Watanzania tumeanza udini?

Watanzania tumeanza udini?

Mbona naona udini wa wazi wazi hapa tunatokaje?
Haya unaoyaona yalifichwa kwenye vifua vya watu, yalikuwa yanatafuta sababu yakuyatoa ndiyo wameipata sasa. Na utalipima hili kwakutulia na kuangalia mijadala inavyoendelea hapa tunazungumzia nchi kuna watu wako busy mara TEC, CCT, BAKWATA kama anatafutwa Sheikh au Askofu nawakumbusha Tanzania is a Secular State na si religious State. Haiwezi kuongozwa kwa Tamko la kutoka taasisi ya Kiislamu wala ya Kikristo. Huo ushauri wa Viongozi wa dini waupeleke kwa waumini wao tena kwenye nyumba za ibada. Siyo kila siku viongozi wa dini wako mbele kuitisha press na kutoa ushauri wa kinafiki. Manchi mengi yanayoweka viongozi wa dini mbelembele huwa yanakuwa nyuma sana kimaendeleo.
Nazichukia sana hizi dini za kuletewa zimekuwa chanzo cha machafuko sehemu nyingi kutokana na ajenda za siri za hao walizozileta.
 
Haya unaoyaona yalifichwa kwenye vifua vya watu, yalikuwa yanayafuta sababu yakuyatoa ndiyo wameipata sasa. Na utalipima hili kwakutulia na kuangalia mijadala inavyoendelea hapa tunazungumzia nchi kuna watu wako busy mara TEC, CCT, BAKWATA kama anatafutwa Sheikh au Askofu nawakumbusha Tanzania is a Secular State na si religious State. Haiwezi kuongozwa kwa Tamko la kutoka taasisi ya Kiislamu wala ya Kikristo. Huo ushauri wa Viongozi wa dini waupeleke kwa waumini wao tena kwenye nyumba za ibada. Siyo kila siku viongozi wa dini wako mbele kuitisha press na kutoa ushauri wa kinafiki. Manchi mengi yanayoweka viongozi wa dini mbelembele huwa yanakuwa nyima sana kimaendeleo.
Nazichukia sana hizi dini za kuletewa zimekuwa chanzo cha machafuko sehemu nyingi kutokana na ajenda za siri za hao walizozileta.
Lile tamko la wakotoliki sio la kinafiki
 
Lile tamko la wakotoliki sio la kinafiki
Hao Wakatoliki unaowatetea siyo Malaika, ni binadamu kama wewe nao wana mapungufu yao. Ndiyo maana sikutaka kumtaja mtu au taasisi nimezungumza kwa ujumla wake.
 
Sheikh Ponda yeye ana mwaga ukweli mtupu muangalie YouTube kule.
Yule alikuwa Mgombea nafasi ya Ubunge jimbo la Temeke kwa tiketi ya ACT, swali la msingi angekuwa amepata nafasi ya Ubunge angesema hayo alioyasema? Namuachia mwenyewe Sheikh Ponda.
 
Mbona naona udini wa wazi wazi hapa tunatokaje?
Samuya kaamua kuja na kete hiyo, divide and rule lakini huu moto aliouwasha lazima utamuunguza. Kawatengeneza BAKWATA wamsafishe, in reality unadhani kuna kiongozi wa dini anaweza kufurahia raia kutekwa, kulawitiwa na kuuawa kisa tu anapingana na rais? Kuna kiongozi wa dini anaweza kukubali real opposition wasishiriki uchaguzi eti abaki peke yake na irrelevant candidates wakati ni wazi hilo lazima lizae vurugu? Vyama vingi literally it means lazima kuwe na options ili watu wachague watakacho na kuwe na fairness katika ulingo wa kinyang'anyiro vinginevyo ni kukaribisha vurugu.
 
Huko anakotupeleka samuya ndio kubaya zaidi.
Asijihusishe na mambo ya Imani kama chombo cha kujisafishia. Mgogoro wake utakua mkubwa zaidi.
 
Yule alikuwa Mgombea nafasi ya Ubunge jimbo la Temeke kwa tiketi ya ACT, swali la msingi angekuwa amepata nafasi ya Ubunge angesema hayo alioyasema? Namuachia mwenyewe Sheikh Ponda.
Ndio angesema. Yule Mzee hajawahi kuyumba
 
Mbona naona udini wa wazi wazi hapa tunatokaje?
Hii ni kwaida ya CCM inaposhindwa kwa hoja huanzisha vihoja ili kuwadhoofisha wanaoipinga kwa hoja.

Hivi vituko havijaanza sasa. Kama wewe ni mtanzania, utakumbuka CUF ilipoanza kuwa tishio, iliitwa chama cha kiislamu ili wakristo wasikiunge mkono. NCCR-Mageuzi nayo ilibandikwa jina chafu kuipunguza nguvu.
Chadema kiliitwa chama cha wachaga na watu wa kaskazini ili kupunguza nguvu kwa kushawishi watu wa maeeneo mengine na kabila nyingine kutojiunga na hicho chama.

Hivyo usishangae, kwa tunaofahamu tunajua ccm wako kwenye kibano kikali ndio maana wametumia hii silaha ya udini, ukabila utafuata soon.
Uzuri watanzania wengi wameshawashitukia(ukiwemo wewe, ndio maana ukauliza).
Tuendelee kupambana ushindi uko karibu.
 
Kuna wakristo wengi tu wanamkosoa kiongozi aliyepo madarakani kwa kuikashifu dini yake na sio kumkosoa yeye kama alivyo,kiongozi akosolewe yeye kama yeye na sio kuanza kuikashifu mpaka imani yake,

Kila mtu aheshimu mawazo ya wengine,hiyo ndio demokrasia,kikundi fulani kikitoa tamko kisilazimishe kila mtu akubaliane nao,na pia kiheshimu na mawazo au mtazamo wa taasisi zingine,hakuna taasisi iliyo bora kuliko nyingine,tatizo liaanzia pale kakikundi fulani kujiona wao ndio kama final say,hawataki na wenzao watoe mawazo yao.
 
Back
Top Bottom