Watanzania wengi ni wezi, hatuna uhalali wa kuihoji Serikali

kwakweli huu ndio ukweli mchungu, asilimia kubwa sisi ni wezi na kila mmoja huiba kwa nafasi yake,

mimi nimefanya hata kazi kwenye mashirika ya kimataifa wenye vyeo vya juu kule ni watu wa kenya, uganda, zimbabwe na nchi zingine vyeo vya chini wamewapa watanzania wanaogopa kuwapa vyeo vya juu wataiba,

nimefanya kazi mashirika ya wakimbizi kambi za kigoma kwenye yale mashirika wanaogopa kuwapa vyeo watanzania wakiwatilia mashaka asiyeamini akaangalie mashirika yote yaliyopo kwenye kambi za wakimbizi watanzania wana nafasi gani,

Nimepata kuishi kwenye wilaya flani walikua wanajenga barabara kwa kiwango cha Rami, ndugu zangu watanzania walineemeka kwa wizi wa cement, nondo, mafuta na kokoto, wizi ulikua mkubwa sana watu walijenga mijengo kwaajili ya wizi mpaka mchina alinyoosha mikono, ulikua hata ukiitaji cement ya elfu tano unapata

maofisini kwetu ndio kabisaaa haina haja ya kuuliza, ilifika hadi hatua madereva wa halimashauri wanaenda kupiga nyoka mafuta ya serikali yananyonywa vichochoroni tubadilike tuache wizi,
hebu angalia hii video hapo chini hao Raia nao wana uhalali gani wa kuhoji serikali ilihali nao ni wezi?

Tubadilike jamani
View attachment 1918587
Wazungu wasingekuwa wezi wasingekuwa na neno "thief"
 
Back
Top Bottom