Watanzania tunachakujivunia mbele ya Kenya na Uganda- uwanja wa taifa

Pumb

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
295
104
Kwakweli nimekuwa nikifuatilia michuano ya soka ya CECAFA inayoendelea Uganda kupitia luninga, sijawahi kuona michuano mibovu kama hii hasa uwanja unaofanyikia mashindano hayo. Hali ya uwanja ni mbaya sana umejaa maji na matope, na ni aibu kwa supersport kurusha michuano hiyo maana tunaaibishwa kwa nchi zingine zinazotutazama.

Bila kupepesa macho napenda kuipongeza serikali ya mkapa enzi hizo kutufanyia kitu cha msingi ambacho leo hii tunaweza kutamba na kuwakalisha kimya jirani zetu hasa waKenya ambao hujiona juu kwa kila kitu.

Ushauri wangu hatua ya robo fainali mechi zihamishiwe Tanzania maana tunaviwanja vyote vyenye sifa zinazohitajika.
Pia tuache uwoga tuombe kuandaa michuano ya kimataifa kama Afcon au CHAN maana uwezo tunao.

Hongera Benjamin william mkapa!
 
Kenya haina viwanja vibovu kama jinsi ninavyoona katika runinga ingawa sio za hali ya juu kama vya ulaya. Lakini wa kulaumiwa ni cecafa maana hii michuano ilikuwa iandaliwe Kenya wakaleta siasa duni.

Imekuwaje timu zote kuchezea kwa uwanja moja?
 
Hivi kwanini inachezewa kwenye uwanja mmoja??ebu fikiria kila cku mechi mbili hata kama uwanja ni mzuri lazima uharibike tuu
 
CECAFA wanachojali ni pesa tu bila kuona madhara makubwa yatakayotokea kwa Wachezaji, CUF au FIFA hawalioni hili? Kwanini wasitoe tamko? Ni aibu tupu? Pale hakuna control ball, ni kubutua bora liende mbele matokeo yatakayopatikana ili mradi watu fulani washibe. Hapo ni kuwatesa wachezaji. Hivi wao hawaruhusiwi kugoma?
 
Da sijui Mwenyekiti Tenga naye kabadilika siku hizi,vile viwanja vya UG ni aibu,mechi ya jana kati ya ZNZ na Rwanda ni aibu hilo tope ni kama zizi la ng'ombe la kule Umasaini wakati wa masika.Sijui kwa nini hawakusimamisha mechi ile,huwezi kucheza mpira namna ile na ni rahisi wachezaji kuumia,ukizingatia hawana viatu vya kuchezea katika hali ile ,ule uwanja ni kama bwawa la tope makazi ya mamba.CECAFA waache uroho wa vijisenti,ni aibu kwa mwenyekiti wa shirikisho Tenga,huyu Tenga wa siku hizi si yule wa zamani,sijui ndio kuzeeka
 
Kweli uwanja tunao ila utawala wa uwanja ni mbovu muda c mrefu uwanja utakuwa gofu,vyoo ni vichafu vimejaa,viti vimeng’olewa,speaker za uwanjani wameishaiba,utaratibu kiujumla wa kuingia na kutoka kwenye majukwaa ni mbovu
 
Hata cjui walifikiria nn maana sio kwamba hawajui kua msimu huu Kenya na Uganda wanapata mvua nyingi hata hawakufikiria hilo!
Lingine uwanja mbovu! Kwani hawana viwanja vingine?usema kweli ni aibu kila siku mechi mbili nyasi haziwezi vumilia kabisa! Ila ndo hali halisi ilivyo japo hawaja fikiria!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom