Watanzania wamechoka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wamechoka!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamageuko, Mar 24, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Haishangazi kabisa sasa kuwaona Watanzania wenzetu wakinywa sumu kwa furaha!
  Kuna kisa kimoja kinafanana na hali za Watanzania wa leo:

  Mgonjwa mmoja alikuwa hoi taabani na akaona kwamba njia pekee ya kumsaidia nafuu ni kifo pekee. Ikawa anawatusi madaktari na wauguzi kwa makusudi ili wampe sumu afe apumzike. Walimvumilia lakini ipo siku akaja daktari mgeni na hakuwa na uvumilivu kama wenziwe basi alipotukanwa yeye akaona dawa ni kidogo tu.. kumpumzisha! akachanganya madawa kwa kiwango alichojua kuwa yule mgonjwa hatoamka tena kesho yake. Akampa na yule mgonjwa akanywa ile dawa kwa furaha. Mgonjwa yule akalala fofofoo na baada ya masaa kumi akaamka! Akashukuru kwamba alau daktari aliempa dawa jana anajua kutibu na si wale wengine! aliporejea kwenye zamu daktari yule wenzake wakamuuliza mbona mgonjwa wake anamsifia kwa tiba na hajawatukana, akaenda kumuona kwa mastaajabu maana alijua kwamba mgonjwa yule ndani ya masaa sita angelikuwa ameshakufa!! Alipomfikia mgonjwa yule akasema "katika madaktari wote walionitibu wewe ndio daktari, hawa wengine hawana wanachojua! Ila tafadhali katika ile dawa ya jana ongeza kipimo kidogo!" (mgonjwa yule alikuwa na ujuzi wa madawa aliona mchanganyiko ule akajua atakufa na hakufa!.

  Hii hali ya mgonjwa huyo na hali za Watanzania wa leo hazitofautiani.....
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  weka wazi sijakuelewa...tumechoka nn sasa utawala? njaa?dowans?ufisadi?hai ngumu ya maisha? nini sasa?
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ni kisa kizuri, kinavutia lakini naona kama hakina ukweli na hali halisi.
   
 4. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  yooote hayo mkuu ni majawabu kuliko maswali!

  Si jambo la kushangaza tena, kuwaona baadhi yetu tukila na kunywa takataka pasi na kuuliza wala kudadisi kifuatacho! Hii inadhihirisha kwamba watu wameshachoka!

  Baadhi yetu tunadhani kwamba, hapana anaeuona uchi wetu.. tunajiona tumevaa! hata tukiambiwa nguo zetu hazijatustiri.. sisi husisitiza kwamba TUMEVAA!!

  Kweli Watanzania wamechoka!
   
Loading...