Kwakweli nimekuwa nikifuatilia michuano ya soka ya CECAFA inayoendelea Uganda kupitia luninga, sijawahi kuona michuano mibovu kama hii hasa uwanja unaofanyikia mashindano hayo. Hali ya uwanja ni mbaya sana umejaa maji na matope, na ni aibu kwa supersport kurusha michuano hiyo maana tunaaibishwa kwa nchi zingine zinazotutazama.
Bila kupepesa macho napenda kuipongeza serikali ya mkapa enzi hizo kutufanyia kitu cha msingi ambacho leo hii tunaweza kutamba na kuwakalisha kimya jirani zetu hasa waKenya ambao hujiona juu kwa kila kitu.
Ushauri wangu hatua ya robo fainali mechi zihamishiwe Tanzania maana tunaviwanja vyote vyenye sifa zinazohitajika.
Pia tuache uwoga tuombe kuandaa michuano ya kimataifa kama Afcon au CHAN maana uwezo tunao.
Hongera Benjamin william mkapa!