GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,043
- 119,616
Ni hivi punde tu nimetoka kumtembelea Msanii fulani ( wa Kiume ) ambaye mara nyingi mno huwa hakauki ama Mitandaoni au Luningani au katika Midomo yetu bila kusahau katika Magazeti mengi ya Udaku na hamuwezi amini nimekalia tu katika Kochi lake ( Sofa ) nimegongana na Kunguni wa kufa mtu. Kama na hiyo haitoshi nimeingia katika Gari lake ili anifikishe somewhere ili niweze kutiririka na kuserereka Kitaa na kwenyewe nimekutana na Mende wa kutosha tu.
Cha kusikitisha wakati nikisabahiwa / nikisalimiwa na hao Kunguni na Mende mwenzangu ( Msanii mwenye Sifa ) yeye ndiyo Kwanza hajali na anaona hao Marafiki zake Kunguni na Mende wana haki ya Kuishi katika Nyumba na Gari yake.
Mwisho nimalizie tu kwa kusema Watanzania tupunguze Sifa / Maisha ya Video / Drama / Shobo hasa katika maisha yetu pale tunapokuwa nje ya maeneo yetu ya kuishi kwani kumbe uhalisia wetu haukakisi tunavyoonekana Mitandaoni / Luningani na Magazetini.
Msanii mzima Kwako umejaza Kunguni na katika Gari lako kuna Abiria wengine Mende umewaficha. Sasa kama leo tu nimetoka kumtembelea Msanii huyu na nimekaribishwa Kwake na Mwenyeji Kunguni na Abiria Mende katika Gari lake vipi nikisema nikawatembelee na wengine ambao na wao huku nje wamejawa na Mashauzi kibao?
Nawasilisha na tuishi tu maisha yetu ya asili kisha tupunguze Sifa / Shobo ambazo Kiukweli hatufanani nazo.