Watanzania Tusali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Tusali.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BIG X, Jun 29, 2012.

 1. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwenyezi Mungu tunashukuru kwa upendo wako unaotupa waTanzania, tunashukuru kwa kutupatia CDM yenye viongozi wenye nia ya dhati kutukomboa kutoka kwenye mikono ya mafisadi.

  Tunashukuru kwa kutupa viongozi jasiri kwenye vyama vyetu vingine ambao wameonyesha nia ya dhati kubadilisha upepo unaonuka kwa waTanzania, mfano mzuri ni Dakatari wetu Ulimboka. Tunashukuru uliweza muepusha Daktari ulimboka na kifo, mapenzi yako haya tunajua yana nia ya kuwafichua mashetani ndani ya nchi, tunaomba mapenzi haya yatimizwe sasa.

  Tunajua shetani naye (CCM na wasaidizi wake) wanafanya kujitahidi kila njia kukwamisha yale wewe Mungu ulipanga kuwapatia waTanzania wawe na maisha mazuri. Tunaomba huyu shetani ashindwe sasa.

  Mwenyezi Mungu tunaomba utusaidie kuondokana na udhaifu ambao waTanzania wengi tunao katika kukabiliana na shida na haki zetu, hasa pale tunaposhindwa kabisa kudai haki zetu za msingi kwa kuogopa vitisho vya huyu shetani mkubwa na wasaidizi wake. Tunaomba uipe nguvu CDM na viongozi wake, na wale wote wenye nia ya dhati wasikate tamaa sababu tunajua shetani bado anaendelea kuweka mizizi yake.

  Mwisho tunaomba uwaponye, uwape nguvu wale wote kwa namna moja ama nyingine wameumizwa au wanapata shida zinazosababishwa na huyu shetani na wasaidizi wake.

  AMINA.
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukishasoma hiyo sala, jibu AMINA tafadhali.
   
Loading...