zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Wana JF wote, wenye mtazamo na itikadi kama zangu, ziwe za kidini, kisiasa au kijamii na wale wenye itikadi tofauti na zangu.
Naomba kwanza kuomba radhi kwa wote niliyowaudhi kwa sababu tu ya tofauti za itikadi zetu na muono wetu. Binadam hatujakamilika, naomba nimnukuu Nyerere, alipohutubia pale Mbeya, alisema, hata yeye alifanya makosa katika uongozi wake, na tuyaache yale mabaya na tufate yale mazuri (just quoting from my head, it may not be a word to word quotation).
Hali kadhalika, mimi ni Binaadam, na haiwezekani nikawa na mema na mazuri tu siku zote, kuna mabaya niliyoyaandika kwa mtazamo wa tunaye hitilafiana kiitikadi, ingawa kwangu nayaona mazuri, kuna ghadhabu na hasira katika kukandamiza hizi key board, inafikia kumjibu mtu mambo ambayo yatamkera au yatawakera wengi. Naomba wote niliowaudhi, niliowatolea lugha ambayo hairidhishi wanisamehe sana.
Sina kusudio baya kwa Ama mTanzania yeyote au Binadamu yeyote, no matter ni wa chama kipi au wa dini ipi au awe hana dini.
Maisha yangu yote nimeishi na watu wa itikadi tofauti, fikra tofauti, hata anti zenu (kwa wale wadogo kwangu ki umri) nyumbani tuliyeishi kwa zaidi ya miaka 32 (mkubwa) na zaidi ya miaka 17 (mdogo) kwenye ndoa za halali, hutokea tukakwaruzana, lakini hufikia kusameheana na kuendelea na maisha.
Naomba msamaha kwa wana JF niliowakosea na naomba tusichukiane kwa ama itikadi au imani zetu.
Nna uhakika kuwa tupo hapa jamvini kwa ajili ya kuipenda nchi yetu nzuri. Na nchi nzuri, haiwezi kuwa nzuri bila ya kuwa na watu wazuri na wenye kusameheana. Na bila ya kuwa na watu wenye kuhitilafiana na mwishowe wakakaa chini na kutatuwa maatatizo yao kwa ajili ya kuendeleza nchi (yao) yetu na kuwawachia warithi wetu nchi yenye thamani, kimaadili, kiitikadi na kiimani.
Natumai mtanisamehe kwa niliowakosea na mimi nawasamehe wote niliohisi au kufikiri kuwa wamenikosea.
Tuendelee jamvini, tupingane lakini tupendane, kama wapenzi wa Simba na Yanga, ni mahasimu wa jadi lakini wanapendana na kila mmoja akimkosa mwenzake basi huwa hana raha. Hali kadhalika humu JF, kama hatuna kupingana kwa tunayopingana patakuwa hapana raha humu jamvini.
Kwa mara nyingine tena: Naomba mnisamehe na tusameheane.