Laana ya kuwasaliti mababu zetu na mila zetu nzuri imetupa ufukara kama taifa

Elvis Legacy

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
3,388
4,721
Asalaam

Watanzania wenzangu. Pasipo na shaka yoyote nimejiridhisha kuwa tupo katika kifungo cha ufukara kutokana na laana za kuwasaliti mababu zetu na mila zetu nzuri.

Naomba tuungane kwa kuombea laana hizi zitutoke tuwe huru na hatimaye tupige hatua kimaendeleo.

1.Tukemee laana ya vijana na wazee kutumia muda mwingi kujadili Simba na Yanga kuliko mstakabali na maslahi ya nchi kama kupatikana kwa katiba mpya itakayowawajibisha watawala na kuwapa wananchi nguvu ya maamuzi kwenye nchi yao.

2. Tukemee laana ya kuchagua viongozi wajinga kuanzia mtaa,kata,jimbo hadi taifa. Tuombe mababu zetu watuoneshe viongozi wanaofaa sio kuchagua kwa itikadi zao za vyama.

3. Tukemee laana ya uoga wa kutetea haki zetu, uvivu wa kifikiri, na kutokuwa na maono ya mbali ili kulikomboa taifa letu kwa hawa wakoloni weusi.

4. Tukemee laana ya kufanywa vikaragosi wa kukimbiza moto mchana.

Mengine mtaongezea. Mwaka 2024/2025 tukapate viongozi sio watawala.

Watakatifu mababu na mabibi zetu tunaomba mtusamehe kwa kuwasaliti na tutaenzi mila zote nzuri mlizotuachia. Zile mbaya mtatusamehe.
 
Naunga mkono hoja, hakika tumelaanika kujifanya Wakristu na Waislam. Yaani tunaabudu dini ambazo hazina umuhimu wowote maishani mwetu sie Waafrika na kutufanya watunmwa wa imani potofu.

Miaka 500 ilipita Waafrika tulikuwa na utajiri mkubwa duniani na Waarab pamoja na Wazungu wakiwa na vitabu vyao vya kutungwa na wao wenyewe (Biblia na Qur'an).

Sasa sisi Waafrika ndiyo tuna vitabu vyao kwa wingi huku wao wakibakiwa na mali / utajiri wetu. Kutokusoma kunarudisha nyuma sana jamii zetu haswa Waislam.
 
Asalaam

Watanzania wenzangu. Pasipo na shaka yoyote nimejiridhisha kuwa tupo katika kifungo cha ufukara kutokana na laana za kuwasaliti mababu zetu na mila zetu nzuri.

Naomba tuungane kwa kuombea laana hizi zitutoke tuwe huru na hatimaye tupige hatua kimaendeleo.

1.Tukemee laana ya vijana na wazee kutumia muda mwingi kujadili Simba na Yanga kuliko mstakabali na maslahi ya nchi kama kupatikana kwa katiba mpya itakayowawajibisha watawala na kuwapa wananchi nguvu ya maamuzi kwenye nchi yao.

2. Tukemee laana ya kuchagua viongozi wajinga kuanzia mtaa,kata,jimbo hadi taifa. Tuombe mababu zetu watuoneshe viongozi wanaofaa sio kuchagua kwa itikadi zao za vyama.

3. Tukemee laana ya uoga wa kutetea haki zetu, uvivu wa kifikiri, na kutokuwa na maono ya mbali ili kulikomboa taifa letu kwa hawa wakoloni weusi.

4. Tukemee laana ya kufanywa vikaragosi wa kukimbiza moto mchana.

Mengine mtaongezea. Mwaka 2024/2025 tukapate viongozi sio watawala.

Watakatifu mababu na mabibi zetu tunaomba mtusamehe kwa kuwasaliti na tutaenzi mila zote nzuri mlizotuachia. Zile mbaya mtatusamehe.
We umechanganyikiwa, umaskini wako na wa ukoo wenu ni uzembe wenu usitafute pa kujificha.
 
Naunga mkono hoja, hakika tumelaanika kujifanya Wakristu na Waislam. Yaani tunaabudu dini ambazo hazina umuhimu wowote maishani mwetu sie Waafrika na kutufanya watunmwa wa imani potofu. Miaka 500 ilipita Waafrika tulikuwa na utajiri mkubwa duniani na Waarab pamoja na Wazungu wakiwa na vitabu vyao vya kutungwa na wao wenyewe (Biblia na Qur'an). Sasa sisi Waafrika ndiyo tuna vitabu vyao kwa wingi huku wao wakibakiwa na mali / utajiri wetu. Kutokusoma kunarudisha nyuma sana jamii zetu haswa Waislam.
Mada haihusu dini lakini
 
Hicho ni kichaka tu kama vichaka vingine. Umaskini wako hauna uhusiano wowote na dini wala mazingira yako.

Tatizo limo akilini mwako. Acha kuwasingizia Wakoloni, kwa sababu bila wao huenda hadi sasa ungekuwa msituni ukiwinda swala kwa ajili ya kitoweo.

Kama huoni maendeleo ambayo yamekuja na ukoloni, basi upofu wako ni wa sayari nyingine.

Halafu hizo dini unazotaja zimekuwepo muda mrefu tu kabla ya ukoloni. Amka usingizini!
 
Fika mkoa ama wilaya yeyote hapa Tanzania ambao wananchi wake wanaendekeza Uislam, angalia maisha yao kisha rudi hapa tuyajenge.
 
Uchumi kuanguka, upendo ktk jamii kupungua, maarifa ya watu kupungua, chuki kuongezeka, maovu kuongezeka, umasikini kuongezeka.

Hayo yote ni matokeo ya laana za kukumbatia dini, na tutaendelea kushuhudia makubwa zaidi kama hatutaamka na kuzikemea hizo dini.

Hakuna maendeleo kwa yule anaekumbatia utamaduni usiomuhusu zaid ya laana na mikosi.

Matatizo yote afrika yameletwa na Dini.
 
Back
Top Bottom