Watanzania washushwa ndege ya Precision Air | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania washushwa ndege ya Precision Air

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Che Kalizozele, Nov 29, 2009.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  na Ramadhani Siwayombe, Arusha
  ZAIDI ya abiria 15 raia wa Tanzania waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision Air kutoka Arusha kuelekea Dar es Salaam wameshushwa na kupakizwa raia wa kigeni.

  Tukio hilo lilitokea jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kusababisha mtafaruku uliodumu kwa zaidi ya dakika 30 kabla ya walinzi wa uwanja huo kuingilia kati, ili kutuliza hali hiyo kutokana na abiria hao kugoma kushuka.

  Wakizungumza na Tanzania Daima uwanjani hapo, abiria hao wamedai kuwa, kitendo cha kuteremshwa katika ndege waliyopanda na kupakizwa abiria wengine ambao ni raia wa kigeni (Wazungu) bila kuelezwa sababu za msingi ni cha ubaguzi wa hali ya juu.

  Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa abiria aliyekumbwa na kadhia hiyo, Pamela Msuya, mkazi wa Dar es Salaam, alisema dakika chache kabla ya ndege kupaa hewani, rubani alizima injini ya ndege na wahudumu kuwaeleza kuwa kumetokea dharura, hivyo hawataweza kupaa.

  Alisema kutokana na hali hiyo, waliombwa kusubiri hadi saa 5:40 asubuhi. Awali walikuwa waondoke na ndege hiyo saa 1:00 asubuhi.

  Abiria huyo alieleza kuwa, ilipofika saa 5:40 waliingia katika ndege na rubani kuiwasha, lakini ilizimwa tena na kuamriwa kuteremka kwa maelezo ndege hiyo ilipaswa kupakia abiria wa Zanzibar ambao ni raia wa kigeni.

  Pamela aliendelea kudai kuwa, wakiwa wanashushwa katika ndege hiyo, baadhi ya abiria waligoma na kusababisha kutokea kwa mtafaruku mkubwa wa zaidi ya dakika 30 kabla ya walinzi wa uwanja huo kuitwa na wahudumu wa ndege hiyo na kwenda kuwashusha huku wakiwaita wazamiaji.

  “Si siri, tumedhalilishwa sana, yaani tunaitwa wazamiaji mbele ya wageni, watatuelewaje? Tuna booking ya muda mrefu tofauti na hao (raia wa kigeni),” alisema Pamela.

  Baada ya kushushwa abiria hao, wengine ambao wengi ni raia wa kigeni, walionekana wakipanda ndege hiyo kuelekea Zanzibar.

  Abiria mwingine ambaye hakupenda kutaja jina lake gazetini, alisema alishangazwa na kitendo hicho kutokana na abiria hao (wazungu) kutokuwa na taarifa za usafiri (booking) na kwamba walifika muda huohuo na kupatiwa usafiri.

  Aliongeza kuwa, baadaye waliambiwa kuwa wasubiri ndege ya saa 11:00 jioni ambayo itawapeleka jijini Dar es Salaam.

  “Tulishushwa tukaambiwa tusubiri ndege ya saa tano, tukavumilia na muda huo ulipofika tena wakatuambia tusubiri ya saa 11. Huu si uungwana hata kidogo,” alisema abiria huyo.

  Baada ya jitihada za kupata uongozi wa shirika hilo kugonga mwamba, mmoja wa wafanyakazi wa Precision Air mkoani Arusha ambaye alikataa kutaja jina wala cheo chake, alisema kwa kifupi tatizo hilo linashughulikiwa, na alipoulizwa zaidi aliwataka waandishi wa habari waende katika Uwanja wa KIA.

  “Nimeshawaambia tatizo linashughulikiwa, kama mnataka zaidi nendeni KIA,” alisema mfanyakazi huyo.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  Hii kitu imeniuma saaaaaaaaaaaana!!! nitakukana matusi mimi *****(*)(*&(^%$#%$^^^^^^^^^$%$%&^%$^%&^ zao.haiingii akilini ningekuwa mkubwa hapa nigewajibisha watu.
   
 3. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Miafrika ndivyo ilivyo...NN
   
 4. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Yaani sijui sisi tutaelimike lini,utafikiri unapanda bure bwana!!!!!Kama haitoshi bado mnawapotezea watu muda wao achilia mbali ya usumbufu mliowasababishia.Sijui hao wazungu waliwapa kiasi gani cha pesa mpaka wakawa tayari kuwadhalilisha watanzania wenzao kiasi hiki.HALAFU kwa staili hii mnataka tuyaunge mkono makampuni yetu,ni mara kumi ukaingia gharama kubwa lakini ukawa na uhakika na unachokifanya kuliko UBABAISHAJI HUU.
   
