Watanzania waliotorosha fedha nje kufilisiwa!

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Watanzania waliotorosha fedha nje kufilisiwa

*Serikali yaunga mkono mpango wa Benki ya Dunia
*Meghji asema serikali imejipanga vyema
*Aonya hakuna huruma kwa wale watakaobainika


Ramadhan Semtawa na Kizitto Noya

FEDHA haramu zilizotoroshwa nje na watanzania zikibainika zitarejeshwa nchini na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri wa Fedha, Zakia Meghji aliliambia gazeti hili jana kuwa hatua hiyo ya serikali inafuatia kuridhia kwa Tanzania kwa Mpango wa Benki ya Dunia (WB) wa kurejesha fedha haramu, zilizofichwa katika mabenki ya nchi za nje.

"Tanzania tumejipanga vizuri, ndiyo maana hata uchunguzi wa EPA (Akaunti ya Madeni ya Biashara ya Nje), tumehusisha wakaguzi wa kimataifa," alisema Meghji.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Benki ya Dunia (WB), katika kuzisaidia nchi masikini kujiimarisha kiuchumi kwa kuzuia utoroshaji wa fedha kwenda mabenki ya nchi zilizoendelea.

"Hatutakuwa na huruma na wote watakaobainika kuhusika kufanya ubadhirifu, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao," alionya Meghji.

Jarida la The Economists Intelligency Unit, toleo la Agosti lilinukuu taarifa ya WB, ikielezea azma hiyo ya kusaidia urejeshaji wa fedha haramu zilizotoroshwa nje.

Kwa mujibu wa jarida hilo, tayari mpango huo umeanza kutekelezwa katika baadhi ya nchi, ikiwemo Kenya na Uganda.

Meghji alifafanua kwamba, tayari serikali imeunda vyombo vya kufuatilia mwenendo wa mzunguuko wa fedha zinazoingia na zinazotoka kwenda katika mabenki ya nchi za nje na kwamba serikali imejipanga vizuri kudhibiti mzunguko wa fedha chafu.

"Sisi tumejiandaa vizuri, tuna vyombo ambavyo vimeanzishwa kisheria, hivi vina jukumu la kuangalia mzunguuko wa fedha zinazoingia na kutoka," alisema.

Meghji alitaja sheria ya Kuzuia Fedha Haramu (Anti-Money Loundering) ya mwaka 2007 na ile iliyoanzisha Kitengo Maalumu cha Kuchunguza Mzunguko wa Fedha (Financial Intelligency Unit-FIU) kuwa ndizo zenye jukumu la kuangalia mzunguko wa fedha.

"Tayari tuna sheria ya kudhibiti fedha haramu, pia tuna kitengo cha kuangalia na kuchunguza mzunguko wa fedha, ambacho mkurugenzi wake ameteuliwa ni Mr.(Bwana) Kessy," alisisitiza Meghji.

Hata hivyo, Meghji aliongeza kwamba ni lazima fedha zithibitishwe na vyombo hivyo kama ni haramu ndipo hatua ya kuzirejesha zitachukuliwa.

"Lakini ni hadi itakapothibitishwa na vyombo vyetu kama ni fedha haramu, ndipo hatua zitachukuliwa," alisisitiza.

Alisema FIU inafanya kazi bega kwa bega na mabenki nchini, ikiwa ni pamoja na kuangalia mwenendo wa fedha hizo.

Jarida la The Economists Intelligency Unit, linalochapishwa nchini Uingereza linaheshimika kutokana na kuandika taarifa za ndani za kiuchumi.

Kwa mujibu wa Jarida hilo, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mpango huo, ingawa Benki ya Duania tawi la nchini, limesema mpango huo haujaanza.

Afisa Habari wa benki hiyo tawi la Tanzania, Ichikael Maro, aliliambia gazeti hili wiki iliyopita kuwa kuanza kwa mpango huo, kutategemea agizo la serikali kuhusu utekelezaji wake.

"Kimsingi, sisi hatujiamulii kufanya mazoezi makubwa kama haya, tunategemea uamuzi wa serikali, nadhani Benki ya Dunia katika nchi ambazo zoezi hilo linaendeshwa ilipata maelekezo toka kwa serikali husika," alisisitiza kwa kifupi Maro.

Hatua hiyo inakuja wakati nchi za Afrika zikikabiliwa na tatizo la mzunguko wa fedha haramu, ambazo nyingi hutoroshwa kupitia mabenki ya nje.

