Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,303
- 144,624
Yeah,
Ukiwa na risiti is an added layer of verification, perhaps hata kupata rekodi nyingine ikawa rahisi. Ukitaka kuangalia reel ya surveillance kama una risiti unaweza kujua muda uliolipa.
Kuna jamaa alikuwa kapewa kesi akasema muda huo alikuwa kwenye subway, alikuwa na monthly subway card ambayo alikuwa anatunza risiti yake in case ikipotea aweze kui cancel na kuipata nyingine, akawa kapoteza metrocard lakini risiti anayo.
Akaenda kwenye shirika la usafiri waka verify kwamba alinunua ile card, na ilikuwa inatuumiwa kila weekday kwa pattern ile ile, na siku hiyo ya uhalifu ilitumiwa. Not a foolproof defence, lakini inajenga defence kuliko mtu ambaye hana ushahidi wowote.
Juzi nimejipindua kwenda kununua DVD-R, basi nilikuwa nawahi kurudi home kuna mshkaji alikuwa anakuja home. Sikuangalia vizuri lile stack, kumbe nikawa nimechukua CD-R. Nikazipark kwenye basement lab for a few days, kuja kuangalia ni CD-R. Partly nikataka nizirudishe, partly nikasema niziache tu niende kuchukua DVD-R. Nilichukua risiti lakini nikawa sizioni tena. Nikaona nipotezee tu niende kichukua DVD-R stack nyingine.
So kuna umuhimu sio tu wa kuchukua risiti, bali kuzitunza pia.
Kuna watu wengi kwa mfano, wanatoa michango kwa organizations -mfano 501 (c) ambazo ukipata risiti ile michango unaweza kurudishiwa na serikali (Marekani)
Organizations Eligible to Receive Tax-Deductible Charitable Contributions
Mimi nina file kabisa la risiti za purchases mbalimbali ambazo huwa nazitunza walau kwa miezi kadhaa.
Na kama ulivyosema ukiwa na risiti verification process inakuwa rahisi zaidi.
Halafu siku hizi department stores kama Nordstrom, Macy's na zinginezo hata kama huna risiti na ulinunua kwa kutumia kadi unaweza kuirudisha merchandise na ukapewa full refund yako tofauti na zamani ambapo kama huna risiti basi unapewa in-store credit au unakataliwa kabisa.
Unapoitumua kadi yako kwenye hizo stores inaacha rekodi zake. Hivyo ukienda info zinakuwa retrieved kirahisi. Ni wazi utahitaji kuonyesha kitambulisho ndipo upewe refund yako.
Halafu nahisi kama vile itafikia wakati watu tutakuwa tunatembea na kadi moja tu yenye QR code ambayo inaweza kutumiwa sehemu mbalimbali.
Sasa hivi nimeona hata baadhi ya airlines zimeshaanza kutoa tiketi kwa kutumia QR codes.