Stendi ya Mizigo Bariadi ya Tsh. Bilioni moja, inakusanya Tsh 0 Mwezi mzima

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
34
82
vlcsnap-2023-09-01-00h31m20s102.png

Kuna vitu huwa vinachekesha sana kwenye hii nchi yetu, unafikiria kweli tunao watalaamu wa kutosha? Wanaoweza kung’amua mambo na yakawa sawa? Yakaleta tija kwa Taifa?

Angalieni hiki kituko katika Wilaya ya Bariadi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi ndani ya Mkoa wa Simiyu.

Halmashauri hiyo ilijenga stendi ya Mizigo eneo la Kidulya takribani Kilometa 7 kutoka katikati ya Mji ambayo iligharimu zaidi ya Sh. Bilioni moja.

Mshangao mkubwa hapa, Stendi hiyo licha ya kugharimu kiasi kikubwa cha pesa lakini kimekuwa chanzo mfu cha mapato kwenye Halmashauri hiyo.

Taarifa za ndani zimeonyesha kuwa, ndani ya mwezi mzima Stendi hiyo imekusanya mapato Sh. 0 (yaani hakuna mapato yoyote yaliyokusanywa kwa mwezi mzima).

Unajua hii inashangaza, stendi ya Bilioni 1 tena na zaidi, then mwezi mzima hakuna mapato yamekusanywa, unajiuliza Nani? Alibuni huu mradi, Ni kweli Serikali ina pesa za kuchezea?

Nimefuatilia kujua sababu ni Nini? Moja ni kwamba Wafanyabiashara wamegoma kushushia mizigo yao kwenye hiyo stendi kutokana na umbali.

Pili stendi hiyo haina miundombinu ya kuwezesha usalama wa bidhaa za Wafanyabiashara kuwa salama hasa nyakati za mvua.

Tatu stendi hiyo haina kivuli kwa ajili ya kujikinga mvua au jua kwa wafanyabishara, na wala haina stoo ya kuhifadhi bidhaa pamoja na kukosa ulinzi wa kutosha.

Wafanyabiashara wanasema, umbali wa Kilometa 7 kufika kwenye hiyo stendi kutoka mjini, ndiyo kikwazo kikubwa, wakishushia mizigo inawaongezea gharama kubwa kufikisha mizigo mjini.

Mfano nikishushia mizigo kule stendi, alafu nikachukua gari ndigo (Canter) gharama yake kuleta mzingo hapa mjini katikatika siyo chini ya 300,000, faida yote inasha, lakini kule hakuna stoo ya kuhifadhi mizingo, sasa mvua ikinyesha tutaweka wapi mizigo yetu?

Kutokana na hali hiyo, stendi hiyo ufikia wakati mwezi mzima hakuna gari lolote ambalo limeingia kushusha mzingo, hivyo makusanyo ni Sh. 0 kwa mwezi, na yakiingia hayawezi kuzidi mawili tu, hapo utahesabu mapato haya yakipatikana inawezekana kwa mwezi ikakusanya kidogo sana.

Wafanyabiashara wamesusia hiyo stendi, na walichokifanya ni kutafuta eneo ambalo lipo uchochoroni, Mtaa wa Butiama na kufanya kuwa stendi bubu ya mizigo, wao wanasema eneo hilo lipo karibu sana na mjini.

Unajiuliza Nani? Alibuni huo mradi kupelekwa uko? Je hatuoni kuwa aliingizia hasara serikali? Eneo rafiki lilikosekana mjini? Kwa nini eneo la Mnada usingehamishwa mnada na kujengwa hiyo stendi?

Stendi kukusanya Sh. 0 kwa Mwezi mzima, halafu iligharimu zaidi ya Bilioni moja ni hasara kubwa sana.


Pia soma: Bariadi: Meya aeleza kwanini Stendi ya Mizigo eneo la Kidulya haikusanyi mapato tarajiwa
 
Halafu alijenga magufuri
View attachment 2735386

Kuna vitu huwa vinachekesha sana kwenye hii nchi yetu, unafikiria kweli tunao watalaamu wa kutosha? Wanaoweza kung’amua mambo na yakawa sawa? Yakaleta tija kwa taifa?

Angalieni hiki kituko, uko katika Wilaya ya Bariadi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi ndani ya Mkoa wa Simiyu.

Halmashauri hiyo ilijenga stendi ya Mizigo eneo la Nyaumata takribani kilometa 7 kutoka mjini Katikati, ambayo iligharimu zaidi ya Sh. Bilioni moja.

Mshangao mkubwa hapa, Stendi hiyo licha ya kugharimu kiasi kikubwa cha pesa, lakini kimekuwa chanzo nfu cha mapato kwenye halmashauri hiyo.

Taarifa za ndani zimeomyesha kuwa, ndani ya mwezi mzima Stendi hiyo imekusanya mapato Sh. 0 (yaani hakuna mapato yeyote yaliyokusanywa kwa mwezi mzima)

Unajua hii inastahajabisha, stendi ya Bilioni 1 tena na zaidi, alafu mwezi mzima hakuna mapato yamekusanywa, unajiuliza Nani? Alibuni huu mradi, Ni kweli Serikali ina pesa za kuchezea?

Nimefuatilia kujua sababu ni Nini? Moja ni kwamba wafanyabiashara wamegoma kushushia mizigo yao kwenye hiyo stendi kutokana na umbali.

Pili stendi hiyo haina miundombinu ya kuwezesha usalama wa bidhaa za wafanyabiashara kuwa salama hasa nyakati za mvua.

Tatu stendi hiyo haina kivuli kwa ajili ya kujikinga mvua au jua kwa wafanyabishara, na wala haina stoo ya kuhifadhi bidhaa pamoja na kukosa ulinzi wa kutosha.

Wafanyabiashara wanasema, umbali wa Kilometa 7 kufika kwenye hiyo stendi kutoka mjini, ndiyo kikwazo kikubwa, wakishushia uko mizigo inawaongezea gharama kubwa kufikisha mizigo mjini.

Mfano nikishushia mizigo kule stendi, alafu nikachukua gari ndigo (Canter) ghamara yake kuleta mzingi hapa mjini katikatika siyo chini ya 300,000, faida yote inasha, lakini kule hakuna stoo ya kuhifadhi mizingo, sasa mvua ikinyesha tutaweka wapi mizigo yetu?

Kutokana na hali hiyo, stendi hiyo ufikia wakati mwezi mzima hakuna gari lolote ambalo limeingia kushusha mzingo, hivyo makusanyo ni Sh. 0 kwa mwezi, na yakiingia hayawezi kuzidi mawili tu, hapo utahesabu mapato haya yakipatikana inawezekana kwa mwezi ikakusanya kidogo sana.

Wafanyabisha wamesusia hiyo stendi, na walichokifanya ni kutafuta eneo ambalo lipo uchochoroni, mtaa wa Butiama na kufanya kuwa stendi bubu ya mizigo, wao wanasema eneo hilo lipo karibu sana na mjini.

Unajiuliza Nani? Alibuni huo mradi kupelekwa uko? Je hatuoni kuwa aliingizia hasara serikali? Eneo rafiki lilikosekana mjini? Kwa nini eneo la Mnada usingehamishwa mnada na kujengwa hiyo stendi?

Stendi kukusanya Sh. 0 kwa Mwezi mzima, alafu iligharimu zaidi ya Bilioni moja ni hasara kubwa sana.
Hizi ndio akili za kipumbavu za wanaojiitaga wasomi wa Tanzania,utasikia miradi ya kimkakati 😀😀

Pumbavu sana,yamekaa huko maofisini vichwani hakuna kitu.

Kila siku nawaambia Serikali haipaswi kufanya biashara,weka mazingira mazuri acha private sector wafanye kusanyeni ushuru.
 
Back
Top Bottom