PauliMasao
JF-Expert Member
- Nov 26, 2007
- 286
- 39
Hii yote ni kwa sababu Precisionair wana monopoly ya usafiri wa anga hapa Tanzania. Si mara ya kwanza abiria kucheleweshwa, imagine mtu unaamka saa kumi na nusu alfajiri ili uweze kuondoka saa moja asubuhi halafu unaambiwa utaruka saa tano asubushi! huu ni uhuni mtupu. Nimechoshwa na hawa Precisionair, kwanza bei ya kusafiri peke yake inanitia kichefuchefu. Kusafiri from KIA to Dar na kurudi ni zaidi ya Tshs. 370,000/- kwa mtu halafu unakumbana na matusi kama haya. Sijui ni lini hawa Precisionair watapata competitors, nasikia airline zingine zikitaka ku - operate hapa TZ wanafanyiwa mizengwe ili wasipewe leseni, na hata wakipewa leseni huzuiwa ku-operate kwenye route za Precisionair! Hivi ingelikuwa ni airline ya kizungu wangewashusha waafrika kweli, bila kuzingatia ethics za biashara?