Miongoni mwa nchi zilizoathirika na ufisadi ni Nigeria, ambako mtawala wa kidikteta marehemu San Abacha na Mobutu Seseseko wa iliyokuwa Zaire, waliwahi kuficha mamilioni ya dola katika mabenki ya nchi za nje, ikiwemo Uswis na Ufaransa.

Kutoroshwa kwa mamilioni hayo ya dola kumekuwa kukichangia umasikini na ufukara katika nchi za Afrika, ambazo sehemu kubwa ya bajeti zao hutegemea msaada kutoka kwa wafadhili.
Source: Majira

wako serious????
 
"Hatutakuwa na huruma na wote watakaobainika kuhusika kufanya ubadhirifu, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao," alionya Meghji.

"Sisi tumejiandaa vizuri, tuna vyombo ambavyo vimeanzishwa kisheria, hivi vina jukumu la kuangalia mzunguuko wa fedha zinazoingia na kutoka," alisema.

"Tayari tuna sheria ya kudhibiti fedha haramu, pia tuna kitengo cha kuangalia na kuchunguza mzunguko wa fedha, ambacho mkurugenzi wake ameteuliwa ni Mr.(Bwana) Kessy," alisisitiza Meghji.

"Lakini ni hadi itakapothibitishwa na vyombo vyetu kama ni fedha haramu, ndipo hatua zitachukuliwa," alisisitiza.

Statements kama hizi zinatia moyo lakini sheria ngapi tulizo nazo zinapindishwa? Hii sheria ya kudhibiti fedha haramu tumekuwa nayo kipindi; wangapi wameweza kuifanya sheria hii ionekane kuchukua mkondo wake?

Endapo wataamua kufanya kweli napendekeza waanze na watu wafuatao (uchunguzi wa awali):

1. Balali

2. Sumaye

3. Mkapa

Kisha waendelee na kuzichunguza baadhi ya tuhuma ambazo zimetolewa na wananchi ama vyama vya upinzani ili kupata validity yake.

Wasipuuze kila linalosemwa!
 
"Tayari tuna sheria ya kudhibiti fedha haramu, pia tuna kitengo cha kuangalia na kuchunguza mzunguko wa fedha, ambacho mkurugenzi wake ameteuliwa ni Mr.(Bwana) Kessy," alisisitiza Meghji.
sawa wana kitengo je kipo independent? au ndio kama PCCB ambao wanaripoti kwa rais au tume ya uchaguzi?

invisible hayo majina umeandika so faint unaogopa kuyabold? just curious
 
invisible hayo majina umeandika so faint unaogopa kuyabold? just curious

:) siwezi kuthibitisha kuwa wao wametoroshea fedha nje ndio maana nimeona niya-faint kwakuwa sina hakika lakini malalamiko ya wananchi dhidi ya hawa yamekuwa makubwa.

Panapofuka moshi... Japo wao husema 'debe tupu...'. Naamini ingependeza kusafisha majina ya hawa kwa serikali kufanya uhakiki wa tuhuma dhidi ya watu hawa including rais wa awamu ya 2 na kurejesha imani ya wananchi dhidi ya viongozi hawa.

Itawasaidia wao na itaisafisha serikali. Kama wako safi wala hawataona tatizo kuchunguzwa!

Nimeeleweka sio?
 
Hakuna aliye serious na hili, ni propaganda tu ya kununua wananchi waliochoka kwa bei chee!
 
Another day another populist minister. Kwanza angewauliza hao World Bank wampe list ya watu ambao walinyanganywa pesa na pili benki gani itakubali kuwa kuna mwizi kaweka pesa kwao?

Mabilioni ya Abacha mpaka leo hayajarudishwa sembuse vijishilingi vilivyoibiwa bongo

what a load of crap!
 
game theory....

mie nimechoka na siasa za bongo,JF tunapiga kelele weee lakini wanasiasa bwana wanajuana hawatupani.kesho na keshokutwa mara utasikia hao hao akina Dr Slaaa wamerudi tena CCm,ndio maana nikasema mie yangu macho tu.
 
Nafikiri ni propaganda na kutaka wananchi wasahau hao ya mafisadi.

Serikali inawajua baadhi ya waliotorosha pesa nje, sasa kwanini mpaka isubiri WB?

Balali mwenyewe alishawahi kusema kusema kuhusu mabilioni yaliyotoroshwa na Watanzania nje ya nchi.

Tusiwaamini hawa jamaa mpaka tuone matokeo yake.
 
Naomba nisaidieni,
Pesa kwani ni cash tu? Vipi wale walioiba wakaenda jenga mahekalu huko ng'ambo? Nadhani kama kweli wako serious katika swala hili isiishie kwenye cash kwenye mabenki, iende hadi hao waliochota na kujenga mahekalu huko ughaibuni!

