Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 38,237
- 88,521
Habari Wakuu!
Bado nafuatilia hofu aliyonayo mtanzania. Hofu ya kisiasa. Wasiwaai na kutokuaminiana. Awamu ya tano Watu walikuwa na hofu ya usalama wao, nazungumzia uhai wao na Uhuru wao. Awamu hii Watu wanahofu ya Rasilimali zao.
Hofu
Wasiwasi
Mashaka!
Mali zetu jamani zinaibiwa. Oooh! Itakuwaje yule kateuliwa pale, ni jizi na fisadi mwenye vyeti vya Wizi. Oooh! Mkataba Fulani umeingiwa, uuuuwiii! Tumepigwa! Hofu! Vilio! Mashaka! Hofu ya kisiasa.
Nini kifanyike?
Ni lazima apatikane kiongozi ambaye atawatoa Watanzania hofu, wajione wapo salama, wao, Uhuru wao na Rasilimali zao. Kiongozi ambaye atawafanya watanzania wajihisi salama.
Kiongozi huyu yupo au hayupo?
Kiongozi huyo kama hayupo atapatikana wapi? Kina Nani watakuwa Wasaidizi wa kiongozi huyo? Bila Shaka lazima wawe Watu waadilifu, wazalendo, ambao hawana tamaa na uroho wa Mali.
Nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam