Watanzania Wengi ni Wavivu? The Moment of Truth!

Uvivu wa wafanyakazi katika serikali kuu inatokana na dhana kuwa ukishaajiriwa huwezi kufukuzwa.

Wafanyakazi wa serikali wana tabia ya urasimu a.k.a umangimeza (Bureaucrasy).

Pia wafanyakazi wa serikali hawajibu barua au email za watu yaani wanaogopa kutoa information 'conservativu' - Ila ukienda physically unatoa chochote na information unapewa.

Unakuta mfanyakazi amekalia ofisi na hataki mtu mwingine aguse kitu, na yeye hataki kufanya kazi. Ukiwa mbunifu ndo unakuwa adui.

Unakuta watu wameajiriwa miaka ya 1970 - 1980 na hawataki ajira zitoke kwa vijana wa Vyuo Vikuu.

Serikali yetu imelala fofofo, ni tofauti na KENYA, ZANZIBAR, South Africa, USA, UK. Hawa ukiwaandikia email unapata majibu in 72 Hours maximum.

Sasa hapa kwetu Tanzania utangoja mwezi mzima na hupati majibu, ukipiga simu hamna jibu. Ukienda mwenyewe na Rushwa yako mkononi unapata kila kitu.

Tunakwenda wapi Tanzania?

Kwenye red hapo upo sahihi kabisa.
 
Ukiwa una compare Tanzania na nchi jirani kama kenya ama Uganda ama Rwanda utangundua kua watanzania ni wavivu kwa asilimia kubwa sana tofauti na mataifa mengine.

kunasiku Mkapa alitoa hii kauli lakini watu walimshambulia sana , lakini mimi naamini ukweli una uma na ndio maana walimshambulia. watanzania tunapenda kupiga stori tunapenda kushadadia mambo na tunachukia mambo ya kuumiza akili.

mfano mdogo tu ni unaweza kuta kijana ni graduate lakini eti ana kaa nyumbani akisingizia hana kazi na anasubiri mpaka eti kazi zitangazwe na ndipo afanye application. huyu kijana angeweza kufanya kazi yakujitolea hata sehemu yeyote ambayo ingemsaidia hata kupata kujuana na watu zaidi na hata kua na experience zaidi lakini ana oana haina maana kama kukaa nyumbani.

mfano mwingine una kuta mtu kaajiriwa ofisini lakini kufanya kwake kazi mapaka asukumwe mara kwamara . Napenda sana wakenya wanavyo fanya kazi wko so smart na hakuna mchezomchezo mara viruhusa vya hapanapale mara hayupo offisini. kusema kweli East Africa community ita tufanya tuwe watumwa wakenya kama tusipo angalia nafasi zote nyeti zitashikwa na wakenya na sisi tutabaki tunapiga kelele za umbeya na ushabiki.

Hii issue ilitokea south Africa ambapo wazungu walikua wana waajiri watu ambao walikua wanaona wana weza fanya kazi na baada ya muda ikawa wa south afrika wengi hawapo kwenye nafasi zajuu, ndo ikaja ile vita ya wahamiaji.

ukiongelea mambo ya siasa Tanzania utapata mashabiki kibao lakini ongelea swala la kumputer imetengenezwa vipi ama gari limetengenezwa vipi ama ni lini nasisi tutakua na kiwanda chetu. kusema kweli unaweza usipate mchango wowote. angalia tu ishu ya kanumba ilivyo chukua mudamrefu ikiongelewa lakini sijawahi sikia hata sikumoja kitu chochote chauvumbuzi kikiwa kinaongelewa hata kwa sikumoja.

Jamani Tanzania tubadilike tufanye kazi tuachane na uvivu. sisemi tusiongelee siasa kabisa hapana namaanisha kua angalau tuwe pia na vitu vyauvumbuzi amabavyo vitatuzaidia
 
Kiufupi: Mfumo uliopo unaoruhusu watu kupata mali kiujanja ujanja bila kutumia njia halali au hata kuwa na faida kwa nchi, na hizi tamaduni zetu za kiafrika za kulindana lindana kufugana hata mtu anayejiweza kufanya kazi ndiyo zinawafanya watu wengi waendelee kusota mjini hata kama hana inshu ya maana.
 
sio kweli labda useme hawajui sana,uwezo wa kuelewa ni mdogo,hata wewe hapo uwezo wako ni mdogo,mkuu nipo arusha,wakenya wengi wakija hapa wanafungua ofisi na kufanya kazi,sio kwamba watanzania hawawezi kufungua ofisi kama hizo,ila ni uwezo wa kugundua mambo bado upo chini kidogo
 
mikonomiwili,

Nakuunga mikono miwili wacha mmoja.

Watanzania ni wavivu wa kutupwa. Makazini kila siku visingizio, leo kafa shangazi, kesho mjomba, kesho kutwa jirani, mtondo bibi.

Wote huo ni uvivu tu. Sasa wakifa ukienda wewe ndio watafufuka? kaa kazini ukimaliza muda wako wa kazi nenda. Ukiwaambia hivyo wanakwambia "huna imani". Sasa imani kwenye kifo?

Ndio maana hatuendelei. Ni mfumo mbaya wa kuwa kila kitu cha umma ndiyo umeua uwajibikaji.

Mijitu imekaa inataka kufanyiwa tu, viongozi wafanye hivi viongozi wafanye vile.

Mimi ningepiga marufuku hawa wagombea ubunge na wabunge wote kujidai kwenda kupeleka sijui mabati, sijui simenti, Huu mfumo ndio unauwa uwajibikaji na unaendeleza uvivu.

Leo unakuta kijiji kinauza mbao lakini hakina madesk kwenye shule zake. Huu ni uvivu wa hali ya juu.
 
Huo uwezo wakugundua mambo unaosema ni mdogo ndo uvivu wenyewe. sisi tunapenda viwe tayari hatupendi kubuni vyakwetu ama kufikiria kubuni vyakwetu. Nakisingizio kikubwa ni kua eti hatuna hela . issue sio hela wala nini nikua ni wavivu wakufikiri .

ndugu uvivu sio wakutumia nguvu tu hata mtu kuachakukaana kubuni shuhuli yake ni uvivu pia. unkiangalia maranyingi tukiona mtu kajenga kibanda cha saloon na wewe unaenda kuweka kibandakama kile palepale bunichakwako weka kitu tofauti hata kamautanza kidogokidogo baadae utaibuka.

nilienda hoteli moja mwanza nihoteli kubwatu lakini hudumazao nimbaya sana yaani mbaya unaagizakitu mpaka uletewe niamasaa na ukiletewa kiwangochake ni chachini sana . sasa huo nini kama sio uvivu wakufanya kazi.

tujikwamue kwenye hii kitu jamani tuachevisingizio lasivyo tutakua watumwa.
 
Ni kweli sisi wavivu sana, unakuta bwana mdogo ameanza kazi mpya mpya ana miezi miachache tu lakini akienda lunch hadi bosi wake aanze kumpigia simu anamtafuta yupo wapi :thinking:
 
Hata kidogo Watanzania Sio Wavivu Siasa Zetu zimetufanya kuwa watulivu sana mpaka Mnadhani ni Wavivu

Toka wewe Umezaliwa Umesha wahi kuishi bila chakula? labda bila pesa lakini ukilinganisha na hizo nchi ulizozitaja zote

zina matatizo ya Vyakula, Sisi ng'atu hata kidogo pamoja na wao kuwa na big farmers kama Kenya.

Ukiangalia hizo Nchi zilikuwa zinaendeshwa kibepari, sisi tulikuwa wasocialist hapo labda tulikuwa tunazuia Maendelea au

Ubunifu wa Wafanya Biashara wadogo lakini Sio Uvivu. HATA KIDOGO WATANZANIA SIO WAVIVU; LABDA WEWE!!!
 
