Watanzania wakimbilia Kenya kukwepa kipigo cha polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wakimbilia Kenya kukwepa kipigo cha polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Dec 14, 2007.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Watanzania wakimbilia Kenya kukwepa kipigo cha polisi

  Na Samson Chacha, Sirari

  VURUGU kubwa zimezuka katika eneo la Sirari upande wa Tanzania, mkaoni Mara kati ya polisi na raia ambao hatimaye walikimbilia nchini Kenya ili kujiokoa.

  Chanzo cha vurugu hizo ni wananchi kupinga uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Issa Machibya, kuagiza uchimbaji mashimo makubwa katika njia za panya kuingia Kenya ili kudhibiti biashara ya magendo.

  Kufuatia vurugu hizo raia hao jana waliamua kufukia mashimo hayo baada ya kufanyika mkutano kati yao na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, kisha polisi zaidi ya 30 waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya kutoa machozi walifika katika eneo hilo na kuanza kuwatawanya.

  Nguvu hizo za polisi za kuwatanya raia hao, ziliwafanya wakimbilie kuvuka mpaka na kuingia eneo la Kenya ili kujiokoa.

  Kufuatia vurugu hizo kuvuka mpaka, polisi nane wa Kenya walipinga hatua ya polisi wa Tanzania kutaka kuwashambulia na kuwakamata raia hao ndani ya mpaka wake.

  Hali hiyo ilisababisha raia hao wa Tanzania kupiga mayoye wakiunga mkono msimamo wa polisi wa Kenya.

  Msimamo wa polisi wa Kenya ulikuwa ukilenga kuliepusha jeshi hilo na kashfa iwapo kungetokea mauaji au majeruhi ya raia ndani ya nchi yao hivyo walilizuia magari ya polisi wa Tanzania yasiingie ndani ya ardhi ya nchi yao.

  Msimamo huo wa askari polisi wa Kenya, uliwalazimu askari wa Tanzania wakiongozwa na Kamanda wa Wilaya ya Tarime (OCD) Mrakibu wa Polisi Bandola, kukaa mpakani wakisubiri kuwatia mbaroni raia hao.

  Awali, katika mkutano wao na mbunge Wangwe wananchi hao walijadili mambo mbalimbali ya maendeleo na ndipo likafika suala Machibya kuchimba mashimo hayo.

  Wananchi hao kwa nyakati tofauti, walipinga uamuzi huo wakisema mashimo hayo yalichimbwa kupita katika nyumba zao.

  Licha ya kuchimba mashimo hayo, pia walipinga uamuzi wa mkuu huyo kuweka seng'enge na vyuma kupita pembezoni mwa barabara kuu ya kuingia mpakani.

  Baada ya mkutano huo, wananchi walikubaliana kufukia mashimo hayo ndipo polisi walifika katika eneo hilo na kuanza kuwatanya na wao wakakimbilia Kenya.

  source mwananchi
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  AMANI NA UTULIVU KWA KWENDAMBELE!!!!!!!!!!!!!!!!!,,

  Ni mwendo wa Amri toka juu asubuhi hadi jioni, siku hadi mwaka.., TUTAFIKA LAKINI.
   
Loading...