Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,893
- 3,200
Nawasalimu wana jamvi, ni imani yangu mko vizuri kabisa na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya Ujenzi wa Taifa.
Katika utafiti wangu usio rasmi, nimegundua kwamba akili za Watanzania wengi hazina tofauti na akili za kitoto!
Ukimpiga mtoto, ukampatia pipi halafu ukamuuliza aliyekupiga nani, lazima atanyoosha mkono kwa mtu mwingine na siyo wewe uliyempiga!
Haiwezekani matatizo yetu mengi yasababishwe na viongozi wa juu kabisa, halafu lawama zote tuwatwishe watendaji wa chini.
Hatuwezi kutatua matatizo yetu kama Taifa kwa kushughulika na matokeo badala ya kushughulika na kiini cha matatizo hayo.
Ili tuendelee, Watanzania tuachane na akili za kitoto na tuwaambie viongozi ukweli pale wanapotuumiza pasipo kupepesa macho.
Kwa mfano suala la mgawo wa umeme mbona awamu ya 5 lilibaki historia na Watanzania tukasahau mgawo wa umeme kwa muda mrefu?
Kwa mtizamo wangu, Rais wa awamu ya 5, hakupenda ujinga ujinga pale linapokuja suala la maslahi kwa Taifa. Hili la umeme sote tunakumbuka kile alichokisema bungeni kwamba kuna watu wanahujumu miundombinu ya umeme ili tu wanufaike aidha kwa kupewa fedha na wafanyabiashara wa majenereta au kwa kuuza majenereta yao moja kwa moja n.k.
Tuache ujinga, tuwe wazalendo.