Nimenyimwa hati ya kusafiria kisa mi ni wa Kigoma

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,191
1,231
Habari zenu wadau.

Ninayo masikitiko makubwa sana kuona nimenyimwa hati ya kusafiria) Passport)Kisa mimi ni mzaliwa WA Kigoma!! Picha ilianza hivi:Mimi Ni kijana mwenye umuri WA miaka 37, Babu na mababu zangu wote mzaa baba na mama wote ni wazaliwa wa wilaya moja wapo ktk mkoa wa Kigoma,Kwa kifupi mimi ni muha original,mnamo mwaka 1990 wazazi wangu walihamia mkoa wa Kagera wilaya ya Ngara, Na huko ndiko niliko patia Elimu yangu ya shule ya msingi na Secondary pia,

Km tunavyo jua ili upate passport kuna vigezo unatakiwa kuwa navyo,
Mimi nilipata mwaliko WA kwenda Norway kwa ajili ya Kuhibiri injili,Hivyo nikatumiwa barua ya mwaliko,kwenye mwaliko huo gharama zangu ilikus ni kupata passport tu na mambo mengine madogo madogo,

Wenyeji wangu walikuwa wapo tayari kulipia gharama zote za usafiri NK.

Baada ya hapo nilianza kuchukua hatua za kupata hyo nyaraka muhim,Kwa bahati nzuri kila kilicho hitajika nilikuwa nacho,Nilijaza form online ile ya kuomba pass kisha nikaipeleka ofis za uhamiaji,

Pale zilikaguliwa zikaonekana zote zipo sahihi,Nikapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole kisha nikaondoka, Baada ya Mwezi mmoja niliitwa tena ofisi za uhamiaji "Eti nihojiwe maana imeonekana kwamba huenda Mimi sio mtanzania,Nilifika pale nikajaza taarifa zote wanazo hitaji,

Cha ajabu Leo ni miezi 5 imepita sipewi haki yangu, Na gharama zote nimetumia zaid ya Lack 2 ,Swali langu nifanyeje ili wanirudishie gharama zangu?
 
Mkono mtupu haulambwi mchungaji,
Btw, kwanini utumie zaidi ya laki 2 wakati gharama ya passport kwa ofisini ni laki na nusu tu.
Kuna za viapo na za sijui nini Kuna Ile kama hujui kujaza fomu mwenyewe na kudownload unaenda steshenari zilizopo karibu na uhamiaji....Bado nauli..na kama hizo harakati unaona zunakuchelewesha Kuna kaela may be ametoa pia asaidiwe
 
Ndiyo
Nilipo-bold kuna gap umeacha wazi kuna kitu hujaeleza walikwambia ikipita miezi 5 hupati passport?
Aeleze.Alifuatilia au amekaa anaperuzi mistari ya biblia ya kwenda kuhubiri Norway?Hata hivyo,kuna raha na karaha za kuzaliwa na kuishi mikoa ya mipakani.Vilevile kaeleza familia yao ilivyohamia Ngara.Mulemule!Lazima Uhamiaji wawe na haja ya hofu.
 
Kuna za viapo na za sijui nini Kuna Ile kama hujui kujaza fomu mwenyewe na kudownload unaenda steshenari zilizopo karibu na uhamiaji....Bado nauli..na kama hizo harakati unaona zunakuchelewesha Kuna kaela may be ametoa pia asaidiwe
Kwa maelezo yake,

"Kwa bahati nzuri kila kilicho hitajika nilikuwa nacho,
Nilijaza form online ile ya kuomba pass kisha nikaipeleka ofis za uhamiaji,

Pale zilikaguliwa zikaonekana zote zipo sahihi,Nikapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole kisha nikaondoka,
Baada ya Mwezi mmoja niliitwa tena ofisi za uhamiaji...."

Labda nauli na elfu 20 ya form.
 
Usalama ni muhimu....hasa kwa wakazi wa mipakani....

Uchunguzi ni muhimu mno....kuna Burundi na Rwanda huko....

SERIKALI haionei....jiulize kwann wasiwaonee wakazi wa Tarakea....wakazi wa Udigoni Tanga....wakazi wa Sambaani milimani....wakazi wa Njombe....wakazi wa Kyela....wakazi wa Nanyamba....?!!!

Pole mkuu ....

Endelea kuwakumbusha...watakupatia.....
 
Habari zenu wadau.
Ninayo masikitiko makubwa sana kuona nimenyimwa hati ya kusafiria) Passport)Kisa mimi ni mzaliwa WA Kigoma!!
Picha ilianza hivi:Mimi Ni kijana mwenye umuri WA miaka 37,Babu na mababu zangu wote mzaa baba na mama wote ni wazaliwa wa wilaya moja wapo ktk mkoa wa kigoma,Kwa kifupi mimi ni muha original,mnamo mwaka 1990 wazazi wangu walihamia mkoa wa kagera wilaya ya Ngara,Na huko ndiko niliko patia Elimu yangu ya shule ya msingi na Secondary pia,

Km tunavyo jua ili upate passport kuna vigezo unatakiwa kuwa navyo,
Mimi nilipata mwaliko WA kwenda Norway kwa ajili ya Kuhibiri injili,Hivyo nikatumiwa barua ya mwaliko,kwenye mwaliko huo gharama zangu ilikus ni kupata passport tu na mambo mengine madogo madogo,

Wenyeji wangu walikuwa wapo tayari kulipia gharama zote za usafiri NK.

Baada ya hapo nilianza kuchukua hatua za kupata hyo nyaraka muhim,Kwa bahati nzuri kila kilicho hitajika nilikuwa nacho,
Nilijaza form online ile ya kuomba pass kisha nikaipeleka ofis za uhamiaji,

Pale zilikaguliwa zikaonekana zote zipo sahihi,Nikapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole kisha nikaondoka,
Baada ya Mwezi mmoja niliitwa tena ofisi za uhamiaji "Eti nihojiwe maana imeonekana kwamba huenda Mimi sio mtanzania,Nilifika pale nikajaza taarifa zote wanazo hitaji,
Cha ajabu Leo ni miezi 5 imepita sipewi haki yangu,
Na gharama zote nimetumia zaid ya Lack 2 ,Swali langu nifanyeje ili wanirudishie gharama zangu?
kuna shida sana kwa watu wanaotoka mipakani.
 
Kwa maelezo yake,

"Kwa bahati nzuri kila kilicho hitajika nilikuwa nacho,
Nilijaza form online ile ya kuomba pass kisha nikaipeleka ofis za uhamiaji,

Pale zilikaguliwa zikaonekana zote zipo sahihi,Nikapigwa picha na kuchukuliwa alama zavidole kisha nikaondoka,
Baada ya Mwezi mmoja niliitwa tena ofisi za uhamiaji...."

Labda nauli na elfu 20 ya form.
Ndio....
Ila hizi ofisi hizi ukitaka uende kiunyoofu upate huduma ni ngumu....
 
Kwa maelezo yake,

"Kwa bahati nzuri kila kilicho hitajika nilikuwa nacho,
Nilijaza form online ile ya kuomba pass kisha nikaipeleka ofis za uhamiaji,

Pale zilikaguliwa zikaonekana zote zipo sahihi,Nikapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole kisha nikaondoka,
Baada ya Mwezi mmoja niliitwa tena ofisi za uhamiaji...."

Labda nauli na elfu 20 ya form.
Ungekuwa mluguru ni 4 days only. Mimi ilichukua 4 days
 
Back
Top Bottom