Watanzania tumheshimu Rais, hatukufunzwa hovyo hivi

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
Wanabodi,

Nawaomba Sana na kuwasihi Watanzania wenzangu tuitunze na kuienzi tunu yetu ya taifa inayoakisi malezi na maadili yetu ya kitanzania ambayo Ni heshima na uungwana kwa binadamu wenzetu.

Hivi karibuni kuna magenge yanazuka mitandaoni yakimkosoa Rais wa JMT Mh. Samia Suluhu Hassan, kwa bahati mbaya sana wanamkosoa kwa kumsodoa kwa maneno yasiyo na sitaha kwa kiongozi wa nchi, tabia hii haifai kabisa na sio nidhamu tuliyofunzwa Watanzania.

Ikiwa twahitaji kumkosoa Rais Basi na tufanye hivyo kwa lugha yenye staha na heshima, na tukumbuke kuwa huyu Ni Rais wa nchi yetu, huzuni yake Ni yetu pia, heshima yake ni yetu na akidhalilika Ni taifa linadhalilika, ukimdhalilisha Rais wako Ni Nani unayemtegemea amheshimishe?

Tuvumilie na tufunike hisia zenye hasira ndani yetu Kisha tukosoe kwa staha.

Nawasihi sana, Uhuru wa kuongea na kuonyesha hisia zetu usigeuke kuwa Uhuru wa kutukana na kuonyesha hasira zetu.

Mwisho:
Tuna wajibu wa kumsikiliza Rais na kuamini kwamba hakuna mama anayeweza kuwapa watoto wake sumu, hisia za mama ni nzito sana kwa watoto.
 
Ukishaona mkosoaji anatumia lugha za hovyo basi ujue hana hoja yeyote ya msingi, mkosoaji mwenye hoja atatumia nguvu kubwa kuipambanua hoja yake ila asiye na hoja ya msingi huwa mkali au hutumia vitisho na lugha za kudhalilisha, ustaarabu kwe siasa za Afrika ni shida sana.
 
Wanaomkosea heshima Rais Samia ni vijana wa mataga ambao wana hasira ya kuondokewa na mpendwa wao Rais Magufuli.

Wengi tulishawahi kuonya kwamba kundi la mataga limejaa vijana wasioweza kufanya siasa za hoja.

Uwezo wa vijana wa mataga upo kwenye kupotosha, kutukana, kudhalilisha, na vurugu.
 
Nadhani ni busara sana kwetu Watanzania tukajikita kuchambua Sera za nchi na mwelekeo tuutakao kwa taifa letu kwa kuiweka mbele taswira chanya ya taifa letu.

Ni mbegu mbaya Sana ikiwa tutaendekeza kutengenezeana timu zinazojiita majina yanayotukuza kiongozi mmoja huku yakimdhalilisha na kumkosea heshima mwingine.
 
Huwezi kutengeneza taswira chanya kuhusu nchi iliyojaa dhuluma na udhalimu. Juzi tu kesi 147 zimefutwa kwa sababu zilikuwa ni za kubambikiwa na wahusika hawajachukuliwa hatua zozote zile za kisheria. Nyingine chungu nzima zilikuwa zimeshahukumiwa na wahusika kulipishwa faini ya mabilioni au kuhukumiwa kifungo cha miaka mingi na wakati huo huo mama yuko kimya kuhusu kuwatendea haki Watanzania hawa.

Mama yuko kimya kuhusu COVID-19 ambao wanalipwa mabilioni ya pesa za walipa kodi pamoja na kuwa wameokotwa barabarani na kikatiba hawana hadhi ya kuwa Bungeni.

Lissu kadhulumiwa sana haihitaji hata dakika 10 kwa mama kutoa amri kwamba Lissu aliyewahi pesa yake yote matibabu lakini bado akapiga kimya sijui hadi lini!? Bado tuna safari ndefu sana katika nchi hii.

Nadhani Ni busara Sana kwetu watanzania tukajikita kuchambua Sera za nchi na mwelekeo tuutakao kwa taifa letu kwa kuiweka mbele taswira chanya ya taifa letu.