Ni kweli sisi wavivu sana, unakuta bwana mdogo ameanza kazi mpya mpya ana miezi miachache tu lakini akienda lunch hadi bosi wake aanze kumpigia simu anamtafuta yupo wapi :thinking:

Hiyo ni individual case by case, hata wewe umejua huyo jamaa ni mvivu na Boss wake kwanini asimfukuze? kwani huyo ni mtoto wa Mkubwa?

Kuna Sheria zinazofuatwa kwa watu kama hao lakini sio wote nchi nzima.
 
Ukiwa una compare Tanzania na nchi jirani kama kenya ama Uganda ama Rwanda utangundua kua watanzania ni wavivu kwa asilimia kubwa sana tofauti na mataifa mengine.

kunasiku Mkapa alitoa hii kauli lakini watu walimshambulia sana , lakini mimi naamini ukweli una uma na ndio maana walimshambulia. watanzania tunapenda kupiga stori tunapenda kushadadia mambo na tunachukia mambo ya kuumiza akili.

mfano mdogo tu ni unaweza kuta kijana ni graduate lakini eti ana kaa nyumbani akisingizia hana kazi na anasubiri mpaka eti kazi zitangazwe na ndipo afanye application. huyu kijana angeweza kufanya kazi yakujitolea hata sehemu yeyote ambayo ingemsaidia hata kupata kujuana na watu zaidi na hata kua na experience zaidi lakini ana oana haina maana kama kukaa nyumbani.

mfano mwingine una kuta mtu kaajiriwa ofisini lakini kufanya kwake kazi mapaka asukumwe mara kwamara . Napenda sana wakenya wanavyo fanya kazi wko so smart na hakuna mchezomchezo mara viruhusa vya hapanapale mara hayupo offisini. kusema kweli East Africa community ita tufanya tuwe watumwa wakenya kama tusipo angalia nafasi zote nyeti zitashikwa na wakenya na sisi tutabaki tunapiga kelele za umbeya na ushabiki.

Hii issue ilitokea south Africa ambapo wazungu walikua wana waajiri watu ambao walikua wanaona wana weza fanya kazi na baada ya muda ikawa wa south afrika wengi hawapo kwenye nafasi zajuu, ndo ikaja ile vita ya wahamiaji.

ukiongelea mambo ya siasa Tanzania utapata mashabiki kibao lakini ongelea swala la kumputer imetengenezwa vipi ama gari limetengenezwa vipi ama ni lini nasisi tutakua na kiwanda chetu. kusema kweli unaweza usipate mchango wowote. angalia tu ishu ya kanumba ilivyo chukua mudamrefu ikiongelewa lakini sijawahi sikia hata sikumoja kitu chochote chauvumbuzi kikiwa kinaongelewa hata kwa sikumoja.

Jamani Tanzania tubadilike tufanye kazi tuachane na uvivu. sisemi tusiongelee siasa kabisa hapana namaanisha kua angalau tuwe pia na vitu vyauvumbuzi amabavyo vitatuzaidia
hilo ni sahihi kabisa.sio huko vijiweni tu hata hapa JF pia.mijadala ya siasa inawachangiaji wengi sana.jamaa mmoja aliwahi niambia tz inaongoza kwa wasomi wa political sciance kuliko taaluma zingine.
 
Nafikiri umezingatia ngazi zote - kuanzia uongozi wa nchi mpaka ule wa familia!
 
Hii statement iko general sana na haitoi picha halisi ya watanzania wengi. Kwa sababu umeongelea graduates basi ningependa kuamini unaongelea vijana walio mijini. Lakini kumbuka 80% ya watanzania wanaishi vijijini. Wanajilisha wenyewe, wanalima na kulisha huku mijini tena kwa kutumia jembe la mkono. Sasa hivi Mbeya wakulima wanalia, mazao yanaozea ndani, je, nani alilima hayo mazao, Wakenya?

