Watanzania tuzitambue na kuzithamini juhudi za Rais Samia Suluhu

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Wasalaam

Kama unatafakari vizuri sana na kuwa na matumizi sahihi ya akili yako, basi utaniunga mkono katika hoja tajwa hapo juu, pia kuziunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu.

Ni ukweli usiopingika kuwa, mtangulizi wa Mama yetu huyu, alivuruga na kuleta taratibu nyingine ambazo zilikuwa zikienda kinyume kabisa na sharia na katiba ya nchi.

Rais Dkt. Samia, yupo katika hatua ya kuireform nchi, ameleta maridhiano baina ya chama chake na vyama vingine, na hili limewezekana, Ajira ambazo zkmekuwa kirio cha muda mrefu ameendelea kutatua kwa kuajili watu katika serikali yake kinyume kabisa na mtangulizi wake.

Miradi mikubwa mikubwa ambayo wengi walidhani ingeshindikana inazidi kukamilishwa Siku hadi siku, ujenzi wa madarasa, madaraja na na vituo mbali mbali vya afya vinakamilishwa Siku baada ya siku, watoto under five wote wanatibiwa bure bila kubaghuliwa, wazazi wanajifungua bure kabisa bila gharama yoyote (kinyume kabisa na mtangulizi wake ambaye siasa zilitawala sana tofauti na uhalisia).

Rais wetu Dkt. Samia, anajipambanua si tu kwa uongozi wake, Bali pia upendo na utu bila kujali tofauti ya itikadi za vyama , leo hii hakuna wasiojulikana, leo hii Ruksa kwa vyama pinzani kuendelea na utaratibu wa kikatiba wa mikutano ya hadhara, leo hii kila mwananchi yupo huru bila kuhofia usalama Wake.

Tuna kila sababu ya kutambua juhudi na kumuunga mkono rais Dkt. Samia

Samia Suluhu Hassan for Tanzania

Mimi sio chawa.

Nayeyuka kitahilatahila.
 
Back
Top Bottom