Watanzania wengi wana akili za Kitoto!

Watanzania wengi wana akili za Kitoto!

Watoto mbona wana akili sema tu hawana akili kabisaa usiwafananishe na watoto wenye akili Tanesco walikua wanauza nguzo za Umeme Tsh 1 M wakiwaaminisha wasio na akili kuwa nguzo zinatoka SA wakati hao SA nguzo zao nyingi zinatoka Malawi hawauzi nguzo wale harafu hakuna hata mtu mmoja aliejua kwa miaka mingi mpaka Waziri mmoja akaja kufichua huo ufisadi...
 
Sasa si uwaunganishe watu wazima wenzie mbona unalialia kama mtoto tu na wewe
Kwani na wewe ni kati ya hao wengi wenye akili za kitoto?
Mbona unatokwa na povu sana Mkuu ilhali mimi sikumtaja mtu yeyote kwamba ana akili za kitoto?!
Anyway, Watanzania wengi (siyo wewe) tuna akili za kitoto.
 
Watoto mbona wana akili sema tu hawana akili kabisaa usiwafananishe na watoto wenye akili Tanesco walikua wanauza nguzo za Umeme Tsh 1 M wakiwaaminisha wasio na akili kuwa nguzo zinatoka SA wakati hao SA nguzo zao nyingi zinatoka Malawi hawauzi nguzo wale harafu hakuna hata mtu mmoja aliejua kwa miaka mingi mpaka Waziri mmoja akaja kufichua huo ufisadi...
Ahsante sana kwa ufafanuzi Mkuu.
 
Yule mwendazake ndio ametufikisha hapa kwa kupora uchaguzi akiamini analisaidia taifa kumbe analiangamiza ona sasa leo hatuna watu wa kuiwajibisha serikali

Ingekua enzi za mzee wa kasi na viwango au enzi za Anna naamini kabisa hata rais angekua ameshapigiwa kura ya kutokua na imani nae
Yeye alitaka watu ambao watampa Uraisi wa Maisha kumbe Mungu si Abdallah Leo hii katuachia Msala.
 
Haiwezekani matatizo yetu mengi yasababishwe na viongozi wa juu kabisa, halafu lawama zote tuwatwishe watendaji wa chini.
Wanaopeleka lawama kwa viongozi wa chini ni viongozi wa juu na wala sio wananchi mkuu.

Ukifuatilia hata humu jamvini wananchi wengi wanalaumu VIONGOZI WA JUU kwamba wanazingua na watu wanatoa mifano ya magufuli enzi zake.

Hivyo kama utoto ilikuwa useme wanao VIONGOZI WA JUU na sio wananchi kwa sababu hao viongozi wa juu ndio wanawalaumu viongozi wa chini(sio mzizi wa tatizo) na wananchi wanalaumu viongozi wa juu(mzizi wa tatizo).
 
Mfano wako wa watoto hauna uhalisia kabisa. Wala hauleti maana yoyote kiuhalisia. Ni ujuha tu.

Pia maelezo yako ya uongozi kuwa ni mbovu, hilo nakukatalia kabisa.

Tanzania ni wazi kabisa kuwa uongozi uliokuwa mbovu ni ule wa awamu ya kwanza, ndiyo ulioweka misingi na ndiyo hadi leo hii katiba inayotumika Tanzania, msingi wa sheria na kanuni za kuendesha nchi, uliwekwa na awamu ya kwanza.

Tanzania watendaji ni wabovu kuanzia ukitoka tu nfazi ya uongozi wa juu, ambayo kiuhalisia haina njaa leo wala kesho. Imeshalindwa na katiba.

Utakuwa ni mjinga leo hii usitegemee kuwa utakapomchukuwa mtendaji ambae historia inaonesha toka alipotokea huko ni umasikini na njaa kali iliyomfanya kuwa na tamaa ya kila kitu umpe vimadarakakidogo halafu usitegemee kuwa hatafakamia na kulewa hayo madaraka.

Watendaji wazuri watatoka kwenye nasaba zilizoshiba siyo nasaba zenye njaa.
Sawa Bibi, lakini mbona huku kwetu hawa wanaotoka kwenye nasaba zilizoshiba/zilizovimbewa hawana msamiati wa kiasi kwao?!
Maana hata Mkuu alionekana kushangazwa nao kipindi fulani.
Mimi nafikiri, ili tuendelee tunawahitaji sana Wazalendo bila kujali wanatokea kwenye familia za hadhi ipi (matajiri/maskini).
Hata hivyo, historia inaonesha wale wa kutokea familia za kawaida huwa wanakuwa viongozi wazuri na wazalendo zaidi hasa hasa katika nchi yetu. Hayati JKN, Hayati BWM na Hayati JPM, wote hawa wametokea kwenye familia za kawaida na wengine familia maskini kabisa, lakini athari za uongozi wao kwa Taifa letu, zimekuwa chanya zaidi kulinganisha na wale ambao hawajawahi kuhisi njaa!!
 
