Watanzania tuwe na utamaduni wa kutembea haraka ,Mimi nadhani itaongeza uchapakazi

Kwa waliosoma life skills kutembea haraka ni moja ya vigezo muhimu vya kustaarabika na uchapakazi .Tanzania utamaduni wa kutembea haraka haupo yaani watu wanatembea kama waliochoka ndo maana hata nchi yetu ina sifa ya watu wasiokuwa na furaha kadri ya takwimu kwa sababu ya watu kutembea kama vile wamekula sijui nini,ukitembelea mitaa mingi ya dar hata mwanza watu wanatembea kama hawana kazi za kufanya yaani wengi wanatembea sijui kusharobaro wengine wakinengua hasa mademu halafu tunasema nchi ya uchumi wa kati kufikia 2025 .hebu tazama nchi za wazungu watu wanatembea haraka hata baadhi nchi za Africa kama Kenya na south Africa movement zao zina uharaka tofauti ilivyo bongo.utamaduni wa kutembea haraka unapaswa uwepo kwenye nchi inayotaka kupiga hatua
Wewe unaona mbali sana! Yote uliyisema naunga mkono 100%.
Hata utembeaji sasa ulivyo wa hovyo kwa hawa watz ni noma.
 
Namshukuru nimewahi kufundishwa na Ma-Prof kutoka USA, Canada, Uingereza, Russia, India, SA, Scotland yaani hawapotezi muda. Dakika 5 kabla ya kipindi mtu yupo mlangoni anasubiri. Na ikitokea siku ya kazi imeangukia kwenye public holiday lazima atafute muda wa kufidia. Hakuna nyoronyoro kama hawa wahadhiri wetu. Kama pale UDSM unaweza kuta mhadhiri haingii class wiki tatu nzima bila sababu za msingi. Baada ya hapo analeta slides za kufa mtu na kutangaza test ndani ya siku mbili.
Ukweli mtupu
 
Hii tabia na ile ya kusimama kumsalimia mtu njian kisa unamfaham vinanikera sana kwa kweli, nasema kutoka moyoni, mimi hata naenda kushiriki mkate wa bwana kanisan nakua wa kwanza na nikfka pale anajivuta vuta niokote mwenyewe nile nisepe. Nachukia watu slow sana kwa kweli nina visa ving vya kukosana na watu waliotaratbu siwezag kuvumilia kbsa.
 
Hakika umenena mkuu. Kuna watu wapuuzi sana utakuta limeziba njia linaenda taratibu kama konokono. Hata baadhi ya waendesha magari barabarani
 
Kizazi kisichosoma vitabu! Mbona hizo ni life skills zinafundishwa form two na hata darasa la sita.
1,tembea kwa kujiamini na kwa haraka.
2,Ongea kwa sauti inayosikika usipayuke au kunong'ona.
3,usigeukegeuke nyuma bila sababu.
4,kaa kushoto kwa barabara.
5,usichekecheke kama zuzu.
6,usitumie dk nyiiingi kusalimia watu njiani.
7,kama huna sababu ya muhimu usimtembelee mtu alfajiri.
sio..ukae..kulia,mkuu..kwa..barabara..zetu..za..bongo..ili,uone..gari..inapokuja,mbele..yako?
 
kweli mwendo can tell the whole story ya mtu fulani,kutembea taratibu ni dalili kubwa ya kukata tamaa ,slow people,slowest nation
 
Yaan makonda anipangie mda WA kuondok bar na wew pia unipangie mwendo kwel?
 
Kwa waliosoma life skills kutembea haraka ni moja ya vigezo muhimu vya kustaarabika na uchapakazi .Tanzania utamaduni wa kutembea haraka haupo yaani watu wanatembea kama waliochoka ndo maana hata nchi yetu ina sifa ya watu wasiokuwa na furaha kadri ya takwimu kwa sababu ya watu kutembea kama vile wamekula sijui nini,ukitembelea mitaa mingi ya dar hata mwanza watu wanatembea kama hawana kazi za kufanya yaani wengi wanatembea sijui kusharobaro wengine wakinengua hasa mademu halafu tunasema nchi ya uchumi wa kati kufikia 2025 .hebu tazama nchi za wazungu watu wanatembea haraka hata baadhi nchi za Africa kama Kenya na south Africa movement zao zina uharaka tofauti ilivyo bongo.utamaduni wa kutembea haraka unapaswa uwepo kwenye nchi inayotaka kupiga hatua
Hii sifa ya kutembea haraka,wakati fulani wanayo hata vibaka. Siyo determinant ya uchapakazi.
 
Unaongea ukweli tupu. hakuna jambo huwa linanikera kama watembea kwa miguu Bongo.

Watu hawana haraka anatembea kama njia yake. Halafu wanawake ndiyo wanakera unakuta anatembea ni kafupi kamejaza njia na mikono anairusha kote kama panga la helkopita.

Tembea A/dam uone watu walivyo na haraka ukiwa slow hadi unajistikia.
Nimecheka kwa sauti mpk kila mtu ananitizama hv natembea tembea tu mtaani huku nikisoma huu uzi
 
Back
Top Bottom