Tunaongelea wakati huu siyo huko nyuma. Vinginevyo tusingekuwa na matajiri waliotoka familia maskini kama wangebakia kulaumu wazazi hawakuwachia chochote.
Hivi nchi inakosa kitu gani kufanya nchi iwe zaidi ya poor leadership?
Mgodi wa Kiwira ulipoanza 1988 ulikuwa na uwezo wa kuzalisha 6MW kwa kutumia vumbi la makaa ya mawe, na zilikuwa nyingi kwa mgodi na kiasi kinachobaki kingeweza kuusadia mkoa wa mbeya japo baadaye Wilaya ya Kyela iliipata umeme huo. Sasa jiulize hawa watawala nini kwa ajili ya mgodi w
Kwa hiyo wewe unajua Tanzania ni Nyerere tu? Unajua Hitler alivyoharibu uchumi wa ujerumani 1939-1945, wangekaa kama wewe kumlaumu Hitler wangefika hapo walipo leo? Huyo Nyerere mpaka anaondoka madarakani hakuwahi kuanzisha mgodi wowote mkubwa ukiacha mgodi wa almasi Mwadui ambao aliukuta kwani huo umeanza 1940, pamoja na kujua kuwepo kwa madini mengi sana hapa nchini.Hoja yake kubwa ilikuwa hawezi kuruhusu madini yachimbwe wakati hana wataalam wazawa wa kuyasimamia, kama angekuwa haipendi nchi hii asingekosa wa kuyachimba na yeye akafaidika.
Sasa waliofuata nyuma mwenyewe unajua kinachoendelea.
Mabadiliko huwa hayazuiwi na historia ni suala la utashi tu. Viongozi tulio nao leo wakitaka katiba mpya, 2024 haitaisha tutakuwa nayo.
Tatizo la umeme halina uhusiano na usamaria wa awamu ya kwanza,ni uzembe wa kipindi hiki unaotokana na uswahili mwingi pasipo kuchukua hatua. Maharage Chande alituambia maji yamepungua wakati ni uongo,waliomuweka walipoona ataumbuka wamemtoa maana kisingizio cha maji hakipo tena. Kwa nini wasitoke na kusema ukweli shida ni nini. Majuzi tunamsikia Makonda mtu mkubwa ndani ya ccm naye analalamika,maana yake hata wenye ilani hawajui tatizo la kukosekana umeme ni nini!!!