Wanaopeleka lawama kwa viongozi wa chini ni viongozi wa juu na wala sio wananchi mkuu.

Ukifuatilia hata humu jamvini wananchi wengi wanalaumu VIONGOZI WA JUU kwamba wanazingua na watu wanatoa mifano ya magufuli enzi zake.

Hivyo kama utoto ilikuwa useme wanao VIONGOZI WA JUU na sio wananchi kwa sababu hao viongozi wa juu ndio wanawalaumu viongozi wa chini(sio mzizi wa tatizo) na wananchi wanalaumu viongozi wa juu(mzizi wa tatizo).
Ni sahihi Mkuu, lakini sisi wanachi ndo tumewapa madaraka hao viongozi wa juu!
Kwa maneno mengine, wale viongozi wa juu ni wawakilishi wetu tulio wengi. Tuna haki ya kumwondoa kiongozi yeyote wa juu tukiona haendani na sisi. Lakini hatufanyi hivyo kwa sababu wengi tuna akili za kitoto!
 
Kwani na wewe ni kati ya hao wengi wenye akili za kitoto?
Mbona unatokwa na povu sana Mkuu ilhali mimi sikumtaja mtu yeyote kwamba ana akili za kitoto?!
Anyway, Watanzania wengi (siyo wewe) tuna akili za kitoto.
katika utoto unajifunza mengi sana ukitaka,
lakini kulialia na kubwekwabeka kiujumla jumla ni tatizo la kiafya akilini
 
Ni sahihi Mkuu, lakini sisi wanachi ndo tumewapa madaraka hao viongozi wa juu!
Kwa maneno mengine, wale viongozi wa juu ni wawakilishi wetu tulio wengi. Tuna haki ya kumwondoa kiongozi yeyote wa juu tukiona haendani na sisi. Lakini hatufanyi hivyo kwa sababu wengi tuna akili za kitoto!
kweli we ni mtoto dah 😜
 
Rais Hana Nia ya dhati ya kupambana na ubadhirifu, uzembe,RUSHWA na ufisadi. Kama wewe siyo msafi huwezi kusafisha wengine. Nchi imemshinda kabisa Bora aondoke zake sasa hivi
 
Mkuu, kwani wewe unafaidika/kunufaika na jinsi mambo yanavyoenda?
Kama ni mnufaika, naomba unisamehe.
Hata hivyo mara zote umekuwa negative sana kwa post zangu hapa jamvini!
Unawezekana ukawa sahihi Ila Mimi sipendi MTU anayetweza utu wa MTU.
 
Mfano wako wa watoto hauna uhalisia kabisa. Wala hauleti maana yoyote kiuhalisia. Ni ujuha tu.

Pia maelezo yako ya uongozi kuwa ni mbovu, hilo nakukatalia kabisa.

Tanzania ni wazi kabisa kuwa uongozi uliokuwa mbovu ni ule wa awamu ya kwanza, ndiyo ulioweka misingi na ndiyo hadi leo hii katiba inayotumika Tanzania, msingi wa sheria na kanuni za kuendesha nchi, uliwekwa na awamu ya kwanza.

Tanzania watendaji ni wabovu kuanzia ukitoka tu nfazi ya uongozi wa juu, ambayo kiuhalisia haina njaa leo wala kesho. Imeshalindwa na katiba.

Utakuwa ni mjinga leo hii usitegemee kuwa utakapomchukuwa mtendaji ambae historia inaonesha toka alipotokea huko ni umasikini na njaa kali iliyomfanya kuwa na tamaa ya kila kitu umpe vimadarakakidogo halafu usitegemee kuwa hatafakamia na kulewa hayo madaraka.

Watendaji wazuri watatoka kwenye nasaba zilizoshiba siyo nasaba zenye njaa.

Aya yako ya tano, ndio inafanya wengine tuamini udikteta ndio unaweza kuitoa nchi hapa ilipo. Hao watendaji wabovu unaowazungumzia kutoka familia zenye njaa tayari wapo kwenye mifumo kuanzia ngazi ya Urais, mawaziri mpaka chini huko.

Hiyo katiba iliyokosewa awamu ya kwanza ndiyo hiyo mpaka leo tumeshindwa kuirekebisha, huoni kama hao hao watendaji njaa njaa ndio wanaoikwamisha kwa maslahi yao binafsi?

Suluhu ni nini sasa? tuendelee kulialia na kukubaliana na hali au tuchukue hatua kwa kufanya mapinduzi na kuweka tunachoona kinatufaa.
 
Tuchukue hatua, tuweke wanaotufaa.
Naunga mkono hoja
 
Hapo nitakupinga, awamu ya kwanza utailaumu bure. Ni sawa na mtu mzima anayemlalamikia baba yake kuwa hakumsomesha ndio sababu ya yeye kuwa na maisha magumu, anasahau wapo wenzake wamepata elimu wakiwa jela.
Ukirudi kwenye hoja yako,ni kweli awamu ya kwanza iliacha katiba mbovu,na hata Mwalimu Nyerere aliwahi kukiri hivyo waziwazi,hata hivyo hata Kenya hawakuwa na katiba nzuri,tulikuwa na tofauti ndogo tu, isipokuwa Wakenya waliamka kudai mabadiliko ya katiba bila woga,na pamoja na machafuko ya 2007 ambayo yalisukuma kupatikana kwa katiba mpya 2010, bado ukweli unabakia kwamba siye itatuchukua muda mrefu sana kuwa na katiba angalau kama ya Kenya,siye tuko too complacent.
2015 alivyoingia Magufuli,tukaridhika na utendaji wake, hata wale waliokuwa mstari wa mbele kudai katiba,km akina Polepole na Prof. Kabudi wakaridhika kwamba katiba hahitajiki tena kitu ambacho ni ujinga ulitufunika kwa kuamini mtu na kumsahau Mungu, na yaliyotokea ni historia.
Kama kweli tunahitaji mabadiliko ya kweli ni sisi kuamua na kuacha kubakia kulalamika eti tuliachiwa katiba mbovu na awamu ya kwanza, mbona tulidai vyama vingi na Mwalimu huyohuyo akaunga mkono akiwa Mwenyekiti wa ccm!!
Watawala wanatufahamu ni wepesi wa kuridhika na ndio sababu tukiona akina Makonda wakifokea watu kwenye majukwaa tunachekelea,tunasahau kuwa tunahitaji mfumo utakaosimamia mambo yetu bila ghiliba za viongozi za kutembea na makamera na waandishi machawa kutuzuga.
Katikati ya changamoto ya ukosefu wa umeme wao wako busy na vitoto vyao eti kwenye mkutano wa chipukizi,halafu utegemee kuna suluhu bila wananchi kuamka na kuwakataa na wajue tumewakataa.
 
Wewe unaifananisha Kenye ambayo haijajiingiza kwenye balaa ya usamaria mwema na sii tuliojiingiza kwenye mabalaa ya kunyang'anya mali za watu tokea awali?

Piga uwa, utarudi kuuona ubovu tokea awamu ya kwanza. Huwezi kujenga nyumba ya ghorofa kumi kwenye misingi ya nyumba za chini. Nani aliiweka misingi mibovu kwa miaka 25 mfululizo?
 
Aya yako ya tano, ndio inafanya wengine tuamini udikteta ndio unaweza kuitoa nchi hapa ilipo. Hao watendaji wabovu unaowazungumzia kutoka familia zenye njaa tayari wapo kwenye mifumo kuanzia ngazi ya Urais, mawaziri mpaka chini huko.

Hiyo katiba iliyokosewa awamu ya kwanza ndiyo hiyo mpaka leo tumeshindwa kuirekebisha, huoni kama hao hao watendaji njaa njaa ndio wanaoikwamisha kwa maslahi yao binafsi?

Suluhu ni nini sasa? tuendelee kulialia na kukubaliana na hali au tuchukue hatua kwa kufanya mapinduzi na kuweka tunachoona kinatufaa.
Kila mmoja na mawazo yake, upo huru na fikra zako.

Mama Samia kaja na Reconciliation, Resilience, Reform, Rebuild. Amzazo mimi naamini kama watendaji watazifanyia kazi inavyotakiwa, tutabadilika haraka sana kama nchi.

Reconciliation kwa maana nyingine, tuwache kuwa taifa linaloendeshwa na watu wanaotegemea uchawi na waganga wa kienyeji.
 
Back
Top Bottom