduma za msingi.

Hata hivyo, kuna mwamko unaonekana miongoni mwa wananchi na taasisi za kiraia katika kuelimisha na kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa. Asasi hizi zimechukua jukumu muhimu katika kuelimisha umma, kushinikiza mabadiliko, na kusaidia kuweka mifumo inayopambana na rushwa.

Programu mbalimbali za kupambana na rushwa, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa, kusaidia waathirika wa rushwa, na kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma.

Kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa na kuhamasisha hatua dhidi ya watoa rushwa na wala rushwa nchini Tanzania. Elimu ina jukumu muhimu katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu athari za rushwa kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa jamii.

Kupitia kampeni za elimu watu wanaweza kufahamu madhara ya rushwa katika maeneo kama elimu, afya, miundombinu, na upatikanaji wa huduma za msingi. Wanaweza pia kuelewa kuwa rushwa inachangia pengo la kutokuwepo kwa usawa na kuwafaidisha wachache wakati wengi wanakosa fursa na huduma muhimu.
 
Rushwa ni adui wa haki kweli na naamini hakuna mtu anayetaka kutoa rushwa ila mifumo ya utoaji huduma na watoa huduma wanachangia kwa kiasi kikubwa rushwa kuendelea kushamiri kwa kuchelewesha huduma au kutokutoa huduma stahiki kwa usawa.

Hali hiyo inasababisha mtu kushawishika atoe kitu ili apate haki yake ambayo bila kutoa kitu itachelewa au hatoipata kabisa. Kuna haja ya kuja na mifumo rafiki katika kutoa huduma ili watu wasiweze kuona rushwa ndio njia rahisi ya wao kupata huduma.

Kila mmoja wetu aone ana wajibu wa kutenda haki na kupigana vita dhidi ya rushwa ili kutenda haki kwa kila mtu.
 
Ogopa sana hii kitu inaitwa RUSHWA, ni adui wa haki, maendeleo na chungu mzima. Bahati mbaya ofisi nyingi Serikalini zimejenga mazingira ya rushwa ili kupata huduma bora. Bila kutoa hiyo rushwa huwezi kupata huduma iliyo bora, au huduma ya siku moja unaweza kamilisha baada ya wiki/mwezi.

Mamlaka husika inafanya vizuri kupambana na rushwa ila nasisitiza iongeze jitihada hasa sehemu za vijijini huko maana wananchi wengi ndio wanapitia kaa la moto wanapohitaji huduma za kijamii kama afya nk

Kila mwananchi aone jukumu la kupambana na rushwa si la serikali tu bali ushirikiano baina ya mwananchi na serikali.
 
Ogopa sana hii kitu inaitwa RUSHWA, ni adui wa haki, maendeleo na chungu mzima. Bahati mbaya ofisi nyingi Serikalini zimejenga mazingira ya rushwa ili kupata huduma bora. Bila kutoa hiyo rushwa huwezi kupata huduma iliyo bora, au huduma ya siku moja unaweza kamilisha baada ya wiki/mwezi.

We acha tu, mfano ofisi ya vizazi na vifo, RITA kuna mazingira ya rushwa sana ili kupata vyeti vya kuzaliwa kwa watu ambao hawana.

Ukienda RITA makao makuu wanakwambia acha jina njoo baada ya siku 30 uje ujue kama cheti cha kipo au hakipo kwenye mtandao kwa wale ambao wanaenda kuhakiki, baada ya hizo siku 3 ndio ukajaze fomu za kuomba cheti.

Halafu wanakuangalia kama umeonesha kuhamaki wanajua unashida wanakwambia kama una 10000, tunakuangalizia leoleo na fomu unajaza na kama unaweza kuongeza 30000 kama hakipo unatengenezewa leo leo na kuondoka nacho.

Mtu anaona nikae siku 30, kisha nije kujaza fomu halafu nisubiri miezi bora nitoe 40000 niondoke nacho, watu wanatoa 40000 na kuondoka na cheti, wakati gharama ya cheti haizidi 10000.

Mazingira ya rushwa yanalazimishwa sana kila sehemu, tunatakiwa kushirikiana na TAKUKURU kuhakikisha tunatembea katika uwanja wa vita pamoja
 
Ni kweli kabisa kwamba rushwa ni tatizo kubwa nchini Tanzania na inaathiri maeneo mbalimbali kama vile sekta ya umma, miundombinu, afya, elimu, na biashara. Hali ya rushwa inaweza kuelezewa kama changamoto inayosababisha ukosefu wa uwazi, upendeleo, na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Rushwa ina madhara makubwa kwa ufanisi wa huduma za umma, ukuaji wa uchumi, na usawa wa kijamii. Sekta muhimu kama afya na elimu zinapata athari kubwa, kwani rasilimali zinapotumiwa vibaya au kutokuwa wazi, huduma muhimu kwa wananchi hupungua na ubora wake hushuka.
 
Back
Top Bottom