 5. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Waafrica wataacha lini kujiona wao ni second class na kupapatikia wazungu?
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Tukiitwa wapumbavu tunakataa, na ajabu ni kuwa inawezekana hii issue itaishia kwenye carpet tu hakuna atakayechukuliwa hatua na wala precision air haitachukuliwa hatua. Ni kama hakuna mtu wa kutetea utu na heshima ya mtanzania.
  This is how niggers are. Nyani ngabu where are you???
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  wablack i mean atz tuna akili fupi sana wangejua huku mizungu inavyotubagua kila sehemu huku kwao halafu hadi kwetu tena tunabaguana sababu yao pia?????shem on them shem shem shem on them hawa wafanyakazi wa hii ndege kwanza mimi ningekuwa hapo ninaamini ningepelekwa jela yaani mzungu anibague kwake halafu na kwetu tena??astaghafl***%$$%^&*((&%%$%^&&^%zao
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  hivi jamani tuna serikali kweli???? mnamsahau mwananchi kweli jamani /machozi yamenitoka...nina uhakika hao walioshushwa walikuwa ni wafanyabiashara wajenzi wa nchi
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  tuliza kichwa chako sasa mi nna hasira(avotor)teh teh!!
   
 10. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inauma sana,

  lakini msishangae, hiyo ni sera ya kitaifa. angalia kwenye maeneo mengine kama ardhi, uwekezaji nk. ni rahisi mzungu kumpa mkono rais wa tanzania kuliko mtanzania mwenzake.

  kuondokana na hali hii ji suala la kuamua tu. naam ubaguzi ndio kwanza ubachipua kwa sura nyingine!!!!!!!!
   
 11. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao waathirika wanaweza kushtaki kwa ajili ya damage na negligence, na inaweza hata kufilisi shirika iwe fundisho, wasikae kimya ni udhalilishaji mkubwa. wamelewa visifa kidogo vya mafanikio wamesahau kuwa watanzania ndio waliochangia mafanikio yao kwani ndio wateja wao wakubwa
   
 12. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na Precision ndio wameshakuwa kama KQ yetu maana ndio wenye routes za ndani! Wapi pa kukimbilia? Hakuna ushindani katika hiyo fani...kama wangekuwemo wengine wangejiuliza kwanza kabla ya kuwashusha
   
 13. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kweli Money is power, kwa nini wasiwatafutie charter????

  Lakini ni kitend cha aibu sana!!
   
 14. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sijawahi kuwa na hasira kama nilivyosoma hii habari, hawa prec wanahisi ndio wametawala soko ndio maana wanawatenda watanzania vibaya lakini wasisahau kuwa ni watanzania hawa ndio wanaowapa biashara kila siku na si wageni wa msimu.

  nimesikitika sana na kuanzia sasa nikitaka kusafiri prec itakuwa option namba 2/3...:(
   
 15. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tutakuwa hivihivi hadi tufunguke vichwa vyetu, imagine nchi imeshindwa( noop haitaki) kuleta upinzani kwa kuirun ATCL effectively, mambo kama haya ndo ya kuchukulia point za soko,but ATC inawekewa viongozi hopeless,poor and shallow in thinking,Prcision watafanya watakavyo, mimi nilishalala arusha 2days nkielekea mwanza tu imagine,eti kadege kana problem why asilete ingine?mh anyway niliwadai damage nkapata km 4.8m!
   
 16. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi majuzi nilisafiri na hawa prec nilisikitika sana na huduma iliyokuwa ikitolewa na dada mmoja mzungu MMOJA alimuuliza swali basi akamhudumia kwa haraka na tabasamu juu, mama mmoja mwenye mtoto mdogo alihitaji huduma yule dada alikunja sura utadhani amegombana naye basi MAMA akamuuliza DADA TUMEGOMBANA akaondoka zake mara baada ya kumuhudumia kama BUBU kisa MSWAHILI, acheni hizo bwana mkiomba kazi mikono nyuma mkipata vifua mbele....*****fu?
   
 17. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ndio upumbavu unaopigiwa gitaa bila kukicha huu
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hivi haya yametokea nchini kwetu eeeh wabongo bwana tumezidi ..wametutawala na bado wanaendelea kututawala ...
   
 19. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inauma sana uko ndani ya nchi yako haafu unanyanyaswa?,AGR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. M

  Magezi JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa nini precision isisusiwe??
   
Loading...