Serikali hii inayomiliki magari ya Tshs 5 trilion imeshindwa kujenga reli ya uhakika ili watu wasafirishe mazao yao kuja mijini! Hapo utamlaumu nani? Na mbaya zaidi, serikali inapiga kelele kuhusu kilimo kwanza lakini ni lini serikali hii ilikaa chini na watu wa vijijini na kujadili namna bora ya ku-implement kilimo kwanza? Matreka na power tillers ziko Dar, hela za kukopesha wakulima zimepelekwa TIB ambayo iko Dar, hata watu wa utabiri wa hali ya hewa wamejikita kutoa taarifa za mvua kwa watu wanaoishi mabondeni huku Dar. Wakulima wanaagalia mawingu kama 1800!

Kwa kifupi watu wanaolisha hii nchi ni watanzania 80 % waliotelekezwa na serikali ya CCM. Year in year out, wakubwa wapanga mipango hapa Dar, wanaitekeleza kwa sytle wanayotaka hapa hapa Dar, wakulima wamebaki kama yatima.

Lingine linaifanya nchi hii iwe kama kichwa cha mwenda wazimu ni 'weak industrial base' Wakubwa wameua viwanda na badala yake wamejigeuza mawakala wa viwanda vya nchi za nje. Kiwanda cha maziwa Arusha kimeuzwa kwa WaKenya, na matokeo wameng'oa hata mitambo na kupeleka kwao Kenya. Watanzania wamekosa ajira huku wakenya wakipata ajira. Tanganyika parkers haipo, kiwanda cha ngozi kimekufa, na ukitaka kuanzisha 'cottage industry (kiwanda kidogo) utakuta kuna mkubwa ana tenda ya vitu kama hivyo kwa bei chee toka China. Kwa mazingira haya huwezi ku-encourage watu waanzishe viwanda maana hakuna mkakati maalum wa kuwalinda. Na bado CCM wanataka kubaki madarakani!
 
mikonomiwili,

Nakuunga mikono miwili wacha mmoja.

Watanzania ni wavivu wa kutupwa. Makazini kila siku isingizio, leo kafa shangazi, kesho mjomba, kesho kutwa jirani, mtondo bibi.

Wote huo ni uvivu tu. Sasa wakifa ukienda wewe ndio watafufuka? kaa kazini ukimaliza muda wako wa kazi nenda. Ukiwaambia hivyo wanakwambia "huna imani". Sasa imani kwenye kifo?

Ndio maana hatuendelei. Ni mfumo mbaya wa kuwa kila kitu cha umma ndiyo umeua uwajibikaji.

Mijitu imekaa inataka kufanyiwa tu, viongozi wafanye hivi viongozi wafanye vile.

Mimi ningepiga marufuku hawa wagombea ubunge na wabunge wote kujidai kwenda kupeleka sijui mabati, sijui simenti, Huu mfumo ndio unauwa uwajibikaji na unaendeleza uvivu.

Leo unakuta kijiji kinauza mbao lakini hakina madesk kwenye shule zake. Huu ni uvivu wa hali ya juu.
uzalendo unalazimishwa mkuu uliza marekani na china kwa hiyo viongozi wako ndo wameshindwa kuongoza vyema wananchi wao!
 
hilo ni sahihi kabisa.sio huko vijiweni tu hata hapa JF pia.mijadala ya siasa inawachangiaji wengi sana.jamaa mmoja aliwahi niambia tz inaongoza kwa wasomi wa political sciance kuliko taaluma zingine.
Hili ndo tatizo mkuu kuwa na mi HR kibao halafu inakuwa na akili za wizi tuuu!
hii ndo inaongoza kwa uvivu na ulevi!
 
Dah asante sana kwa kuongelea hii kitu...watz ni wavivu sisi ni wavivu sana compared na nchi zingine. Mtu anaingia asubuhi kazini yuko kwenye facebook siku nzima afu anatamba ana kazi. Ingia kwenye bank ndio kabisa utataka kumpiga mtu vichwa.. unakuta mashosti wako kila mtu na meza yake wanapiga story za mabwana zao wakati we mteja umekaa pale unasubiri huduma.. Wengine wanaingia wana sign in wanatoka huwaoni tena...na kuna wale lunch hour wanafanya lunch 3hrs...mwajiri wako amekupa lisaa lizima lunch yeye anakula lunch 3hrs.. Wa kenya siwapendi lakini wanachapa kazi sana.

