Watanzania wengi hawachukui Stakabadhi (Risiti)

Watanzania wengi hawachukui Stakabadhi (Risiti)

wa hapahapa

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
7,460
Reaction score
4,404
Stakabadhi hutolewa baada ya kununua huduma au bidhaa.

WanaJFamiiForums, ni kwanini Watanzania wengi hawajali umuhimu wa stakabadhi!?
 
stakabadhi hutolewa baada ya kununua huduma au bidhaa.

wana JF,
ni kwanini watz wengi hawajari umuhimu wa stakabadhi !
Kwa mimi binafsi sioni sababu ya kutochukua risiti ninaponunua bidhaa ila Mara nyingine nikiwa na haraka huwa sichukui .
 
Mara nyingi wabongo tunapenda kudai punguzo la bei na wauzaji wanachokifanya ni kutoa gharama za VAT kisha kukupa punguzo.

Hivyo ukinunua bidhaa na ukadai stakabadhi basi muuzaji atataka uongezee asilimia kumi na nane ya malipo uliyompatia ili akupe hiyo stakabadhi ya malipo.
 
Sababu wengi hawapangi hesabu za matumizi yao.
Ila kwa mie Risiti ni ya umuhimu sana
 
mauzo\manunuz pasipo stakabadhi..
inasaidia mfanyabiashara asilipe kodi husika.

hivyo taifa linapoteza mapato..
 
nashangaa sana tiket za daladala hazina namba ya tiket...
zile tiket ni bandia lkn abiria wanashindwa kujua/kuhoji.
 
Kuna mchizi alikuwa na tabia ya kuchukua stakabadhi kila sehemu.

Kuna siku akawa anaendesha gari masafa marefu kwenye highway US.

Trafiki wakajipindua wakambabatiza speeding ticket.

Kwenda mahakamani akaenda na ticket za toll zote anaonesha hapa nilipita muda huu, hapa nikapita umbali huu, hapa nikapita umbali huu, umbali wa pote hapa ni huu, muda niliotumia ni huu, kama ningekuwa nakwenda zaidi ya speed iliyowekwa nisingefika humo nilipofika kwa muda huo.

Jaji akaona jamaa ana make sense na polisi wamembabatiza tu.

Risiti zinaweza kukusaidia kitu ambacho kinakuja mbeleni hata kama hujakijua.

Unaweza kupewa kesi ya mauaji, ukaulizwa muda huu ulikuwa wapi? Ukasema nilikuwa restaurant nakula peke yangu.

Ukiwa huna risiti kushawishi ni vigumu. Kama una risiti unaionesha na inaku link na uhakiki wa kauli yako.
 
Unaweza kuoeea kesi ya mauaji, ukaukizwa muda huu ulikuwa wapi? Ukasema nikikuwa restaurant nakula peke yangu.

Ukiwa huna risiti kushawishi ni vigumu. Kama una risiti unaionesha na inaku link na uhakiki wa kauli yako.

Kwenye scenario kama hiyo hata kama huna risiti kuna vitu vingine vinavyoweza kukutoa hatiani.

Mfano, kama ulilipia kwa kuchanja credit au debit card basi lazima time stamp itakuwepo kwenye moja ya paper trail, iwe kwenye back end or front end.

Juu ya hilo, kama ni kiwanja, migahawa mingi sana ina surveillance cameras.
 
biashara nyingi kimfumo hazipo rasmi.

mf. muuza genge au machinga kamwe uwezi kumkuta na stakabadhi..
 
Kwenye scenario kama hiyo hata kama huna risiti kuna vitu vingine vinavyoweza kukutoa hatiani.

Mfano, kama ulilipia kwa kuchanja credit au debit card basi lazima time stamp itakuwepo kwenye moja ya paper trail, iwe kwenye back end or front end.

Juu ya hilo, kama ni kiwanja, migahawa mingi sana ina surveillance cameras.

Your right Mkuu NN kwa mazingira uliyopo

Najaribu kuwaza huku kwetu Kwentengwe

All in all wote tuna tatizo....kuanzia wafanyabiashara kutoa risiti mpaka wanunuzi kuchukua receipt...

Hao TRA nao usijidanganye kwenda kupeleka kesi ya mfanyabiashara ambae hajakupa receipt, unaweza kuwa unapeleka kesi ya nyani kwa Tumbili.....
 
Kwenye scenario kama hiyo hata kama huna risiti kuna vitu vingine vinavyoweza kukutoa hatiani.

Mfano, kama ulilipia kwa kuchanja credit au debit card basi lazima time stamp itakuwepo kwenye moja ya paper trail, iwe kwenye back end or front end.

Juu ya hilo, kama ni kiwanja, migahawa mingi sana ina surveillance cameras.

Yeah,

Ukiwa na risiti is an added layer of verification, perhaps hata kupata rekodi nyingine ikawa rahisi. Ukitaka kuangalia reel ya surveillance kama una risiti unaweza kujua muda uliolipa.

Kuna jamaa alikuwa kapewa kesi akasema muda huo alikuwa kwenye subway, alikuwa na monthly subway card ambayo alikuwa anatunza risiti yake in case ikipotea aweze kui cancel na kuipata nyingine, akawa kapoteza metrocard lakini risiti anayo.

Akaenda kwenye shirika la usafiri waka verify kwamba alinunua ile card, na ilikuwa inatuumiwa kila weekday kwa pattern ile ile, na siku hiyo ya uhalifu ilitumiwa. Not a foolproof defence, lakini inajenga defence kuliko mtu ambaye hana ushahidi wowote.

Juzi nimejipindua kwenda kununua DVD-R, basi nilikuwa nawahi kurudi home kuna mshkaji alikuwa anakuja home. Sikuangalia vizuri lile stack, kumbe nikawa nimechukua CD-R. Nikazipark kwenye basement lab for a few days, kuja kuangalia ni CD-R. Partly nikataka nizirudishe, partly nikasema niziache tu niende kuchukua DVD-R. Nilichukua risiti lakini nikawa sizioni tena. Nikaona nipotezee tu niende kichukua DVD-R stack nyingine.

So kuna umuhimu sio tu wa kuchukua risiti, bali kuzitunza pia.

Kuna watu wengi kwa mfano, wanatoa michango kwa organizations -mfano 501 (c) ambazo ukipata risiti ile michango unaweza kurudishiwa na serikali (Marekani)

http://www.irs.gov/Charities-&-Non-...ceive-Tax-Deductible-Charitable-Contributions
 
migahawa na hosptali binafsi nyingi ni nadra sana kutoa stakabadhi baada ya kutoa huduma.

wanawekaje kumbukumbu zao !.
 
Back
Top Bottom