Watanzania tulioko Switzerland

Mkuu naweza kupata mchongo wa kuja huko kusoma PhD au kupiga kazi, Mimi Nina masters
 
Mkuu naweza kupata mchongo wa kuja huko kusoma PhD au kupiga kazi, Mimi Nina masters
naomba nikujibu kwa niaba.
njia itakayokufaa ni ya kutumia masomo kwa kazi itakuwa ngumu na hiyo masters yako ya vyuo vya huko nyumbani, hawa jamaa huku hawaitilii maanani elimu inayozalishwa na baadhi ya nchi za afica na hutaweza kushindana na watu toka bara la ulaya, America na asia kwenye soko la ajira la kimataifa, hii itakuwia vigumu mno na utayaona maisha ya hapa kama jehenamu, lakini ukija kwa njia ya masomo utatakiwa usome baadhi ya kozi ili kuboost elimu yako atleast uweze kutambuliwa kwenye mifumo ya ajira na utakuwa unafanya part-time job kipindi uko masomoni na kuyasoma mazingira vizuri ya nchi kabla ya kujichanganya, hii njia itakuwa nzuri na itakusaidia sana

Kwa PHD kama utapata scholarship itakuwa ni jambo jema na kama utaweza kujigharamia pia ni vizuri, nina rafiki zangu wawili wanasoma PHD tuko nao huku Switzerland mmoja raia wa Nigeria anasoma chuo cha Geneva Bussiness School hapa mjini Geneva na chuo kinamlipa CHF 30,000 kwa mwaka,na atatumia miaka 4 tu kumaliza PhD yake, mwingine ni raia wa rwanda anasoma ETH Zurich Institute of science, Technology and policy PHD pia yeye analipwa CHF 35,000+ kwa mwaka

Ada za PHD kwa huku zinaanzia CHF2500 na kuendelea kutokana na chuo husika na kwa elimu ya PHD na mifumo ya elimu ya vyuo vya hapa itakuchukua miaka 4 mpaka 7 kumaliza na tambua Switzerland ni moja ya nchi ya ulaya wanayotoa elimu bora kabisa ulimwenguni na vyuo vyake ni vya hadhi ya juu kimataifa na hutojuta kusoma huku, Karibu mkuu tuwe pamoja huku lakini tambua maisha ya hapa ni ghali sana
 
Ok ngoja ni Google .
Ila na hii Corona
 


Nipe connection mkuu pls
 
Naomba nijue changamoto mnazokutana nazo foreignera especialy wa kutoka Afrika

Sent using Jamii Forums mobile app
kwangu changamoto ni upweke wa kumisi maisha ya kujichanganya na ujamaa ya huko nyumbani, naishi na watu tuliokulia makuzi na tamaduni tofauti kuanzia vyakula, style ya maisha, mahusiano n.k hii ni changamoto kubwa sana kuimudu

kimaisha sioni changamoto, nimeajiriwa na kampuni kubwa ya kimataifa na nalipwa vizuri ikiwemo kulipiwa nyumba, usafiri na mengineyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…