Watanzania Wengi ni Wavivu? The Moment of Truth!

Nadhani mleta mada hii si mtanzania na sijui anasemaje kama tulikuwa na naibu katibu mkuu wa UN mtanzania. Je kazi hakufanya? Vipi kwa wanasiasa wazalendo wanaotaka kutetea taifa na wanalishwa sumu na hao wanaotaka Tanzania iendelee kudharaurika? Kiukweli watanzania kinachowaponza ni utu wao wa kuthamini wageni na sio kitu kingine. Uzalendo wao unawafanya wakubali malipo madogo kwa kuwa hawataki kuvuruga amani. Lakini siku inakuja yatatokea kama ya afrika kusini maana imefika wageni kututukana wakiwa nchini mwetu hapa hasa hawa wakenya na wahindi. Kama mtoa mada sio mzalendo aangalie asije amsha hasira za watanzania hapa.
 
Kinachomsumbua mtoa mada ni mawazo ya kikoloni. Haiwezekani mtanzania mzalendo kuwa na mtizamo wa namna hii tena wakati huu ambao hata wazanzibar wanajadili uwezekano wa kuwazuia watanganyika kwenye ajira katika secta ya utalii ili kulinda ajira zao.

Mawazo yako yananifanya nibashiri kuwa wewe kama si mkenya basi muhindi au mchina au ni kiongozi wa idara ya uhamihaji (umesukumwa na rushwa). Lakini sikushangai sana maana wewe ni sawa na kasuku unafuatisha aliyoyasema PINDA, angalia usimfuate huyo maana hata jina lake linamtambulisha.
 
Tatizo sio uvivu, ila hawalidhiki na wanochokipata kutokana na kazi wanazozifanya(sio wote). Anafanya kazi huku anafikilia kutafuta kazi nyingine, utendaji hauwezi kuwa mzuri. Anaweza kuendelea na hii hali mpaka anasitafu.
 
Tatizo sio uvivu, ila hawalidhiki na wanochokipata kutokana na kazi wanazozifanya(sio wote). Anafanya kazi huku anafikilia kutafuta kazi nyingine, utendaji hauwezi kuwa mzuri. Anaweza kuendelea na hii hali mpaka anasitafu.
hii inakuwa ni vicious circle, chukulia mfano unafanya kazi ya production wakikulipa kidogo una tegea kazi ukitegea kazi production inapungua, production ikipungua hata ule mshahara mdogo uliopata una pungua ukipungua unazidisha uvivu ukizidisha uvivu production inazidi kupungua........................................................ mshahara zero au kufukuzwa kazi
 
Hili ni Tatizo letu watanzania


Tumekua wajinga sana sana kwa POROJO kazi hatutaki na tunapenda matokeo mazuri bila ya deliberate initiatives,

Kusifia watu au Mtu , kushabikia Siasa asubuhi,mchana na usiku that's what we capable of, ila tunashindwa kutumia rasilimali zinazotuzunguka kututalia matatizo yetu kwakua we have chosen to fail, na Kama tungekua wabunifu (creative) basi Leo hii kungekua na mabadiliko makubwa sana nchi I mean across East Africa,

Kwa mfano, Mtu amezungukwa na Mawe lakini anatumia Nyasia na udongo kujenga nyumba wakati nchi za wenzetu Mawe Hadi barabara wamejenga kwa Mawe, nenda Bruxelles, middleburg na France wametumia Mawe, ila huku Mtu anakanyaga vumbi Mawe yamepangana tu, tafsiri yake ni nini,

Ni uvivu na kushindwa kuwa creative kwa kutumia resources zinazotuzunguka kututatulia matatizo yetu mpaka waje wazungu ndio tuamke,


Kwahiyo uvivu tunao kwakua hatuna priorities we as individual forget about government Kwani tumekua tukidhani kila kitu ni Govt ujinga sana....

