ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,964
- 3,895
Suala la kuchukua mikopo ni muhimu na ni Chachu ya Maendeleo ya mtu na biashara yake kiujumla.
Ila Kuna watu hawastaili kuingia kwenye hii mikopo ambayo inasababisha vilio vya Kila siku hasa Kwa kina mama, huku wengi wao wakibaki kutumika kimapenzi bila shurti hasa Kwa mikopo midogo.
Nimekuja kugundua kumbe Kukopa ni ulevi na inaleta uraibu kama ule wa pombe, Kuna jamaa mmoja tunafanya nae kazi ofisini yeye ni Mzee wa Kukopa, mtaani Kila mtu anamdai, ofisi imemkopa, staff wamemkopa, bank mbili zimemkopa, amemshauri na mkewe nae amekopa bank. Huyu jamaa asipokopa anaumwa, ila afadhali huyu ana kazi, Kuna wale wenye biashara ndogo, Kuna ndugu yangu alikufa sukari na presha zilipanda kwakuwa alishindwa kufanya marejesho na lodge zake mbili zikauzwa.
Sasa naona Kuna rafiki yangu wa karibu sana ameshaingia kwenye hii michezo ya Kukopa na ananogewa Sasa hivi anataka akaweke nyumba na hapo awalinalikopa Kwa Kiwanja nikamsaidia kidogo Kiwanja kiende na vimkopo vya sakosi, Sasa anataka kuweka nyumba aende bank kabisa ila naona anapotea, namshaurije.
Hata matajiri wanakopa, ila Kukopa kunakuhitaji uwe na akili mnooo.
Kama unaweza kudunduliza dunduliza usikope, Kukopa Kuna wenyewe wataalamu