Watanzania tumepatwa na ugonjwa mbaya sana! Tusipokuwa makini tutawaliwa tena hata na Waafrika wenzetu

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Ukifuatilia mazungumzo, mijadala, mawazo na taarifa mbalimbali kutoka kwa viongozi wa kisiasa, wafanyakazi, wakulima, wanahabari, wanafunzi, na kwa usahihi zaidi tuseme wananchi wa kawaida kwa ujumla wetu, utagundua kitu kimoja kikubwa, wengi hatuna MAARIFA ya kutosha!

Ugonjwa huu wa kukosa MAARIFA ni kutokana na sisi Watanzania kutopenda kabisa KUJISOMEA!

Watanzania "WANAOWAJIBIKA KUJISOMEA) " wamebaki kuwa ni wale tu wanaokabiliwa na mitihani mbalimbali kutoka katika Mabaraza ya mitihani!

Hali hii imepelekea Nchi yetu kuwa na watu wa ajabu ajabu na hasa viongozi wa kisiasa ambao hata wanapozungumza kuhusu jambo fulani iwe ni kuhusu uchumi, siasa au utamaduni, huwezi kujua wanaongozwa au kusimamia kanuni zipi!

Hii imepelekea Nchi hii kufeli kwenye mambo ya msingi mengi tukiwa bado ni Taifa changa lenye watu takribani milioni 60, ebu fikiria kwa akili hizi tulizonazo Watanzania tukifika watu milioni 100! Hali itakuwaje?

Tumekuwa "Taifa la Kijinga" la kufuata mtu mmoja anawaza nini au ameona nini, au kikundi fulani kinawaza nini au kimeona nini na risk ya kupotea ni apparent.

Kama unaweza kupinga hii hoja yangu basi ebu nieleze kama Taifa la watu milioni 60 iweje kila mwaka tujenge madarasa kwa ajili ya watoto wetu baada ya matokeo ya mitihani kutangazwa?

Nieleze ni kwanini kama Taifa hatujitoshelezi kwa sukari,mafuta ya kula, sementi n.k lakini tumeshindwa kabisa kutumia fursa hizo kutatua tatizo la ajira kwa vijana wetu wanazagaa ovyo mitaani!

Tumekuwa watu wa ovyo wenye mawazo finyu na ya kimasikini sana! Kama Taifa hatuna ndoto kubwa (big dreams) kwa watu wetu na tunaona hata wale wachache wenye mafanikio kutokana na ndoto zao kubwa (big dreams) na jitihada zao binafsi kama maadui, wezi na watu wanaostahili kudhibitiwa kwa hali zote.

Watanzania na hasa viongozi wa kisiasa mliopewa dhamana ya kuongoza mnatakiwa kubadilika, kusimama na kutambua kuwa Tanzania kama Taifa ni kubwa na ni muhimu kuliko mtu yeyote mojamoja.

Mnapaswa kutafuta MAARIFA hasa kwa KUJISOMEA taarifa,tafiti na machapisho mbalimbali ili kujua mwelekeo sahihi wa Dunia tuliyonayo na kuacha kabisa kushupaza shingo kuwa MNAJUA KILA KITU!

Watanzania pia tunapaswa kubadilika sana na kutafuta MAARIFA kwa njia mbalimbali na hasa kwa KUJISOMEA na kuacha kutoa muda mwingi kwa mambo ya mizaha, ucheshi na vituko vingine vingi.

Kwa msingi huo tunaweza kujenga hali inayoweza kutusaidi kujenga Taifa imara lenye watu wanaojitambua kwa manufaa ya kizazi chetu na kizazi kijacho.
 
Wengi siyo kwamba hawana maarifa haswa kwa suala ulilosemea la kujaribu kurudisha watu nyuma wenye big dreams!

Percent kubwa ya watanzania wana roho mbaya sana! Mtu anakuchekea kumbe anatambani kukufanya mishikaki akukule na ugali kabisa!

Watu hawapendi kufikiri nje ya box, na akifikiri nje ya box lazima watu wamuwazie tofauti, either waseme mwizi, fisadi, anatumia uchawi, ametoa kafara, etc etc etc. ukikaa na watanzania kama umefanikiwa usiposemewa hayo hapo juu, just know wewe ushahamishwa nchi na aliens upo mars na siyo tz tena!

