Watanzania wa diaspora: sensa, ID mpya etc

Mwali

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
7,014
5,610
Salaam kwa wote, Eid Mubarak kwa ndugu zangu waislam!
shkamoo kwa wakubwa na maaraba kwa wdogo zangu wote.

Wanajamvi, kuna mdogo wangu anasoma Kenya,
kanipigia sim kuniuliza kuhusu sensa, na hizi ID mpya.
Anataka kujua inakuaje kwa watanzania wanao ishi nje ya nchi?
itabidi arudi au kuna utaratibu wowote wa serikali kuwasajili hao compatriotes walio nje?

Huyu mdogo wangu ni Mtanzania ila familia yake
ilihamia Kenya toka 2002, yeye akiwa bado 9 years.
Kwa muda wote huu alikua akitumia ID ya baba yake (Baba Mkubwa kwangu)
na sasa ana miaka 19. Alipoenda kujiunga university walimlazimisha kupeleka ID,
akapeleka his EAC passeport, na ikakubaliwa.

That is the only ID he has. inatosha kwa kupata ID mpya?
hana hata cheti cha kuzaliwa, kilipotea wakati wa kuhama.
Ba mkubwa nae anatumia passport ya dharura
(emergency travelling document, ile ya karatasi A4).

mdogo wangu angependa kutumia nafasi hii ya sensa
au usajili wa ID mpya kutafuta passport mpya
maana amepanga kuendelea masomo yake ughaibuni.
Nawaombeni wana JF, nisaidieni kuelewa yafwatayo:

  1. Ni lazima a-participate katika sensa? anaweza kuparticipate ubalozini?
  2. Atapataje ID mpya? aende ubalozini au arudi Tanzania?
  3. Itakua rahisi/ngumu kiasi gani kwake kupata passport ikiwa hapati ID mpya (Kumbuka hana cheti cha kuzaliwa, ana EAC passport peke yake)

Asanteni wote kwa majibu mtakayo toa.
 
Hmmm...huyo ni mbona ni kama wewe mwenyewe Mwali....
Kha! Huyu ni mtoto wa Bamkubwa, anasoma USIU Nairobi.
Mi mtu mzima, nina kitambulisho na sina safari za nje.
Mwenzangu vipi? umeshiriki sensa? Ume-aidantifiwa?
 
Kha! Huyu ni mtoto wa Bamkubwa, anasoma USIU Nairobi.
Mi mtu mzima, nina kitambulisho na sina safari za nje.
Mwenzangu vipi? umeshiriki sensa? Ume-aidantifiwa?

Not to derail.

But...

Mwali mtu mzima?

Kiranga anaweza kuwa mpole.
 
Not to derail.

But...

Mwali mtu mzima?

Kiranga anaweza kuwa mpole.
Sasa hapa itabidi mods wanibadilishie heading ya thread,
kuanzia hii post tujadili maana ya neno "utu uzima" kwanza
 
Kha! Huyu ni mtoto wa Bamkubwa, anasoma USIU Nairobi.
Mi mtu mzima, nina kitambulisho na sina safari za nje.
Mwenzangu vipi? umeshiriki sensa? Ume-aidantifiwa?

Aaah mie tena....mbona nshafanya hivyo kitambo.
 
Sasa hapa itabidi mods wanibadilishie heading ya thread,
kuanzia hii post tujadili maana ya neno "utu uzima" kwanza

Huna dogo.

Mtu nusu yukoje?

Unanikumbusha nilivyokuwa na mjadala kuhusu dhana ya "mtoto wa mkubwa", nikaipinga kwa kuuliza kwani kuna "mtoto wa mtoto"? Kuweza kuwa na mtoto ndo ukubwa wenyewe huo.

Kwa hiyo labda katika muktadha huo, mtu mzima kinyume chake ni mtu mgonjwa.

Na hata mtoto, seuze mwali, anaweza kuwa mtu mzima.
 
Niliposema mimi ni mtu mzima lengo langu lilikua
kujitofautisha na huyo kijana ambae mwaka huu
ndio mara yake ya kwanza kujitafutia kitambulisho.
Mimi "mtu mzima" sababu nina miaka kadhaa natumia
kitambulisho changu mwenyewe, sio cha mzazi.
 
Hahitajiki kuhesabiwa kwa sababu watahesabiwa wale waliolala tz usiku wa jmosi tarehe 25. Kuhusu id kwanza inabidi atambuliwe kama mtanzania kwa kuthibitisha uraia wake kupitia wake kwenye relevant bodies hapo anaweza kupata hati zote za kusafiri na kusoma nje kama Mtanzania. Issue ya yeye kurudi bongo kuhesabiwa haina maana, ndugu zake wanafamilia waliopo tz wataulizwa kama wanandugu aishie nje nao watajibu. Kuhusu id zinatolewa kwa wakazi wa bongo hata kama sio wabongo. Siku akija bongo watampatia.
 
Hilo la sensa linamake sense.
Ila kwa upande wa ID ningeomba unifafanulie kidogo
atapaje ID bila birth certificate? PP yake ya EAC inatosha?
Au akija itabidi tena atafute mashahidi, nyumba kumi etc?
 
Hilo la sensa linamake sense.
Ila kwa upande wa ID ningeomba unifafanulie kidogo
atapaje ID bila birth certificate? PP yake ya EAC inatosha?
Au akija itabidi tena atafute mashahidi, nyumba kumi etc?

Alizaliwa mwaka gani? hospitali gani?
 
alizaliwa April 1993. Anajua hospitali.
unadhani wanaweza kua na records?

Nitashangaa sana wakiwa hawatunzi kumbukumbu kama hizo manake hiyo 1993 ni juzi juzi tu.

Ingekuwa labda kazaliwa mwaka 19 kweusi kama mimi hapo ningeelewa.

RITA pia amejaribu kwenda?
 
Nitashangaa sana wakiwa hawatunzi kumbukumbu kama hizo manake hiyo 1993 ni juzi juzi tu.

Ingekuwa labda kazaliwa mwaka 19 kweusi kama mimi hapo ningeelewa.

RITA pia amejaribu kwenda?
Hajajaribu chochote, anapima kwanza urefu wa maji.
 
Back
Top Bottom