Watanzania Wanahitaji kudai Uhuru Wao.

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,570
19,442
Nadhani Tanzania iko chini ya Advanced Neocolonialsim ambapo uchumi umeshikwa na watu wa nje, wakati serikali imeshikwa na watanzania wasiokuwa na mapenzi na nchi hii na tayari ama wana maskani yao nje ya nchi au wana mipango ya namna hiyo.

Kwa nini?

(a) Aliyekuwa Gavana wa Benki kuu akisimamia wizi mkubwa wa pesa zetu, baada ya kuacha ofisi alirudi kwake Marekani, ambako ndiko alikomalizia maisha yake.


(b) Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali akisimamia mikataba mingi mibovu, amegundulika kuwa na vijisenti vingi sana huko kwenye mabenki ya nje. Siku yoyote akitaka ataondoka na kwenda kwenye vijisenti vyake. Huyu bwana naye alikuwa ametushikia bendera ya karatasi tu.

(c) Aliyekuwa katibu Mkuu wa wizara ya fedha akisimamia matumizi na mapato ya serikali yetu ana maskani yake ya kudumu huko Marekani. Siku yoyote anaweza kuondoka.

(d) Leo hii nimesoma headline moja kuwa aliyekuwa waziri wa elimu akisimamia kuharibika kwa elimu nchini ili vizazi vijavyo viweze kutawaliwa kirahisi naye ana mpango wa kuhamie Marekani.

(e) Kuna tetesi kuwa kiongozi mmoja mzito sana anauza mali zake kwa kasi sana, inawezekana lengo lake ni kuhamia nje ya nchi kutokana na mwenendo wa kesi za ufisadi zilizoanza. Kiongozi huyu anasemekana ana majumba Marekani na Afrika ya Kusini.

(f) Viongozi wetu wengi waliowahi kushika nafasi nyeti wana maskani mengine nje ya nchi wakati hakuna viongozi wa nchi za nje walio na maskani yao nchini mwetu.

Huu ufisadi tunaosikia kila siku ni matokeo ya viongozi wetu kuitumia nchi yetu kama sehemu ya wao kuchuma, halafu wakalie walichochuma huko nchi za nje. kwa kifupi, tunahitaji uhuru wetu tena, safari hii ikiwa ni dhidi ya Advaced Neocolonialism.
 
JF we dare to speak openly. Huyo kigogo anayeuza mali zake kwa kasi ni nani?. Kama umeamua kuja hapa na kuleta maada basi ni bora uweke kila kitu wazi. Kama huna uhakika ni bora usije na maada zako.
 
Watanzania Wanahitaji kudai Uhuru Wao.

Mkuu Kiuchuguu,

- Hiii haijakaa sawa kwa sababu umechanganya ishu mbili muhimu sana nazo ni (1) kuwa na uhuru, na (2). kutojua namna ya kuutumia,

- Maana kama ni uhuru Wa-Tanzania tunao toka 1961, sasa labda tatizo ni namna ya kuutumia, sasa hilo haliwezi kuwa ni tatizo la viongozi wetu, bali ni letu sisi wananchi wa Tanzania.

Kuwa na uhuru ni one thing, na kujua kuutumia ni another story of its own, kama huamini angalia Africans Americans huko US.
 
Tujiulize tulitaka tuwe huru ili iwe nini? Je ni manufaa gani tumeyapata tangu tuwe huru? Je Mkoloni angeendelea kututawala tungekuwa na matatizo gani?

Why did we seek independence? for what and from what?
 
Tujiulize tulitaka tuwe huru ili iwe nini? Je ni manufaa gani tumeyapata tangu tuwe huru? Je Mkoloni angeendelea kututawala tungekuwa na matatizo gani?

Why did we seek independence? for what and from what?

Mchungaji, 'kujiuliza' kwa nini tuliomba na kupata uhuru si bora, manake, wengi hatukuishi ukolonini.
Ila, nakuelewa...

* Sisi wananchi hatukupata uhuru... ule wa 1961. Tulikombolewa kutawaliwa na wazungu afu tukatawaliwa na viongozi wetu. Viongozi wetu wametutawala badala ya kutuwakilisha. Tunahitaji uhuru wa:
1. kufundishwa na kuielewa katiba... ka wengi hatuijui, tutajuaje imekuwa out-dated?
2. kutamka mapingo bila uoga wa kutupwa jelani ama...
3. kuwa na vyombo vya habari ambavyo vinachambua uongozi wa viongozi bila uoga wa kuchapwa adhabu

... mnajua mengineyo...

tunahitaji wengi ambao wanatamka ukweli ka huyu mchungaji ... bofya linki chini.
YouTube - MCHUNGAJI MUNISHI AIKEMEA SERIKALI YA KIKWETE GTV
 
Kinachonikera ni kuwa wananchi wengi hatuoni faida ya uhuru kwa vile. Kero za maisha tulizo nazo zinazidi zile kero za ukoloni. Halafu baadhi ya viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza na kutuondolea kero hizo wanaifanya nchi hii kama ni sehemu ya wao kuchuma na kwenda kutumia mavuno yao nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom