Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
Sasa ni dhahiri watanzania wamekataa siasa za chuki na ugomvi na badala yake wanataka wanasiasa kuhubiri amani na upendo kwa maendeleo ya Taifa lao.
Itakumbukwa mwezi Juni na Julai kulikuwa na uchaguzi mdogo wa Kata 26 ambapo awamu ya kwanza ulifanyika Juni 16 kwa Kata 22 na Julai 14 kwa kata 4.
Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba aliweka Kambi katika kata 10.Kwa mujibu wa vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii, kiongozi huyo aliripotiwa kumwaga kila aina ya kashfa kwa chama cha CHADEMA na hususani viongozi wake wakuu.
Kiongozi huyo alikuwa anazunguka na kijana anayeitwa Mussa Tesha akidai kwamba alimwagiwa Tindikali na Chadema.Mwigulu alidai Chadema ni chama cha kigaidi na kamwe kisichaguliwe kwa sababu kinataka kusambaratisha Tanzania.Alikuwa akiyasema hayo huku akijua fika ameshinikiza kukamatwa makada wa Chadema na kufunguliwa kesi ya ugaidi ili wasipate dhamana.Kwa hiyo hotuba zake tayari zikawa zimeshaihukumu Chadema bila hata kesi ya Tindikali haijasikilizwa.
Kama vile haitoshi kiongozi huyo alikuwa akizunguka na vijana wawili waliofukuzwa Chadema Mtela Mwampamba na Juliana Shonza.
Vijana hawa nao badala ya kueneza sera za chama chao kipya wakawa kila wanapopanda Jukwaani ni kuwashambulia tena kwa matusi viongozi wakuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa na Freeman Mbowe.Pia wakawa wanawatukana Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mwanachama maarufu wa Chadema Ben Saanane ambaye alikuwa chanzo cha kufichua njama za vijana hawa na hatimaye kufukuzwa Chadema.
Hatimaye Watanzania wakazungumza kupitia sanduku la kura na katika hali ya kushtusha CCM ikashindwa katika kata zote alizoweka kambi Mwigulu Nchemba na vijana wake Mtela Mwampamba na Juliana Shonza.
Yafuatayo ni matokeo ya kata zote ambazo Mwigulu Nchemba aliweka Kambi.
Iseke Singida
CDM 831
CCM 791
Nyampulukano Sengerema
CDM 1483
CCM 1088
Bashnet Manyara
CDM 2008
CCM 1130
Iyela Mbeya
CDM 1918
CCM 1163
Ifakara Kilombero
CDM 4353
CCM 3723
Dongobesh Mbulu
CDM 1558
CCM 974
Kimandolu Arusha
CDM 2761
CCM 1163
Themi Arusha
CDM 674
CCM 326
Kaloleni Arusha
CDM 1470
CCM 330
Elerai Arusha
CDM 2047
CCM 1471
Wananchi kadhaa waliohojiwa na vyombo vya habari walilaani tabia ya wanasiasa kusimama Jukwaani na kuporomosha matusi dhidi ya wapinzani wao.Wametoa onyo kali kwa wanasiasa wenye tabia hizi waache mara moja vinginevyo vyama vyao vitafutika katika historia.
Wananchi wamesema wanachotaka kusikia ni sera za chama husika vinginevyo propaganda zimepitwa na wakati na adhabu kubwa kwa wanasiasa hao ni kuviadhibu vyama vyao kwenye sanduku la kura.
Kwa matokeo hayo inabidi Mwigulu Nchemba ajitathmini kama anatosha kwenye nafasi aliyokabidhiwa na chama chake.Pia anapaswa afahamu yeye na vijana wake waliofukuzwa Chadema wameiteka CCM kwa siasa zao za chuki na matusi na watanzania wanaitazama CCM kwa jicho hilo.Isitoshe Katibu Mwenezi CCM Nape Nauye anaonekana kana kwamba hana kazi ya kufanya kwani Mwigulu na vijana wake hawa ndiyo wamekuwa wasemaji na taswira ya CCM