Taifa la Wasaga Sumu hahahaaa😂😂😂
 
Umeandika UJINGA Mkuu.

Jisemee wewe usisemee Watanzania.

Mimi nawaona wengi tu wanasoma sana, Juzi nilikuwa na kiongozi mmoja nikawa namchomekea viswali vya mitego nikimpima uelewa nikagundua anajua mavitu mengi tena current, na anauelewa mpana ila humble sana.


Sasa usitujumuishe wengine kwenye malalamiko haya mkuu
 
Naunga mkojo hoja.. mkuu umeona hatari ya ongezeko la watu kam hii ya sasa tu inatushinda. Nafkiri huo muda ukifika kutakuwa na vichwa vingine siyo hivi
 
Umechelewa sana kulifahamu hilo! Karibu, kwani wengi wameshalifahamu hilo ndio maana wanapigania kwa udi na uvumba ili kuondokana na janga hilo.
 
Hii mada ni muafaka sana kwa sasa. Kama Watanzania tunadhani kuna ambaye atawaza kwa niaba yetu. Hata hivyo walioamka wakitaka kuonesha njia wanawekewa vikwazo lukuki. Tuangalie kwenye biashara na teknolojia. Wajasiriamali na Wabunifu hawapewi kipaumbele na wanawekewa vigingi vingi.

Kwa mfano, anayetoka nje ya nchi akija hapa anapewa upendeleo sana ikiwemo kutolipa kodi kwa kipindi fulani lakini Mzawa kabla hajafanya biashara anayotaka hutakiwa kuingia gharama ikiwemo kulipa kodi TRA na Halmashauri wakati hajazalisha chochote.

Mbunifu hapewi fursa ya kuendeleza kipaji chake na kama ndiyo amebuni silaha basi ndiyo kabisa anafanywa mhalifu.
 
Tukijua kukamua Ng'ombe inatosha!
123319.jpg
 
Huku ni kupampuka huku.... Ulivyoanza tuu ilidhihirika nawe ni kundi la watanzania waliosemwa ktk mada ya msingi. Wanazuoni hawajengagi hoja hivyo. Yani wewe kuhojiana na mzee mmoja ndio unatoa hitimisho na KANUSHO ZITO namna hii.....
Huyo mmoja ni mfano. Na kwa sababu ilikuwa random ni research tosha pia nikujumuisha na baadhi niliowahi kuwaona. Jamaa kajumlisha sana mambo aisee.

Pia sijengi hoja kwa kuzingatia wananzuoni huo nao ni utumwa. Najenga hoja kama binadamu binafsi mwenye akili timamu ninayetumia ubongo wangu independently bila kujali popular opinions huwa zinasemaje
 
Wengi siyo kwamba hawana maarifa haswa kwa suala ulilosemea la kujaribu kurudisha watu nyuma wenye big dreams!...
Walioasababisha haya yote ni wanaume wa Taifa hili, wameshindwa kusimamia sehemu yao ya kula kwa jasho na kumlilia Mungu awabariki kulisha familia zao na kuandaa urithi wa watoto wao hivyo kushindwa kusimama kwenye nafasi zao za ujemedali na kuweka Taifa lenye kuinuliwa Sasa wao wamebaki nyuma na kupeleka mbele wanawake kupambana ambao wao wanaamua kwaajili ya mkate tu maana kazi ya kukusanya na kujenga siyo yao.
 
Umeandika UJINGA Mkuu.
Jisemee wewe usisemee watanzania.
Mimi nawaona wengi tu wanasoma sana, Juzi nilikuwa na kiongozi mmoja nikawa namchomekea viswali vya mitego nikimpima uelewa nikagundua anajua mavitu mengi tena current, na anauelewa mpana ila humble sana.


Sasa usitujumuishe wengine kwenye malalamiko haya mkuu
Mkuu jibu hoja za mleta post.
1. Kwanini kila mwaka bado tunahangaika na madawati pamoja na ujenzi wa madarasa? Je wenye mamlaka hawajui trend ya udahili na ufaulu?
2. Kwanini tuna uhaba wa mafuta na cement? Je waliyopewa dhamana hawaoni kama hizi ni fursa za kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wetu?
 
Back
Top Bottom