Watanzania tupendane, tusaidiane, tushirikiane na tushikamane, lets stand as one. Ila pia tuelezane ukweli, why tumekula ng'ombe mzima tukabakiza mkia

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Leo ni Jumatatu nyingine, nimepata fursa za kuendelea na zile makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa”, kwa vile sakata la kushikiliwa kwa ndege yetu nchini Afrika ya Kusini, kunaendelea, nami leo naendelea na kuzungumzia kushikwa kwa ndege hiyo lakini katika muktadha wa tukio hili, lituimarishe katika uzalendo wetu kwa nchi yetu, tuongeze upendo baina yetu kwa kuipenda nchi yetu, serikali yetu na viongozi weke, na badala ya kulitumia kufarakana, tulitumie kutuongezea mshikamano baina yetu na baada ya kukombolewa kwa ndege yetu, then sisi Watanzania, tukae chini na kuambiana ukweli, na kwa uwazi bila kuficha ficha, ni nini haswa kilichosababisha mdeni wetu huyu asilipwe deni ambalo tumeishakula ngombe mzima, tukabakiza tuu mkia na kuamua kukataa kulipa.

Hili la kushikwa kwa ndege yetu ni janga, wakati wa majanga, ndipo unaweza kubaini nani ni rafiki wa kweli na nani sii rafiki, majanga badala ya kuleta tafrani na utengamano, huleta upendo, ushirikiano na mshikamano, natoa wito kwa hili la ndege, Watanzania tuungane tuwe kitu kimoja chini ya serikali yetu wakiwemo wanasiasa, vyama vyote, Watanzania wote, lets stand as one, wakiwemo CCM na Wapinzani, tuwe kitu kimoja, tusimame pamoja na serikali yetu na tuongee lugha moja na sauti moja, ndege yetu iachiwe.

Wanasiasa wa pande zote, badala ya kuanza kunyoosheana vidole nani kafanya nini, tuhubiri zaidi upendo, ili kujenga mshikamano wa kweli kwa serikali, CCM, Wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla, hili tukio, lituunganishe, lituongezee upendo wa kupendana kwa dhati, kuheshimiana, na kushirikiana kuleta maendeleo kwa taifa letu kwa sababu, its only together we can!. Maadam sote tunajenga nyumba moja ya Tanzania, tunagombea fito za nini?.

Upendo ndio amri kuu kuliko zote humu duniani ambayo Mungu ametupa. Naomba kuazima hii mistari kutoka kitabu fulani kuhusu upendo "Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno. Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote"

Kwa vile CCM ndio chama tawala na serikali yake, viongozi wake wote kuanzia juu kwa Mwenyekiti hadi kwa mjumbe wa shina, na viongozi wote wa serikali, kuanzia rais wa nchi hadi mwenyekiti wa serikali ya mtaa, wana wajibu na jukumu sio tuu la kuhubiri upendo kwa maneno tuu, bali kwa kufanya matendo yanayoashiria upendo wa kweli, (practicing what you preach) kwa kuwapenda kwa dhati Watanzania wote, na watu wote, wakiwemo wapinzani ambao nao ni Watanzania, itawaheshimu wote, haitawanyanyasa, haitawabagua, haitawadharau, haitawabeza, wala kuwa tweza na itawatendea haki, wananchi wote.

Kama serikali ya CCM itaonyesha upendo wa dhati zaidi, pia itachukua yale mazuri ya wapinzani na kuwashirikisha katika kuya implement kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Kwa kwa hali ilivyo sasa kati ya CCM na Wapinzani ni kama paka na panya, hali inayopelekea taifa linapokumbwa na majanga kama hili la kushikwa kwa ndege yetu, CCM, serikali na wale wenye mapenzi mema na taifa letu, tunaumia kuona ndege yetu imeshikwa, huku baadhi ya wapinzania na wenzetu wengine wasiolitakia mema taifa hili, wakishangilia na kubeza kila kinachofanywa na serikali ya CCM, huu sio uzalendo.

Kuna dhana imejengeka kwa CCM ikijiona ndio pekee yenye hati miliki ya kutawala taifa hili la Tanzania milele, hivyo yoyote atakayetishia status quo ya CCM kutawala milele, kuonekana kama ni adui, na sisi jf tukiwemo, hivyo CCM inawaona wapinzani kama maadui wenye lengo la kuwapokonya tonge mdomoni, au kutaka kukitia mchanga kitumbua chao, hivyo kutumia kila mbinu kuhakikisha inabakia madarakani by hooks and crooks, ikiwemo kutumia mbinu ya bao la mkono, kuminya demokrasia, kuminya uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa kukusanyika, kukandamiza upinzani hata ikibidi kuikanyaga katiba, wataikanyaga kwa lengo la kuwakomoa wapinzani kumbe wanawakomoa wapinzani sio kuwakomoa wapinzani bali ni kuwakomoa, Watanzania wenzetu.

