Watanzania Tusameheane

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,062
0
Wana JF wote, wenye mtazamo na itikadi kama zangu, ziwe za kidini, kisiasa au kijamii na wale wenye itikadi tofauti na zangu.

Naomba kwanza kuomba radhi kwa wote niliyowaudhi kwa sababu tu ya tofauti za itikadi zetu na muono wetu. Binadam hatujakamilika, naomba nimnukuu Nyerere, alipohutubia pale Mbeya, alisema, hata yeye alifanya makosa katika uongozi wake, na tuyaache yale mabaya na tufate yale mazuri (just quoting from my head, it may not be a word to word quotation).

Hali kadhalika, mimi ni Binaadam, na haiwezekani nikawa na mema na mazuri tu siku zote, kuna mabaya niliyoyaandika kwa mtazamo wa tunaye hitilafiana kiitikadi, ingawa kwangu nayaona mazuri, kuna ghadhabu na hasira katika kukandamiza hizi key board, inafikia kumjibu mtu mambo ambayo yatamkera au yatawakera wengi. Naomba wote niliowaudhi, niliowatolea lugha ambayo hairidhishi wanisamehe sana.

Sina kusudio baya kwa Ama mTanzania yeyote au Binadamu yeyote, no matter ni wa chama kipi au wa dini ipi au awe hana dini.

Maisha yangu yote nimeishi na watu wa itikadi tofauti, fikra tofauti, hata anti zenu (kwa wale wadogo kwangu ki umri) nyumbani tuliyeishi kwa zaidi ya miaka 32 (mkubwa) na zaidi ya miaka 17 (mdogo) kwenye ndoa za halali, hutokea tukakwaruzana, lakini hufikia kusameheana na kuendelea na maisha.

Naomba msamaha kwa wana JF niliowakosea na naomba tusichukiane kwa ama itikadi au imani zetu.

Nna uhakika kuwa tupo hapa jamvini kwa ajili ya kuipenda nchi yetu nzuri. Na nchi nzuri, haiwezi kuwa nzuri bila ya kuwa na watu wazuri na wenye kusameheana. Na bila ya kuwa na watu wenye kuhitilafiana na mwishowe wakakaa chini na kutatuwa maatatizo yao kwa ajili ya kuendeleza nchi (yao) yetu na kuwawachia warithi wetu nchi yenye thamani, kimaadili, kiitikadi na kiimani.

Natumai mtanisamehe kwa niliowakosea na mimi nawasamehe wote niliohisi au kufikiri kuwa wamenikosea.

Tuendelee jamvini, tupingane lakini tupendane, kama wapenzi wa Simba na Yanga, ni mahasimu wa jadi lakini wanapendana na kila mmoja akimkosa mwenzake basi huwa hana raha. Hali kadhalika humu JF, kama hatuna kupingana kwa tunayopingana patakuwa hapana raha humu jamvini.

Kwa mara nyingine tena: Naomba mnisamehe na tusameheane.
 
Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,099
2,000
Mhhhhh! Inafurahisha kusoma, ni jambo la kupongezwa endapo hii move itabakia positive na tukawa na positive thinking, tukubali kutokubaliana, tuelewe kuwa wengine wanaweza kuwaza tofauti na namna tunavyowaza, tutambue pia kuwa kuna mambo ambayo tukiyaandika mbele ya kadamnasi aidha tunajishushia staha yetu ama ya jamii husika, na pia tujaribu kuwa mifano kwa wanachama wapya wanaoitembelea JF na kuonyesha ukongwe wetu kwa kuwaelekeza pale wanapokosea.

Aidha, mods si malaika, wanaweza kukosea. Tujitahidi kuwaelekeza kiungwana, tujaribu kuvaa viatu vyao na kushika nafasi zao kujiuliza ingekuwa vipi tungekuwa sisi ndio tunaihudumia hadhira hii, tukiwakosoa kistaarabu ni wazi watarekebisha madhaifu yao na kuwa watumishi wetu wasio na mishahara lakini msaada mkubwa kwetu.

Naupongeza uamuzi wako mkuu Dsm pamoja na Mganyizi, tunapofunga mwaka uwe ni mwanzo wa ukurasa mpya, ya kale yapite na tuyagange yajayo; tusiendelee kuumizwa na makovu ya uchaguzi, tuwe mfano kwa wanasiasa, siamini kama kuna mtu anafurahishwa na mwanasiasa asiyeaminika au fisadi, haijalishi yuko ndani ama nje ya chama chako.

Mwaka ujao tuhakikishe tunajihadhari na udini, tuwakemee wanaotaka kulipeleka taifa huko n.k; tujaribu kujiepusha na kujadili maisha binafsi ya watu, kuna mambo ambayo ni wazi mtu unapoyaongelea aidha unakuwa umedhamiria kumchafua mtu kwa malengo flani lakini pengine kujadili maisha binafsi ya mtu yanawasaidia wengine kutambua uzuri na ubovu wa mhusika (japo inakera/kuuma).

Nawatakia kila la heri kuelekea mwisho wa mwaka 2010!
 
MpendaTz

JF-Expert Member
May 15, 2009
1,827

Ingefaa kila aliyewahi kumkashifu mwingine hapa kwa sababu yoyote ile kuiga mfano huu.
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
10,471
2,000
A Great Thinker, nimependa bandiko lako...
Binafsi sina kumbu kumbu za kukerwa na wewe ila nimekusamehe....
na mimi si umenisamehe Bana?
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,456
2,000
Kuna harufu ya rushwa hapa! Msamaha utatolewa kama DR. Dau ataomba msamaha wa watoto waliokufaTabora kwa uzembe wake, ayajiuzuru mara moja bila masharti, EL atajiuzuru bila masharti kwenye nyadhifa zote na kuendelea kwenye buashara zake, RA atajiuzulu nafasi zake zote na kurudishwa pesa za walipa kodi bila masharti yoyote, JK ataomba msamaha wa Wizi wa kura na kujiuzulu na uchaguzi mpya kufanyika. Tukifika hapo utasamehewa wewe pamoja na wao.

Tena uwaambie hizi nahau zao na hadithi za Pwagu na Pwaguzi haziwasaidii.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom