Da sijui Mwenyekiti Tenga naye kabadilika siku hizi,vile viwanja vya UG ni aibu,mechi ya jana kati ya ZNZ na Rwanda ni aibu hilo tope ni kama zizi la ng'ombe la kule Umasaini wakati wa masika.Sijui kwa nini hawakusimamisha mechi ile,huwezi kucheza mpira namna ile na ni rahisi wachezaji kuumia,ukizingatia hawana viatu vya kuchezea katika hali ile ,ule uwanja ni kama bwawa la tope makazi ya mamba.CECAFA waache uroho wa vijisenti,ni aibu kwa mwenyekiti wa shirikisho Tenga,huyu Tenga wa siku hizi si yule wa zamani,sijui ndio kuzeeka