Juzi nilikua naongea na MD mmoja hivi sitataja kampuni akawa ananiambia kua amechoka kuwaajiri watanzania sasa hivi akitaka mtu anatafuta wakenya au analeta wazungu coz kampuni yake headquarters ziko ulaya..nilijisikia vibaya bt ndio akaniambia hana jinsi kwa sababu performance ya wabongo ni mbaya mno kampuni yake haiperform vizuri. ITS A SHAME
 
Mvivu ni wewe baba yako mama yako wajomba zako na jirani zako!
Watanzania wanafanya kazi sana tena sana, tunayo mifano mingi tu ya utendaji mzuri wa watanzania nchini tanzania. Tatizo lililopo ni mifumo mingi haijakamilika ya kitechnolojia ya kuweza kubaini nani anafanya kazi nani hafanyi kazi. Mfano we nenda ofisi nying ulaya utakuta ukiingia ofisini kuna sehemu unagusisha kadi, na inaerkodi muda, the ukitoka hivyo hivyo na hii inapelekea hata hao unaowaita wanafanya kazi kuwa wafanya kazi hata kama ni wavivu. Nakupatia mfano mwingine, nchi kama Norway wafanyakazi wanalindwa na sheria nyingi sana, wavivu wengine hutumia hizo sheria zinazowalinda kuchkua likizo ya ugonjwa hata mwaka mzima, na huyo mvivu anaendelea kulipwa mshahara wote kwa kipindi chote, je naye utamuitaje?? Usijilinagnishe na kenya hao ni mabebari, mifumo ya mabebari ni unyonyaji, kazi kubwa anakulipa msharara kidogo ili uendelee kumtumikia. Tanzania ni nchi yenye neema na watu wake ni wema na wanachapa sana kazi! nenda sehemu ambazo watanzania wameajiliwa kama Barrick uone kazi, nenda hata Bank of africa uone, acha ujinga kijana wa kuwadharau watanzania!!
 
Watanzania wanafanya kazi bhana,,,sasa mtoa mada ukitaka kuamin wanafanya kazi angalia kundi la vijana na akina mama wanaohangaika kuitafuta pesa barabarani as wamachinga,nenda bugurun,nenda tandale nenda tandika angalia mijini vijana wanavyohangaika na wamachinga....twende vijijin kuna jamaa amekwambia vizuri tu hapo juu kwamba huko vijiji kuna watu wanapiga kazi mdau acha tu,,,,
twende kwa graduates,hawa jamaa bwana wanakabiliwa na changamoto nyingi,hasa mfumo wa elimu lakini pia mitaji,,,amemaliza shule ana shahada ya ujasiriamali lakini hana mtaji,ameandika business plan lakin hana assets za kumfanya apate mkopo,,,pia tatizo la kupata information...HILI NALO NI TATIZO KUBWA SANA,,,,VIJANA WA KITANZANIA KWAKWELI TUNA TATIZO LA KUPATA TAARIFA,,,,WAPI KUNA NINI NA KIAS GANI
 
Watu wanafanya kazi bana angalia mashamba wanavyohangaika kulima wakishapata mazao serikali inapanga bei lakini wakati huo serikali imesema soko huria nafikiri hujasikiliza bungeni wanavyolalamika kuhusu pembejeo na mbolea srikali inaleta feki hata mbegu pia feki.
Kuna vitu vinachangia uvivu uwe umesoma mnafanya kazi mahali hakuna mpangalio tena siku hizi kuhusu mishahara unaweza kuwa form six ya 1990 ukaanza kazi lakini atakuja wa form 4 akaanza kufanya kazi 2011 na wewe lakini amekuzidi mshahara....angalia mikopo ukitaka hata kama una vitu vyote lakini lazima uhonge kila mahali ..
angalia kilimo kwanza hakuna cha maana zaidi ya maneno ya viongozi angalia matrekta yalio letwa yapo yamepaki kwenye halimashauri yamekaa tu
 
Back
Top Bottom