Watanzania wanaofanya phd ujerumani wanakufa!

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
WATANZANIA WENZANGU,

Hii taarifa nimeipata hivi pinde toka kwa mtanzania mwenzetu ambaye anasoma PhD Ujerumani lkn kwasasa yupo hapa Dsm akifanya Data Colection. Alikuja ofisini kwetu na katika kuongea naye kuhusu maisha na hali ya masomo huko walipo, ndipo aliponiambia hili linalosikitisha sana.

Ni kwamba, kuna watanzania wanasoma PhD Ujerumani kwa ufadhili wenye ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Ujerumani. Hawa wanafunzi kwa makadirio wanaweza wakafikia 50 hivi. Tatizo linalowasumbua katika mambo yao ya masomo ni pesa inapaswa kutumwa na serikali ya Tanzania ili waweze kujikimu kulingana na mkataba waliousaini na Wizara yetu ya Elimu na Ufundi kupitia TCU na serikali ya Ujerumani. Katika mkataba huo, inaonekana serikali ya Ujerumani inalipia kiasi kidogo tu kama gharama ya kujikimu, kwani wajerumani wamechukua gharama kama ya Bima ya Afya na pesa ya waalimu wao. Na serikali ya Tanzania ilikubali kuchukua gharama ya pesa ya kujikimu kwa asilimia kubwa. Na inavyoonekana ni kwamba hata hiyo pesa ambayo serikali ya Tanzania inatakiwa kuwalipia ni pesa iliyotolewa na serikali ya ujerumani kama msaada kwa Tanzania, lkn wakatenga sehemu kwa ajili ya capacity building hasa kwa Vyuo Vikuu vya Umma vya Tanzania.

Huyu ndugu anasema kwamba, serikali ya Tanzania ilitakiwa kuwawekea pesa kwenye akaunti zao mwishoni mwa mwezi february 2013, lkn cha ajabu ni kwamba mpaka sasa AKAUNTI ZAO ZINASOMA SIFURI. Anaendelea kusema kwamba kule Ujerumani wametawanyika katika miji mbalimbali na kwasasa hali zao ni mbaya sana, kwani wanatakiwa kufanyq malipo kwa ajili ya:

1. vyumba wanavyoishi: Hapa anasema kwamba kuna baadhi yao wameshatishiwa kufukuzwa kwenye nyumba na kuchukuliwa hatua za kisheria. Mbaya zaidi kwasasa ni kipindi cha baridi (Winter) kule Ujerumani, hivyo wanahofu ya kudhuuhurika au kufa kabisa ikifikia hatua ya kutolewa kwenye vyumba. Lkn katika hili la nyumba pia kuna wengine tayari wanatakiwa kulipa faini kwa kukiuka mkataba unaowataka kulipia vyumba kila mwanzo wa mwezi.

2. Gharama ya Kibali cha kuendelea kuishi: Jamaa anasema, hii gharama inatofautiana kila eneo, kwani kwa Ujerumani kila Mkoa una taratibu zake. Hivyo, kuna wengine wanatakiwa kulipa kuanzia Euro 80 na wengine hadi Euro 120.

3. Chakula: Anasema kwamba baadhi yao sasa wanashindia mkate na maji ya bomba, kwani hawana pesa kabisa. Mbaya zaidi kun abaadhi yao wana familia huko (mke au mume na watoto).

4. Kujisajili Chuoni kwa muhula mwingine unaoanza mwezi April 2013: Anasema kwamba huko Ujerumani kila muhula kuna gharama ya kujisajili chuoni, na usipojisajili ndani ya muda, basi chuo kitachukulia kama umeacha chuo. Na hii gharama nayo inatofautiana katika vyuo. Kwa wastani hii gharama ni kati ya Euro 200 hadi 300.

5. Nauli: Anasema kwamba baadhi yao sasa wanashindwa hata kwenda chuoni kutoka maeneo wanakokaa kwa kukosa nauli. Hapa ndipo aliponichekesha kwamba ikitokea umepanda gari bila nauli na ukakamatwa, hapo utatakiwa kulipia fani zaidi ya asilimia 100 ya nauli uliyopaswa kulipa.

6. n.k.

Huyu ndugu anasema kwamba kutokana na hali ilivyo, yeye kwasasa ataendelea kukaa hapa Dsm mpaka pesa ipatikane, kwani huku angalao ana uhakika mambo yake yanakwenda. Lkn ana wasiwasi sana kuhusu wenzake huko Ujerumani.

Nilipomuuliza kwamba mmejaribu kuwasiliana na wahusika? akasema kwamba, walianza kuwasiliana na wahusika wote (TCU na Wajerumani) tangu mwezi wa february lkn mpaka sasa hakuna jibu linaloeleweka toka TCU mbali na kuambiwa kwamba pesa zitatumwa BILA KUSEMA NI LINI PESA ZITATUMWA wakati walitakiwa kufanya hivyo tangu mwezi February 2013. Kwa upande wa serikali ya Ujerumani, anasema kwamba, kila wanapowasiliana nao, wao husema kwamba wao kama serikali ya Ujerumani wanatimza mkataba kama unavyotaka isipokuwa tatizo ni serikali ya Tanzania. Na anaendelea kusema kwamba, inavyoelekea ni kwamba serikali yetu inakiuka mkataba, na hivyo haina picha nzuri katika mahusiano ya nchi hizi mbili.

Huyu ndugu anasema kwamba hata mwaka jana tatizo kama hili liliwakuta lkn lilipata ufumbuzi hasa baada ya serikali ya ujerumani kuibana serikali yetu. Kitu ambacho kinaonekana mwaka huu ni kwamba hata serikali ya Ujerumani imechoka kubembeleza serikali ya Tanzania itimize matakwa ya mkataba.

Hivyo wandugu, nimeona ni vema nishare nanyi hii habari, kwani hao wanafunzi ni ndugu zetu sote.

NB1: Hii Habari sio uzushi wala uongo, kwa yeyote mwenye ndugu yake huko Ujerumani masomoni anaweza kuwasiliana naye.

Ahsanteni.

UPDATES:

Wana-JF,
Mpaka leo tarehe 20.03.2013, Wizara ya Elimu na Ufundi kupitia TCU haijawatumia pesa wale watanzania wanaosoma Ujerumani. Pamoja na jitihada kubwa waliofanya kuwasiliana na Waziri husika, Katibu Mkuu wa MOEVT na TCU, lkn mpaka sasa hawatumiwa pesa yoyote na wala hakuna tarehe rasmi waliyoambiwa kwamba watatumiwa pesa. Majibu wanayopata kutoka TCU ni kwamba, muwe na subira pesa itatumwa, lkn katika hayo majibu ya TCU haionyeshi ni lini hizo pesa zitatumwa.

Jamaa yangu anazidi kuniambia kwamba, hali imezidi kuwa mbaya kiasi kwamba kuna baadhi yao wanafikiria kusitisha masomo, kwani wanaathirika kiakili na kimwili.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Poleni sana. Huku magamba wanatanua kama kawa. Wanachagua nchi za kutembelea! Hata hivyo kwa wale mlioko jiji la Hamburg jiepusheni na machangudoa wa mtaa wa St. Paul
 
phd candidate analia njaaaa??? Watanzania nyerere kawalemaza sana kudadadeki hamna box uko?

nokiatochi,
nasikia hata ndugu zako wakenya nao wana programmu kama hiyo. vipi wao serikali haiwajibiki kutimiza sehemu ya mkataba, kwasababu tu ni phd candidate? kuhusu mabox nasikia waarabu, waulaya mashariki wamejazana huko kishenzi.
 
maji ya bomba ndo mpango mzima ulaya, kwani huwa kuna maji mengine ya kunywa??huo ni upepo tu utapita
 
Kwashule ya PhD Germany box alipigiki, huwa shule yake ipo tight na hata vijikazi mshenzi mpaka upate kibali.
 
Nawapa pole hao ndugu zetu wanaoadhirika ktk nchi ya ugenini. Nashauri wale wote wanaotaka kwenda kusomea nje kujiandaa kujifadhiri kwa asilimia zote wasikubali kudanganywa na serikali yetu kuwa itawasomesha kwani inashindwa kuwasomesha hata hawa wa shahada ya kwanza wanaosomea ndani ya nchi
 
Poleni sana. Huku magamba wanatanua kama kawa. Wanachagua nchi za kutembelea! Hata hivyo kwa wale mlioko jiji la Hamburg jiepusheni na machangudoa wa mtaa wa St. Paul
Du! Mkuu, wajiepushe na changudoa wakati hata ela ya kula hawana!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
This is a dead government. Zamani tulijivunia utanzania wetu lakini sasa ni aibu kujitambulisha kama mtanzania. Ee Mungu tunaomba utuondoshee hii kadhia kwa kuiondolea mbali hii serikali hofu. Watanzania tuhamasishane ili ifikapo siku ya kuing'oa serikali hii haramu tuwe tayari. Haijalishi ni lini na wala si lazima ifike 2015. Tusifungwe na kalenda.
 
Poleni sana. Huku magamba wanatanua kama kawa. Wanachagua nchi za kutembelea! Hata hivyo kwa wale mlioko jiji la Hamburg jiepusheni na machangudoa wa mtaa wa St. Paul

Hakuna tatizo si wamefungwa gavana chezea njaa wewe hata tamaa ya kuzini na machangudoa itawajia?!
 
Poleni sana wandugu....ila maelezo yako ya kina sana, ni kama wewe mwenyewe ndo mhusika vile........
 
Poleni sana wandugu....ila maelezo yako ya kina sana, ni kama wewe mwenyewe ndo mhusika vile........

Hapana ndugu. Mimi sio mmoja wao, bali nilipata muda wa kuongea sana na jamaa wakati wa lunch ili niweze kujua jinsi wanavyoishi huko nchi za watu.
 
Unafikiri kwa kutumia makalio, nchi za watu utafanya mradi gani? Ndo maana dada zetu mkifika huko mnajiuza kwa sababu uvumilivu hamuna na maisha yenu wa kushindana yatawacost!!!!
 
..kweli Tanzania tunahitaji muujiza, wajerumani watupe fadhila ya kutusaidia kusomesha wataalamu, nchi (serikali) ipewe fungu la "capacity building" bado lisifike kwa walengwa!!! literally ni kuwa wanatusomeshea bure hawa wataalamu, pesa hiyo ya kujikimu imetoka ujeremani inarudi ujeremani kupitia mtanzania..lakini bado kuna wateule wachache hawafanikishi hili zoezi rahisi, jamaaaniii!!
 
..kweli Tanzania tunahitaji muujiza, wajerumani watupe fadhila ya kutusaidia kusomesha wataalamu, nchi (serikali) ipewe fungu la "capacity building" bado lisifike kwa walengwa!!! literally ni kuwa wanatusomeshea bure hawa wataalamu, pesa hiyo ya kujikimu imetoka ujeremani inarudi ujeremani kupitia mtanzania..lakini bado kuna wateule wachache hawafanikishi hili zoezi rahisi, jamaaaniii!!

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo ndugu yangu.
 
Unafikiri kwa kutumia makalio, nchi za watu utafanya mradi gani? Ndo maana dada zetu mkifika huko mnajiuza kwa sababu uvumilivu hamuna na maisha yenu wa kushindana yatawacost!!!!

Kwa mada inayojadiliwa na kwa post hii yako kuna mambo mawili yanayoweza kuelezea wewe ni nani. You are either below 18 years or immature person intellectually.
 
Kwa mada inayojadiliwa na kwa post hii yako kuna mambo mawili yanayoweza kuelezea wewe ni nani. You are either below 18 years or immature person intellectually.

Inaelekea jamaa hajaelewa dhima nzima ya hii mada.
 
Nina walakini na hii habari kwa 90%!!
Wizara ya Elimu kupitia TCU!!??? TCU siku hizi inahusika na ufadhili wa Elimu Overseas? Isije ikawa kama wenzetu wa Ukraine mwaka 2004/5 kama sikosei!
 
Back
Top Bottom