Ni mbegu mbaya Sana ikiwa tutaendekeza kutengenezeana timu zinazojiita majina yanayotukuza kiongozi mmoja huku yakimdhalilisha na kumkosea heshima mwingine
 
Huwezi kutengeneza taswira chanya kuhusu nchi iliyojaa dhuluma na udhalimu. Juzi tu kesi 147 zimefutwa kwa sababu zilikuwa ni za kubambikiwa na wahusika hawajachukuliwa hatua zozote zile za kisheria. Nyingine chungu nzima zilikuwa zimeshahukumiwa na wahusika kulipishwa faini ya mabilioni au kuhukumiwa kifungo cha miaka mingi na wakati huo huo mama yuko kimya kuhusu kuwatendea haki Watanzania hawa.

Mama yuko kimya kuhusu COVID-19 ambao wanalipwa mabilioni ya pesa za walipa kodi pamoja na kuwa wameokotwa barabarani na kikatiba hawana hadhi ya kuwa Bungeni.

Lissu kadhulumiwa sana haihitaji hata dakika 10 kwa mama kutoa amri kwamba Lissu aliyewahi pesa yake yote matibabu lakini bado akapiga kimya sijui hadi lini!? Bado tuna safari ndefu sana katika nchi hii.

Leo hii mama mnamtambua Ni Rais aliyetokana na uchaguzi wa 2020 mnaosema CCM iliiba kura,? Na kumbe mnamtambua Ni Rais na mnahitaji msaada wake?
 
Unadhani kwanini Mkapa mwaka 2019 alitaka uchaguzi wa 2020 usimamiwe na Tume huru ya uchaguzi? Na huyo ni mtu wa ccm aliyewahi kuwa Rais na Mwenyekiti wa maccm. Kwa sababu alijua Tume iliyopo ni FAKE na KAMWE haiwezi kusimamia uchaguzi huru na wa haki.

1621985694880.jpeg

Leo hii mama mnamtambua Ni Rais aliyetokana na uchaguzi wa 2020 mnaosema ccm iliiba kura,? Na kumbe mnamtambua Ni Rais na mnahitaji msaada wake?
 
Mkuu, sisi tunamfuatisha kiongozi wetu lisu (aka mashikishwa ukuta, zezeta, dishi limeyumba), ndiye alianzisha huo mchezo wa matusi. Aliwatukana wabunge kwa kusema wanaunga mkono mambo ya kijinga, kisha akahamishia matusi kwa rais aliyepita Hayati Dr John Pombe Magufuli. Wafuasi wake kina BAK, tindo, Mmawia, nk wote wanarusha matusi humu mitandaoni kwa muda mrefu sasa.
 
Uko sahihi Sana.....

Ni ADABU MBOVU....
Ni UKOSEFU WA NIDHAMU NDANI YA NAFSI ZAO.....
Ni MALEZI MABOVU WALIYOPATA UTOTONI....

Inakuwaje kijana mkubwa anamtukana mtu mzima....tena RAIS na AMIRI JESHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA?!!! Khaaa khaaaa.....

Mtu huyohuyo hawezi hata kumtukana "mgambo" njiani....Leo mtandaoni anamtukana RAIS WA NCHI Khaaa khaaaa SIASA ZA HOVYO KABISA......

Mfano wa tabia hizo alikuwa nazo Tundu Lissu katika KAMPENI ZA UCHAGUZI ULIOPITA.......

#KaziIendelee
 
Duuh unadhani atafanya yote hayo in a flash? Ile kusema atakutana na viongozi wa vya siasa vingine/wapinzani ili akae nao waone wataipelekaje nchi mbele kwa pamoja ni hatua njema sana maana hapo nyuma kidogo hilo halikuwepo kabisa ilikua nia uadui 100%.

Hebu naombeni tusubiri ataongea nao nini pengine kupitia jukwaa hilo ndio hizo ahueni unazosisema kuhusu akina TL tutazisikia. kufuta kesi na kutoa mtu jela ni vitu vyenye mchakato tofauti mpe mda mama. Nyota njema huonekana mapema.
 
Back
Top Bottom