Mhhhhh! Inafurahisha kusoma, ni jambo la kupongezwa endapo hii move itabakia positive na tukawa na positive thinking, tukubali kutokubaliana, tuelewe kuwa wengine wanaweza kuwaza tofauti na namna tunavyowaza, tutambue pia kuwa kuna mambo ambayo tukiyaandika mbele ya kadamnasi aidha tunajishushia staha yetu ama ya jamii husika, na pia tujaribu kuwa mifano kwa wanachama wapya wanaoitembelea JF na kuonyesha ukongwe wetu kwa kuwaelekeza pale wanapokosea.
Aidha, mods si malaika, wanaweza kukosea. Tujitahidi kuwaelekeza kiungwana, tujaribu kuvaa viatu vyao na kushika nafasi zao kujiuliza ingekuwa vipi tungekuwa sisi ndio tunaihudumia hadhira hii, tukiwakosoa kistaarabu ni wazi watarekebisha madhaifu yao na kuwa watumishi wetu wasio na mishahara lakini msaada mkubwa kwetu.
Naupongeza uamuzi wako mkuu Dsm pamoja na Mganyizi, tunapofunga mwaka uwe ni mwanzo wa ukurasa mpya, ya kale yapite na tuyagange yajayo; tusiendelee kuumizwa na makovu ya uchaguzi, tuwe mfano kwa wanasiasa, siamini kama kuna mtu anafurahishwa na mwanasiasa asiyeaminika au fisadi, haijalishi yuko ndani ama nje ya chama chako.
Mwaka ujao tuhakikishe tunajihadhari na udini, tuwakemee wanaotaka kulipeleka taifa huko n.k; tujaribu kujiepusha na kujadili maisha binafsi ya watu, kuna mambo ambayo ni wazi mtu unapoyaongelea aidha unakuwa umedhamiria kumchafua mtu kwa malengo flani lakini pengine kujadili maisha binafsi ya mtu yanawasaidia wengine kutambua uzuri na ubovu wa mhusika (japo inakera/kuuma).
Nawatakia kila la heri kuelekea mwisho wa mwaka 2010!