Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
213
1,726
Itakumbukwa 28 Machi, 2023 kulikuwa a mechi baina ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (Uganda the Cranes) kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Siku hiyo umeme ulikatika wakati mechi hivo inaendelea katika Uwania wa Benjamin Mkapa.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) alimuelekeza Naibu Waziri Me. Hamis Mwinjuma, (Mb) kukaaa na wataalamu kuchunguza tatizo la kukatika meme katika uwanja huo hasa wakati mechi zinaendelea kuchezwa na kupata suluhisho la tatizo hilo.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) alipokea taarifa ya wataalamu wa meme ambao walimueleza kuwa chanzo cha hitilafu ya kukatika kwa meme Uwanja wa Benjamin Mkapa ni kutokana na mchanganyiko wa meme wa jenereta na umeme wa gridi ya taita katika kuwasha taa za uwanja huo na wakapendekeza kuwa taa hizo ziwashwe na umeme wa jenereta pekee.

Mapendekezo hayo ya wataalam yalitekelezwa kama walivyoshauri. Hata hivyo, hitilafu ya kuzimika kwa taa imejitokeza tena usiku wa leo wakati ya mechi ya Yanga na Rivers United ya Nigeria ambayo ni mechi ya robo fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kutokana na kujirudia kwa hali hiyo licha ya ushauri wa wataalam kufuatwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana. (Mb) ameagiza hatua zifuatazo kuchukuliwa.

1. Kusimamishwa kazi ili kupisha chunguzi watumishi wanaohusika a undeshaji wa uwanja. Kufuatia agizo hilo na kwa mamlaka aliyonayo, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa a Michezo Bw. Saidi Yakubu amewasimamisha kazi watumishi wafuatao ili kupisha uchunguzi,
  • Salum tumbuka - Kaimu Meneia wa Uwanjawa Benjamin Mkapa
  • Manyori Juma Kapesa - Mhandisi wa Umeme wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
  • Tuswege Nikupala - Afisa Tawala Uwanja wa Benjamin Mkapa
Aidha, Katibu Mkuu Bw. Said Yakubu amewasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi watumishi wafuatao ambao nao wanamajukumu ya uendeshaji wa Uwanja wa Benjamin Mkapa
  • Gordon Nsajigwa Mwangamilo
  • Gabriel Mwasele
  • Yanuaria Imboru
  • Dkt. Christina Luambano
2. Kufuatia hatua zilizochukuliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa a Michezo Bw. Said Yakubu amemteua Bw. Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na uteuzi huo unaanza mara moja kuanzia tarehe 01 Mei 2023.

3. Katibu Mkuu kuwasiliana na wadau wote husika ili mechi zitakazochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa zichezwe wakati wa alasiri/jioni badala ya usiku katika kipindi ambacho wizara ianakamilisha taratibu za kupata mzabuni atakayefanya ukarabati mkubwa katika wanja huo kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa ligi/michuano ya kimataifa.

4. Ameagiza mamlaka za nje ya Wizara kufanya chunguzi wa kukatika meme katika uwanja huo na hatua za kuchukua.

Wizara inaomba radhi mashabiki wa soka nchini hususan wa timu ya Yanga kwa kadhia iliyojitokeza. Wizara Inawaahidi Watanzania wote kwamba Itaendeea kutanya ukarabati mdogo na mkubwa ilI Uwanja wa Benjamin Mkapa uendelee kutoa huduma na burudani stahiki kwa Watanzania pamoja na nchi jirani zinazotumia uwanja huo.

IMG_9659.jpeg
 
Hii ilitakiwa iwe kwenye mechi ya Tanzania vs Uganda. Kuwaachia waendelee na majukumu ni kuwapa nafasi kufanya kile kilichotokea leo. Waziri Pindi Chana ungewajibika wewe kwanza.

Najua hizi ni hujuma za wazi ili Simba ikose nafasi ya Ushiriki wa Michuanonya CAF Super Cup kwa kukosa uwanja wa nyumbani.
 
Hii ilitakiwa iwe kwenye mechi ya Tanzania vs Uganda. Kuwaachia waendelee na majukumu ni kuwapa nafasi kufanya kile kilichotokea leo. Waziri Pindi Chana ungewajibika wewe kwanza.

Najua hizi ni hujuma za wazi ili Simba ikose nafasi ya Ushiriki wa Michuanonya CAF Super Cup kwa kukosa uwanja wa nyumbani.
Waziri awajibike na umeme kukatika kwenye kauwanja kama kale?
Bro juta kuzaliwa Tanzania jutaaa ni laana
 
Hii ilitakiwa iwe kwenye mechi ya Tanzania vs Uganda. Kuwaachia waendelee na majukumu ni kuwapa nafasi kufanya kile kilichotokea leo. Waziri Pindi Chana ungewajibika wewe kwanza.

Najua hizi ni hujuma za wazi ili Simba ikose nafasi ya Ushiriki wa Michuanonya CAF Super Cup kwa kukosa uwanja wa nyumbani.
Hata mkienda huko myafanya lipi jipya
 
Kutokana na kujirudia kwa hali ya kukatika umeme katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ( Uwanja wa Taifa DSM) ikianza 28 Machi, 2023wakati wa mechi baina ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya
Taifa ya Uganda (Uganda the Cranes) kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kisha mechi ya Yanga na Rivers United ya Nigeria ambayo ni mechi ya robo fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) ameagiza hatua zifuatazo kuchukuliwa.

1.
Kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi watumishi wanaohusika na uendeshaji wa uwanja. Kufuatia agizo
hilo na kwa mamlaka aliyonayo, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu
amewasimamisha kazi watumishi wafuatao ili kupisha uchunguzi,


i. Salum Mtumbuka - Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
ii. Manyori Juma Kapesa - Mhandisi wa Umeme wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

ili. Tuswege Nikupala - Afisa Tawala Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Aidha, Katibu Mkuu Bw. Said Yakubu amewasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi watumishi wafuatao ambao nao
wana majukumu ya endeshaji wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

i. Gordon Nsajigwa Mwangamilo
ii. Gabriel Mwasele
iii. Yanuaria Imboru

iv. Dkt. Christina Luambano

2.
Kufuatia hatua zilizochukuliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu
amemteua Bw. Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na uteuzi huo
unaanza mara moja kuanzia tarehe 01 Mei 2023.

3.
Katibu Mkuu kuwasiliana na wadau wote husika ili mechi zitakazochezwa katika Uwanja wa Benjamin
Mkapa zichezwe wakati wa alasiri/jioni badala ya usiku katika kipindi ambacho wizara ianakamilisha
taratibu za kupata mzabuni atakayefanya ukarabati mkubwa katika uwanja huo kabla ya kuanza kwa msimu
ujao wa ligi/michuano ya kimataifa.

4.
Ameagiza mamlaka za nje ya Wizara kufanya uchunguzi wa kukatika meme katika uwanja huo na hatua za
kuchukua.

Wizara inaomba radhi mashabiki wa soka nchini hususan wa timu ya Yanga kwa kadhia iliyojitokeza. Wizara
inawaahidi Watanzania wote kwamba itaendeea kufanya ukarabati mdogo na mkubwa ili Uwanja wa Benjamin Mkapa uendelee kutoa huduma na burudani stahiki kwa Watanzania pamoja na nchi jirani zinazotumia uwanja huo.

Screenshot 2023-05-01 at 06.16.39.png
 
Back
Top Bottom