Kwa tukio kama hili la ndege yetu kushikwa na jinsi Watanzania tulivyogawanyika, kunapelekea mtu kujiuliza, hivi sisi Watanzania tuna upendo wa kweli na upendo wa dhati miongoni mwetu sisi kwa sisi bila kujali itikadi za vyama vyetu?, jee tunaupendo wa kweli na wa dhati kwa taifa letu?, haiwezekani taifa liwe kwa majanga halafu sisi tukagawanyika. Huu sio uzalendo. Tukio hili lituunganishe tuwe wamoja na kuongea kwa sauti moja.

Tanzania ni yetu sote, hii nchi sio mali ya CCM au mtu yoyote, ni mali ya Watanzania wote wakiwemo CCM wenye dhamana ya kutawala lakini pia Wapinzani na wengine wote hata wasio na vyama ndio maana tukaweka vipengele vya haki za kila mtu na wajibu wake kwenye katiba yetu, hivyo linapotokea tatizo la kitaifa, bila kujali limesababishwa ni nini, hatua ya kwanza ni kwa sisi Watanzania, kusimama pamoja kutatua tatizo, likiisha tatuliwa, ndipo tutakaa chini kufanya tathmini ni nani aliyetufikisha hapa, tukikutana kuna ushauri mbaya, watu wawajibike na tukikuta kuna usaliti, sheria ichukue mkondo wake.

Katika kushughulika kila jambo, CCM na serikali yake wana wajibu wa kuiheshimu katiba, sheria taratibu na kanuni ili kuonyesha upendo wa dhati kwa Watanzania wote wakiwemo wapinzani, nayo pia itapendwa na wote, na kuheshimiwa na wote wakiwemo wapinzani hivyo sote tutapendane kwa dhati kama Watanzania, tutaheshimiane na kushirikiana katika shida na raha, na katika kuleta maendeleo ya taifa letu.

Kwa kuanzia, kwanza naunga mkono hoja ya heshima, ni two way traffic, kwa mkubwa aheshimu mdogo na mdogo aheshimu mkubwa. Heshima ya kweli huwa earned na sio heshima ya kuwa forced. Mzizi wa heshima ya kweli ni upendo wa dhati. Hivyo upendo ndio utangulie kwa watu wote tupendande, bila kujali tofauti zetu, ndipo heshima ya kweli ifuatie na ipatikane, kwenye upendo wa kweli kunakuwa na heshima, amani, umoja na mshikamano. Kwenye hili la ndege yetu Watanzania tushikamane na serikali yetu.

Viongozi wa chama tawala wawapende kwa dhati Watanzania wengine wote wakiwemo wapinzani, kikiwa na upendo wa dhati, CCM itawaheshimu wapinzani na wapinzani wataiheshimu CCM na kushirikiana nayo kwa pamoja kuleta maendeleo endelevu ikiwemo kuwa kitu kimoja kwenye furaha na huzuni.

Natoa wito kwa serikali yetu kuwa wakweli na wawazi, sio kuhusu nini kilichosababisha ndege yetu kukamatwa, bali nini kilichosababisha tusimalizie kumlipa deni letu mdai wetu huyu.

Kwenye maisha ya kila siku ni kawaida sana kwa binaadamu kukopa, kudaiwa au mkopo au fidia, na kiukweli kabisa kudaiwa sio kosa, kosa ni kushindwa kulipa unachodaiwa, na ikifika mahali, ukazidiwa na madeni hadi yakawa hayalipiki, unakuwa muwazi tuu kuwa deni hili ama sio realistic, halilipiki, na hivyo kukaa na mdeni wako ukamuomba myamalize, hiki ndicho kilichofanyika kati lile deni la dola bilioni 190 la Acacia, tumafanya mazungumzo tukakubali kusamehe na sasa tutalipwa kifuta machozi cha dola milioni 300.

Kwenye kesi ya Richmond, kiukweli kabisa serikali yetu ilishauriwa vibaya, tukavunja mkataba, tukashitakiwa, tukashindwa tukadaiwa fidia, tukayamaliza kimya kimya. Ndege yetu ilipozuliwa Canada, tulidaiwa tukayamaliza kimya kimya, hili deni la huyu mdai nalo tulilipa tena ngombe mzima, tukabakiza mkia tuu, serikali yetu iwe wazi ni kwa nini hatukumalizia kulipa hadi tunakuja kudhalilishwa kiasi hiki?. Tuwe wakweli ili ukweli utuweke huru.

Deni hili limekuwa likionekana kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali mwaka hadi mwaka, pamoja na madeni mengine, kwa vile sasa tumeisha umwa na nyoka, na ndege zetu bado zinapaswa kuendelea na safari za nje, chonde chode serikali yetu, tusidharau mwiba mguu wetu ukaota tende, kinga ni bora kuliko tiba, tukae na wadeni wetu, tusemezane nao kwa uzuri, ili tukio kama hili lisije kujirudia tena kwa siku za usoni.

Tanzania ni yetu wote, tupendane kwa dhati kwa upendo wa kweli, tuheshimiane, tuijenge nchi yetu kwa kushirikiana na kwa mshikamano kwenye shida na raha. Tukipendana, tutaheshimiana na tutashirikiana kuleta maendeleo ya kulijenga taifa letu na kuliletea maendeleo.

Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali
 
Tatizo Jiwe anajifanya anajuwa kila kitu kumbe anajuwa Chemistry tu na kukaanga maganda ya korosho. Jiwe anafanya nchi iendeshwe kwa tabia zake, yaani personal attributes zimekuwa ndiyo national norms.

Tulipe deni, ndege irudi then tujiandae na uchaguzi wa 2020 pengine atapatikana kiongozi mwenye charisma.
 
Tarehe saba kuna mbunge mmoja alishambuliwa bila huruma. Baadae ulikuja kutetea humu kuwa cctv zaweza tolewa muda wowote ule endapo mmiliki wake ataona inafaa hilo likapita

Mbowe amesukwasukwa sana leo mahakamani kesho lockup keshokutwa mkutano wake umevurugwa na askari kwa maelezo toka kusiko julikana. Hilo likapita
Mikutano ya kisiasa, n.k


Watumishi wanapigishwa kwata ilianza uhakiki wakavumilia uhakiki ukaisha hakuna nyongeza, madaraja yao ya mishahara sasa wanaambiwa kukaa miaka 5+ ndipo wapandishwe kwa matamshi yake mwenyewe alisema kulikoniwaongezee bora ninunue ndege
unategemea upendo unao hubiriwa hapa ufanyiwe kazi?
 
Na uombe isitokee vita kati ya Tanzania na nchi yeyote ya jirani kwa sasa, maana hujaona bado chuki na mgawanyiko uliokolezewa moto na Serikali hii ya awamu ya 5.. Vita vya Kagera 1978 wananchi walikuwa wanajitolea (bila ya shuruti) mpaka vyombo vyao vya usafiri kwa sababu ya uzalendo.. Ikitokea vita sasa, nahisi majeshi yatakayotushambulia yatapewa mpaka hifadhi na baadhi ya wananchi wengi..

Wenye mapenzi mema na nafasi za uongozi, walifanyie kazi huu ni mpasuko mkubwa sana..
 
Sikiliza Paskali hii serikali ya awamu hii haiwezi kupata baraka kwa sababu zifuatazo

1. Imemwaga machozi mengi ya raia wasio na hatia, Uvunjwaji wa nyumba za wananchi Kimara-Mbezi ni laana na itawatafuna mpaka wanaingia kaburini

2. Ni baguzi na ni katili, Ni utawala unaonuka udini haijapata kutokea, Ni only siku hizi amegundua kuwa Waislamu kumbe hawana nongwa masikini, lakini teuzi zilizofanywa na utawala huu kwa namna alivyowapiga panga waislamu katika utawala wake ni aibu kubwa. It seems jamaa aliingia pale na pre-conceived mentality kuwa hawa watu si wazuri, niwasideline n.k

3. Kutoheshimu viapo: Unapoapishwa pale uwanja wa Taifa, Ukasomewa dua na Askofu na Sheikh Mkuu, kwa aya nzitonzito maana yake unashuhudiwa na malaika, Then ukitoka hapo ukaanza kutoheshimu viapo ulivyoapa kama vile kuheshimu sheria na katiba, nakuambia kila utakachogusa hakitofanikiwa, kazi yako inakosa baraka, maana umelitaja Jina la MUNGU bure

Kama unabisha Paskali watchout, LAZIMA abadiri nyendo zake la sivyo kila atakachogusa kitaparanganyika tu na hatoacha legacy yoyote ya maana!
 
“Kwa Maslahi ya Taifa” kwako ni pale tu unapoishabikia serikali!!!

Ukiwa na hoja mbadala au kupingana na hoja za serikali wewe sio “Kwa Maslahi ya Taifa”!

Huo mrengo wako ni wa hovyo sana ku-view people that way!

Siwezi shirikiana na serikali au kusimama nayo kwa chochote cha kipumbavu wakifanyacho kama hili suala la ndege!

Never!

Kashirikianeni na hao hao incompetent embaciles !

Hunikuti kwenye huo upumbavu!
 
Kuna kipind China ilikua na Vita vya wenyew kwa wenyew, mjapan akawavamia, wakaungana China yote against Japan. Ila hapa kwet part supremacy ishaharb, wao ndo Kila kitu mkw mpinzan kwao we aduo
 
Kama ulifuatilia sherehe za kupokea ndege zile pale JKNIA utakubaliana nami hadhira ile ilikuwa sio malengo ya kupokea ndege bali sherehe za kuwang'ong'a wapinzani utadhani ni ndege za ccm.
Kebehi ilikuwa kubwa sana, hata majuzi ndege ilipofanyiwa matumizi mabaya ya kwenda Chato kwa sababu ya matambo tuu walipohoji watu wakajibiwa kanunua mwenyewe (yaani magu) msimpangie matumizi.
Sasa iweje Leo ndege ishikwe mnataka tulie pamoja? Imeshakuwa ya wote na sio "yenu" tena?
Hakika kila nisomapo kuhusu kushikwa kwa ndege naagiza tena bia yangu bariiiiidi najipoza.
Na Leo nilipoona utetezi huko SA eti ndege ni ya rais wamekosea kuishika kwani anapata shida kwenda safari za nje! nimecheka mpaka kamasi limetoka
 
Back
Top Bottom