Watanzania Tulipotoka na Tunapoelekea

BigBros

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
1,238
630
Nchi yetu ipo katika utawala wa CCM tokea Uhuru hadi hivi sasa. Nchi imefikia katika hali hii mbovu ya kiuchumi na maendeleo kutokana na sera mbovu za uendeshaji nchi tokea uhuru hadi mwishoni wa awamu 4. Mbali ya kuwa na rasilimali na malighafi za kutosha, hii ni wazi kuwa Tanzania tumeshindwa kujikomboa kiuchumi na kimaendeleo kutokana na uhaba wa uongozi bora.

Rushwa, Utendaji mbovu wa watumishi wa Umma na Wizi wa mali ya Umma ni malimbikizo ya udhaifu wa uongozi wa awamu zilizopita.

Fikra ya mtanzania yoyote yule ya mtumishi wa Umma ni kuwa apige dili na kutazama mustakbali wake kwanza na sio mustakbali wa Taifa. Hizi fikra zipo kwa viongozi wa ngazi za juu hadi ngazi za chini. Kifupi hakuna mfanyakazi wa Umma anayetegemea kuishi kwa mshahara wa Serikali. Fikra hizi zimekuwa zikijijenga katika miaka yote hiyo ya Utawala wa CCM tokea uhuru hadi hivi sasa. Na hii ni kama maradhi ya Saratani yaliotambaa mwili mzima ambayo tiba yake haitapatikana hata kama ukipiga kimo therapy ya hali ya juu, la ziada ni kumuongezea maumivu mgonjwa tu lakini haitokuwa tiba ya hiyo saratani. Mindset ya Mtanzania ni potofu.

Viongozi wote wa siasa wa chama tawala ni matajiri. Tujiulize, wamezipatia wapi mali hizo wakati wao ni watumishi wa Umma miaka yote? Ni wazi kabisa, Pesa za wananchi na pesa za walipa kodi ndio zimewaneemesha na kutumika vibaya. Kifupi wanasiasa ndio wahujumu wa nchi hii.

Awamu ya 5 pia ni uongozi wa CCM ambao umeingia na kasi mpya wa kutaka kutibu hiyo Saratani iliyosababishwa na yenyewe. Imekuja na Kimo therapy kali kabisa ambayo yaleta maumivu makubwa mwilini, hata zile sehemu zilizokuwa haziumwi lakini leo mgonjwa analalamikia maumivu. Mgonjwa huyo ni Mtanzania, na ndiye mlipaji kodi.

Serikali ya awamu ya 5 imekuja na lengo zuri lakini inatengeneza majeraha mapya badala ya kutibu majeraha. Kama kweli kuna wezi wa mali za Umma basi watuhumiwa wa kwanza ni wana siasa na sio wafanyabiashara. Hatujawahi kusikia mwanasiasa fulani amekamatwa na mali zake kutaifishwa hata siku moja bali tunasikia majina ya wafanyabiashara ambao ndio walipaji kodi miaka yote na kuwa sababu kubwa ya kunufaika wanasiasa lakini leo hii wakitajwa hadharani na kuashiriwa kuwa ndio wakwepaji kodi wakubwa. Mbali ya hayo wafanyabiashara waonekana ndiyo sababu ya nchi kuyoyoma kiuchumi.

Serikali yakusanya kodi zaidi ya matarajio yao taribani kila mwezi kwa mujibu wa takwimu za TRA. Lakini Serikali hiyo hiyo yasema Bungeni haina pesa na mitaani yasema Serkali inapesa nyingi. Wafanyabiashara wanabanwa na TRA kila kukicha, imekuwa usumbufu wa hali ya juu kuanzia wafanya biashara wadogo wadogo hadi wafanya biashara wakubwa. Hali imekuwa tete na wafanyabiashara wengi kufunga biashara zao na wengine wengi kutazama hatma ya biashara zao nchi zingine za jirani. Hali hii inaipelekea nchi kokosa mapato na kupoteza local investers ambao ndiyo wengi na ambao ndiyo mafuta ya uchumi wa nchi yetu. Kwa hali hii nchi itazidi kudidimia kiuchumi na kuipeleka katika hali ya yule mgonjwa kuongezeka na maumivu ya hiyo kimo therapy.

Mh. Rais katika hotuba zake amenukuliwa akisema kuwa yeye amechaguliwa na watanzania masikini na sio matajiri. Kwa hiyo atatetea haki za masikini. Hivi sasa kodi zaendelea kupanda juu hadi kumgusa huyo masikini ambaye mh. alisema kuwa atamtetea. Vocha zimewekwa VAT ambazo mtanzania masikini atazilipia. Umeme umepandishwa bei pamoja na VAT ambazo mtanzania masikini atazilipia. Ajira zimepungua kwa mtanzania masikini. Hapo tujiulize huyo masikini anatetewa kivipi wakati anazidi kubebeshwa mzigo wa taifa bila ajira??

Haki imekuwa adimu zaidi kupatikana. TRA wamekuwa sio wakala wa kukusanya kodi bali ni serikali juu ya serikali. Wamepewa nguvu kupita kiasa na kuwa wafusumbufu kwa wananchi. Kila kukicha tunasikia mapya.

Wanasema Tanzania zimefunguliwa viwanda 14,000 lakini hatuvioni na huku unemployment rate kuzidi kuongezeka. Wanasema wafanyakazi hewa 17,000 wamegundulika lakini hakuna aliyeshtakiwa na pia mishahara inayolipwa na serikali imeongezeka kwa zaidi ya kiasi cha 100bn badala ya kupungua. Ni kwanini mishahara hiyo iongezeke, je Serikali imejiongezea gharama baada ya kupunguzwa wafanyakazi hewa? Ni kwanini Serikali haina pesa? Na kama inazo pesa nyingi basi ni kwanini mtanzania anabebeshwa kodi zaidi wakati kipato chake ni wazi kimepungua? Haya ni baadhi ya maswali ambayo mtanzania anajiuliza pasipo na majibu. Ni wapi tunapoelekea?
 
Back
Top Bottom