Ni kwakua hatuna utamaduni wa kujitegemea na huu ni ugonjwa wa kulalamika tunapandikiziwa kusahau mchango wetu binafsi ktk maisha yetu badala yake tunaipa serikali majukumu yetu binafsi na huu ndio uvivu wenyewe...

we mwenyewe unayetoa hoja unalalamika ni mfano mzuri badala ya kulalamika na wewe umeifanyia nini tanzania kwa kutumia hizo rasilimali onyesha mfano kwanza then ulalame
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbali mbali ikiwamo ya Watanzania kulalama kuwa ajira hazipo na zilizopo zinachukuliwa na wageni ama pia kwamba mishahara kati ya watanzania na wageni ina tofauti kubwa. Wakati hayo yote ni kweli issue ya msingi hapa ni kwa nini kuna hali hii. Nachelea kusema Hakuna Taifa masikini lenye watu wavivu, wenye wrong atitude ya kazi kama Watanzania. Mtanzania anaweka bidii kubwa ktk kukwepa majukumu/kazi kuliko juhudi anayoiweka ktk kazi. Mtanzania ni mtu anayehudhuria eneo la kazi na si mwendaji kazini yaani anachojua ni kufika muda mwafaka na kuondoka muda mwafaka bila kujali hapo katikati amekamilisha mangapi (accomplishments of the day). Utamaduni huu ama hulka hii ndio ambyo imemigrate hadi kwa viongozi wa kisiasa wanaolalamikiwa hapa kila mara. Mtu akishapewa cheo anarelax na baada ya miaka mitano dhamira haimsuti juu ya nini alichokikamilisha kwa dhamana aliyopewa. Tutaendelea kuwa rejects za soko la ajira mpaka pale tutakapoamua kuua tabia hii. Hakuna mwajiri asiyetaka uzalishaji ndo mana wengine wanaona bora walete wageni wawalipe juu lakini wajihakikishie uzalishaji.
umekosa kazi? hizo ni lugha za wasiasa uchwara
 
Watanzania sisi sio wavivu ila hatuna cha kufanya.
Kwanza watanzania waajiriwa hawana kazi mbali na walizoajiliwa nazo, ikifika saa kumi jioni ofisi zote zimefungwa Bar zinafunguliwa, zingetokea kampuni ambazo zinaweza kuajili watu kupitia mitandao na hivyo baada ya saa za kazi mtu anaweza kuajiliwa kwa muda kupitia mtandao kama nchi za wenzetu ingepunguza umaskini wa waajiriwa, Ombi kwa wamiliki wa kampuni waanze kuangalia uwezekano wa kuajili watu kupitia mitandao.

Pili, Fursa za biashara zinaondolewa mfano nilitegemea baada ya sisi wafanyabiashara wa ubungo kuondolewa tungepewa eneo la pale TBS na TBS ihamishwe sehemu nyingine ili tusionekane wavivu na kwa kuwa tutalipa kodi ya biashara hivyo gharama ile itasaidia kulipia ofisi za TBS huko watakapohamia.

Tatu, Watu binafsi wanunue viwanja na wavikodishe kwa wafanyabiashara wadogo
 
Mhhh kuna kaukweli ukweli hapo ndo maana tuko nyuma ktk nyanja nyingi za kimaendeleo..kuanzia sanaa..siasa...biashara...kilimo...michezo...kasoro wizi kidogo tumepiga hatua
 
kwa hakika mkuu umenena kamili,sisi watz hatuna la kufanya kampuni zote zinamilikiwa na wakenya au wa africa kusini asilimia 3 iliobaki inamilikiwa na wachagga
 
kwa hakika mkuu umenena kamili,sisi watz hatuna la kufanya kampuni zote zinamilikiwa na wakenya au wa africa kusini asilimia 3 iliobaki inamilikiwa na wachagga

@Nairoberry, mara hii naona umeibukia huku kama Mtazania. Still with stupid?

:nimekataa
 
Naomba mimi na team yangu ututoe kabisa kati ya hao Watanzania wako....halafu usiwaponze wanaotafuta kazi wakakosa ajira kwa utafiti uliofanya hapo ofisini kwako pekee...
 
Changieni basi, nyie wa wapi nyie????????????

mkubwa punguza hasira, una mawazo mazuri ila hilo la watu wakubwa wanunue viwanja wakodishe kwa wafanyabiashara wadogo haipo njema, kwanini hao wafanyabiashara wasijiorganize wakanunua hivyo viwanja?
 
Siyo kweli! NG'OMBE mlishe mashudu ya kutosha, mpe matibabu sitahiki, tengeneza banda lake liwe safi, harafu angalia maziwa utakayomkama ng'ombe huyo.
 
Back
Top Bottom