(Mfano kuna udaku kwamba chenkapa alijenga kitu cha kutisha huko South ambapo alimtaka Mandela afanye ufunguzi, Mzee Mandela alipo ona kufuru akatolea nje kwamba hawezi shiriki dhambi hiyo hasa kwa Umasikini uliopo Tz.)
 
Kuna Vigogo Wengine Watoto Wao Au Ndugu Zao Wamejilipua Nje Na Wanawatumia Pesa , Sasa Kwa Sababu Wanauraia Wa Nchi Zingine Serikali Imeshafikiria Njia Zaidi Ya Kushugulikia Watu Hawa Kama Ndio Wanaotumiwa Na Baba Zao Walio Ndani Ya Tanzania Kutorosha Pesa
 
Naomba nisaidieni,
Pesa kwani ni cash tu? Vipi wale walioiba wakaenda jenga mahekalu huko ngambo? Nadhani kama kweli wako serious katika swala hili isiishie kwenye cash kwenye mabenki, iende hadi hao waliochota na kujenga mahekalu huko ughaibuni!

(Mfano kuna udaku kwamba chenkapa alijenga kitu cha kutisha huko South ambapo alimtaka Mandela afanye ufunguzi, Mzee Mandela alipo ona kufuru akatolea nje kwamba hawezi shiriki dhambi hiyo hasa kwa Umasikini uliopo Tz.)

Kuna wabunge pia wa chama tawala na upinzani ambao wananunua nyumba London. Kununua nyumba pekee sio kosa lakini je wamemuambia TRA? Je wanalipa kodi ya pesa wanazopata toka kwenye pango?

Fagio la chuma likipita naona litakumba wengi sana. Muhimu watuulize wananchi ili tuwasaidie kuonyesha hizo nyumba ziliko.
 
Fagio la chuma likipita naona litakumba wengi sana. Muhimu watuulize wananchi ili tuwasaidie kuonyesha hizo nyumba ziliko.

Dah,

The more tunavyoweza kuchangia topic hii ndo tunaweza kuwapata suspects zaidi. Long time sijamwona Yebo Yebo online, au naye kanunua nyumba hapo London? (joke)
 
Dah,

The more tunavyoweza kuchangia topic hii ndo tunaweza kuwapata suspects zaidi. Long time sijamwona Yebo Yebo online, au naye kanunua nyumba hapo London? (joke)

Invisible,

Unajua jana nilimkumbuka Yebo yebo, kumbe tuko wengi ambao tumemmiss na tungetaka arudi.

Na mimi napotea kuanzia leo kwa kama mwezi. Siendi kutafuta nyumba, nataka nijiongezee maarifa kidogo.

Nitakuwa nasoma JF, ila sitachangia. Wale wanaotaka kunichokoza ili nichangie, nimeandika program ambayo inafuta jumbe zao kuja kwangu.

Kazi njema jamani!!! sikimbii na nitarudi mungu akipenda.
 
Waanze kwanza Mbezi Beach kuna mahekalu hata hao akina Beckham hawana, wakifanikiwa pesa zitumike kufuatilia za nje kinyume cha hapo ni kubwaka tu....
 
Ninaweza onekana pessimistic kwenye hili.. Ila, si tulishaambiwa na mkuu wa PCCB kwamba marais wastaafu wana immunity? Je hiyo immunity itakuwa compromised kwenye investigation hii? Mimi nafikiri hapa tunazidi kuchezewa akili tu... We ngoja uje uone samaki wa aina gani watakaonaswa kwenye mchakato huu. Hizi nyavu zitakamata visamaki viduchu na I'm sure 100% that the biggest fish watafanikiwa kupenya (ama tayari wameshapenya) nyavuni...

Tusikubali kuendelewa kuchezewa akili jamani
 
Nasista Kusema Kuwa Unaweza Kuwa Ni Mchanga Wa Macho Kutupumbaza Na Machungu Tulonayo Juu Za Buzwagi,iptl,twin Towers.
Manake Mwanzo Mambo Ya Stars Yalifunika Sana Yakaisha Naona Wanatafuta Mengine Ya Kuzugia.kama Wakao Serious All The Best
 
Hivi wanaanza kuangalia waliotorosha kiasi gani vile?

Kwani kama wataanzia kima cha chini cha mshahara basi huenda mpaka waje wafikie hao wenye mabilioni basi watakuwa wameshakufa kwa uzee ama kuzila na kuisha na hatimaye account zikawa hazina kitu huko ngambo.
 
Back
Top Bottom