Watanzania tunajua kwamba bei ya kupata hati ya kusafiria ni Tsh 150,000

Achana naye huyo hajui kitu. Nimefuatilia wiki iliyopita nimekutana na hayo makitu niliyoyataja hapo juu. In total iligharimu 275,000/- hadi kuipata. Wapo wenye zaidi ya mwezi wanafuatilia na hawajui watafanikiwa lini
Mimi nilijaribu kufuatilia mtu kaniambia nijiandae na 250k, mwingine ananiambia niandae 350k, kimsingi nahitaji sana hiyo kitu maana fursa za masomo zinanipita hivi hivi
Hata hivyo niliwahi kufanya kazi na wazungu, wao wanashangaa kwanini sikua nayo maana ni hitaji la msingi
 
Andaa viambatanishi kama huna hasa Cheti cha kuzaliwa
 
Ushauri tu mda nzuri wa kutafuta hati ya kusafiria ni mda ambao huna shida nayo yani chukua weka ndani acha ipigwe uvundo siku una shida nayo unaingia ndani unachukua tu, hizi mambo za kukimbizana kimbizana mda mambo unaitaji watu wanapigwa sana
Ni kweli
 
Form unachukulia wapi?
 
Hivi wanatoa hata mikoani au ni dar tu
 
Laki 5 au 6 btn three to five days inakuwa tayari,otherwise utoe laki 2 kwa maana cha juu kinakuwa 50 hapo utaisubiri miezi miwili.
Waziri anatolea ufafanuzk video ya gwajima, halafu sijawahi kuona mtu muongo kama wewe,katafute popote pale wakikuomba zaidi ya 150000 navua nguo
.
 
Form unachukulia wapi?
form inapatikana online kwenye website ya uhamiaji, baadhi ya taarifa unazijaza online na pia utalipia kiasi kidogo cha fedha kama ada ya form (kama 30,000) kupitia mpesa, benki au njia nyingine zimeainishwa pale na kuingiza namba ya muhamala. baada ya hapo unai print hiyo form unaambatanisha na kila walicho ainisha kwa usahihi kisha unakwenda nayo uhamiaji.
website yao iko vizuri na inajieleza vizuri hatua kwa hatua
NB: hiyo ada ya form inahesabiwa kwenye ile 150,000/= hivyo kwenye hatua za mbele utalipia kiasi kilichobakia pekee
 
Aisee barikiwa sana
 
350,000+
 
Wadau mm nna swali hapo kuna ktu sjaelewa hivi passport ndo inakuwa specified kwa nchi Fulani unayokwenda au ni visa, hii imekaaje wadau
 
Wadau mm nna swali hapo kuna ktu sjaelewa hivi passport ndo inakuwa specified kwa nchi Fulani unayokwenda au ni visa, hii imekaaje wadau
Passport ni moja tu na inatumika kama utambulisho wako huko ugenini (humo ndani kuna maandishi ya rais wa JMT anaiomba nchi unakokwenda wakupokee na kukupa ulinzi) visa habandikwa / kugongwa kwenye kurasa za passport yako, passport hizi mpya zina kurasa 50
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…