Watanzania tumheshimu Rais, hatukufunzwa hovyo hivi

Ukishaona mkosoaji anatumia lugha za hovyo basi ujue hana hoja yeyote ya msingi, mkosoaji mwenye hoja atatumia nguvu kubwa kuipambanua hoja yake ila asiye na hoja ya msingi huwa mkali au hutumia vitisho na lugha za kudhalilisha, ustaarabu kwe siasa za Afrika ni shida sana.
sio hoja yeyote, ni hoja yoyote
yeyote inatumika kwa mtu.
 
Mfano wa tabia hizo alikuwa nazo Tundu Lissu katika KAMPENI ZA UCHAGUZI ULIOPITA.......
Ndugu,
Baba ambae kwa kuokoteza vineno unaanza kwa kumwita mwenzio msaliti, pia anatumia muda wake mwingi kutoa kejeli na kutukana wengine wengi hadharani na kwenye vyombo vya habari; muda wote hotuba zake zimejaa lugha chafu na ya kejeli, wote nyie mnaotegemea wanae kumheshimu hata hadharani, wa kweli MNACHEKESHA sana.
Wa kale waliona mbali na kusema hivi; Upendo huvuta upendo. Heshima kwa wengine hujenga heshima kwako na pia kinyume chake.
Haijalishi kuwa WEWE u mfalme au mkuu wa majeshi ili mradi si mgawa pumzi, vitisho/ubabe na ukali usio na mwelekeo kama waa nyati muda wote, HUBOMOA mahusiano na badala yake kujenga chuki na kwa wengine uoga/unafiki. AMEN.
 
Inachukua masaa mangapi kutoa amri kwamba Lissu alipwe haki zake? Kama kafuta kesi 147 FAKE kwanini anashindwa kufuta hukumu za waliohukumiwa na kutozwa faini ya mabilioni au kushindwa kulipa sasa wanaozea lupango? Kutangaza hadharani kwamba COVID 19 si Wabunge hivyo wasiingie tena Bungeni inachukua muda gani? Kumbuka HAKI huinua Taifa Na dhuluma huangamiza Taifa.
Hebu acha uongo banaaaa! Mbona Nusrat Hanje alitolewa usiku usiku kinyume na taratibu ili kutimiza udhalimu wao kwanini hao waliobambikiwa kesi FAKE ishindikane kuwatoa haraka? Ni rahisi kusema apewe muda wakati Watanzania chungu nzima wanaendelea kudhulumiwa haki zao. Ungekuwa ni mmoja wao wa hao waliobambikiwa kesi usingeandika apewe muda.
1622033788379.png
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ni wasukuma wachache ndio wanamtusi Madam president,,wakiongozwa na Muusiba na bashite
 
Nchi huru hii, msilazimishe watu wasimkosoe SSH wakati hana sera wala vision zaidi ya ku please kila kundi kwa kugawa na kutapanya ovyo keki ya taifa.
Dikteta aligawa cake ya Taifa kwa wasukuma wenzie na wachache aliotokanao Tanroads,,,

Samia kaja kutuunganisha Kama Taifa
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
'Mbona enzi za JPM hukujitokeza japo kwa mtindo huu wa utambulisho ghushi kukemea alivyokuwa anadhalilishwa hadi leo hayupo bado kejeli hizo zinaendelea na inawezekana na wewe ni mmojawapo ila kwa kutumia utambulisho mwngine una kuja na hoja ya kuwanasihi watu kutumia lugha ya staha. Anza kwanza kukemea wanaomkejeli Lissu, Mbowe, Lema, Bashiru, Polepole, Makonda, Ndugai, Halima Mdee, Lipumba nk waache tabia hizo mara moja kuliko kutetea upande unaokupa maslahi binafsi na wala hauhisi wafuasi wa watajwa hapo wanaumia kiasi gani kutokana na wanavyoguswa na viongozi hao.

There are three principles of justice dispensation to community, individualism, institutionalism, etc

1. Equality
2. Fairness & impartiality
3. Access
Link: Justice (Stanford Encyclopedia of Philosophy)
Je, mpaka sasa kabla ya kupandisha karipio hilo badala ya kuwashauri umeyimiza hayo hapo juu?
 
Mkuu, usiingie kwenye mtego huo

Maana ukianza kuwajibu kwa hasira na lugha Kama hiyo utafanana nao waliokosa heshima mkuu wangu

Mjinga akikutukana mbele za watu, mtazame na utabasamu, atajidharau sana
ANAINGIAJE KWENYE MTEGO WAKATI KAKUAMBIA WATU WANAOMDHIHAKI RAIS WETU JAMBO AMBALO NDILO UNALALAMIKIA BRO????
 
Rais wetu wa sasa kila anapozungumza, anatamka kila neno kwa staha, heshima na katika kipindi kifupi tumehisi tumetoka kifungoni. Kila binadamu anayo yake upungufu, lakini hadi sasa nimepunguziwa mzigo mzito wa kuijua kesho yangu pindi MUUMBA wetu anapotuzawadia siku inayofuata.
 
Nadhani ni busara sana kwetu Watanzania tukajikita kuchambua Sera za nchi na mwelekeo tuutakao kwa taifa letu kwa kuiweka mbele taswira chanya ya taifa letu.

Ni mbegu mbaya Sana ikiwa tutaendekeza kutengenezeana timu zinazojiita majina yanayotukuza kiongozi mmoja huku yakimdhalilisha na kumkosea heshima mwingine.
Ni vigumu sana kujadili mambo muhimu kitaifa wakati taifa linaongozwa zaidi kipropaganda huku masuala ya sera na mikakati yakipewa "lip-service" tu na viongozi. Na viongozi lazima waambiwe "wamekosea/wanakosea" inapokuwa dhahiri ili kuwatikisa wafanye kazi kwa weledi. Hiyo sio kashfa.

Ukipewa kazi ya umma unatakiwa kuwa na ngozi ngumu. Hapa kwetu Rais kuambiwa anakosea ni kosa la jinai - au uhaini kabisa kwa awamu za kwanza na tano. Huo nao sio utamaduni unaotakiwa.
 
Magufuli yeye hamkuwa mnamzihaki ukiangalia mpaka leo mnaendelea kumtusi. Au nasema uongo ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom