Watanzania waliotorosha fedha nje kufilisiwa
*Serikali yaunga mkono mpango wa Benki ya Dunia
*Meghji asema serikali imejipanga vyema
*Aonya hakuna huruma kwa wale watakaobainika
Ramadhan Semtawa na Kizitto Noya
wako serious????
*Serikali yaunga mkono mpango wa Benki ya Dunia
*Meghji asema serikali imejipanga vyema
*Aonya hakuna huruma kwa wale watakaobainika
Ramadhan Semtawa na Kizitto Noya
Source: MajiraFEDHA haramu zilizotoroshwa nje na watanzania zikibainika zitarejeshwa nchini na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Waziri wa Fedha, Zakia Meghji aliliambia gazeti hili jana kuwa hatua hiyo ya serikali inafuatia kuridhia kwa Tanzania kwa Mpango wa Benki ya Dunia (WB) wa kurejesha fedha haramu, zilizofichwa katika mabenki ya nchi za nje.
"Tanzania tumejipanga vizuri, ndiyo maana hata uchunguzi wa EPA (Akaunti ya Madeni ya Biashara ya Nje), tumehusisha wakaguzi wa kimataifa," alisema Meghji.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Benki ya Dunia (WB), katika kuzisaidia nchi masikini kujiimarisha kiuchumi kwa kuzuia utoroshaji wa fedha kwenda mabenki ya nchi zilizoendelea.
"Hatutakuwa na huruma na wote watakaobainika kuhusika kufanya ubadhirifu, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao," alionya Meghji.
Jarida la The Economists Intelligency Unit, toleo la Agosti lilinukuu taarifa ya WB, ikielezea azma hiyo ya kusaidia urejeshaji wa fedha haramu zilizotoroshwa nje.
Kwa mujibu wa jarida hilo, tayari mpango huo umeanza kutekelezwa katika baadhi ya nchi, ikiwemo Kenya na Uganda.
Meghji alifafanua kwamba, tayari serikali imeunda vyombo vya kufuatilia mwenendo wa mzunguuko wa fedha zinazoingia na zinazotoka kwenda katika mabenki ya nchi za nje na kwamba serikali imejipanga vizuri kudhibiti mzunguko wa fedha chafu.
"Sisi tumejiandaa vizuri, tuna vyombo ambavyo vimeanzishwa kisheria, hivi vina jukumu la kuangalia mzunguuko wa fedha zinazoingia na kutoka," alisema.
Meghji alitaja sheria ya Kuzuia Fedha Haramu (Anti-Money Loundering) ya mwaka 2007 na ile iliyoanzisha Kitengo Maalumu cha Kuchunguza Mzunguko wa Fedha (Financial Intelligency Unit-FIU) kuwa ndizo zenye jukumu la kuangalia mzunguko wa fedha.
"Tayari tuna sheria ya kudhibiti fedha haramu, pia tuna kitengo cha kuangalia na kuchunguza mzunguko wa fedha, ambacho mkurugenzi wake ameteuliwa ni Mr.(Bwana) Kessy," alisisitiza Meghji.
Hata hivyo, Meghji aliongeza kwamba ni lazima fedha zithibitishwe na vyombo hivyo kama ni haramu ndipo hatua ya kuzirejesha zitachukuliwa.
"Lakini ni hadi itakapothibitishwa na vyombo vyetu kama ni fedha haramu, ndipo hatua zitachukuliwa," alisisitiza.
Alisema FIU inafanya kazi bega kwa bega na mabenki nchini, ikiwa ni pamoja na kuangalia mwenendo wa fedha hizo.
Jarida la The Economists Intelligency Unit, linalochapishwa nchini Uingereza linaheshimika kutokana na kuandika taarifa za ndani za kiuchumi.
Kwa mujibu wa Jarida hilo, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mpango huo, ingawa Benki ya Duania tawi la nchini, limesema mpango huo haujaanza.
Afisa Habari wa benki hiyo tawi la Tanzania, Ichikael Maro, aliliambia gazeti hili wiki iliyopita kuwa kuanza kwa mpango huo, kutategemea agizo la serikali kuhusu utekelezaji wake.
"Kimsingi, sisi hatujiamulii kufanya mazoezi makubwa kama haya, tunategemea uamuzi wa serikali, nadhani Benki ya Dunia katika nchi ambazo zoezi hilo linaendeshwa ilipata maelekezo toka kwa serikali husika," alisisitiza kwa kifupi Maro.
Hatua hiyo inakuja wakati nchi za Afrika zikikabiliwa na tatizo la mzunguko wa fedha haramu, ambazo nyingi hutoroshwa kupitia mabenki ya nje.
Miongoni mwa nchi zilizoathirika na ufisadi ni Nigeria, ambako mtawala wa kidikteta marehemu San Abacha na Mobutu Seseseko wa iliyokuwa Zaire, waliwahi kuficha mamilioni ya dola katika mabenki ya nchi za nje, ikiwemo Uswis na Ufaransa.
Kutoroshwa kwa mamilioni hayo ya dola kumekuwa kukichangia umasikini na ufukara katika nchi za Afrika, ambazo sehemu kubwa ya bajeti zao hutegemea msaada kutoka kwa wafadhili.
wako serious????