Watanzania tukubaliane na Zitto Kabwe, kumpa muda Rais Samia

mwasamasole

Senior Member
Oct 25, 2015
106
119
Ni ukweli usiopingika kuwa mfumo uliopo sasa hivi unaoongoza nchi yetu ni mfumo uliosukwa na hayati Magufuli, hivyo siyo rahisi kwa rais aliyepo kuoneasha mabadiliko makubwa na ya kushangaza yanayoweza kuwa tofauti na mtangulizi wake.

Hivyo baada ya muda fulani ambapo atakua kafanya mabadiliko ya uongozi uliokuwepo na akapanga safu ya uongozi anayoitaka yeye ndipo tutakapokua na uwezo wa kujua kama hana jipya au ni kweli kaanza vizuri. Tumpe muda, tuwe na subira.
 
Kuna watu wanalalamika kwanini mama hajamtumbua yule, au kwanini mama anaendeleza kile, nawashauri kuweni watulivu, muda bado.

Kwa Tanzania ili rais aweze kushika madaraka yake barabara ni lazima adhibiti chama chake pamoja na serikali. Kwa sasa mama Samia ndio kwanza ameanza kuishika serikali, kwenye chama bado kabisaa, hivyo basi tuwe wapole.

Akishakuwa mwenyekiti wa chama, akampata na katibu wake, basi wabunge wote wa CCM wakiongozwa na spika Ndugai watalazimika kurudi katika msatari, kinyume na hapo hawana chao 2025.

Kelele zote za ooh tuendeleze ya hayati JPM, au tusimseme vibaya hayati zitakwisha. Yote yatafukunyuliwa na mpendwa wetu atachafuka kwelikweli, ni lazima achafuke ili watu waache kumpima mama kwa kipimo cha aliyoyafanya hayati. Hata JPM alilifanya hilo kwa JK, alimchafua vizuri tu majukwaani.

Pia mama atakua nao uwezo wa kuivunja kabisa serikali bila hofu yoyote na kuanza upya na timu yake.

Tuvumilie, awamu ya sita imeanza lakini bado ipo kwenye 'transition period'.
 
Zitto yeye Sinia lake la Pilau liko Zanzibar kwaivo ameshiba

Alishamuuzia Chama Hayati Maalim Seif.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nilikuwa na imani saana kwa huyu mama lakini hadi muda huu nimeshaona taa nyekundu ataharibu kuliko watangulizi wake woote.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Apewe miaka mingapi? Haiwezakani apewe muda usio na ukomo.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Miaka mitano alikuwa Makamu wa Rais hivyo alitenda kazi zake kwa ukaribu mkubwa na magufuli na hata kumuwakilisha sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Hahitaji muda wa ziada katika utendaji wake.
Ni ukweli usiopingika kua mfumo uliopo sasahivi unaoongoza nchi yetu ni mfumo uliosukwa na hayati Magufuli, hivyo siyo rahisi kwa rais aliyepo kuoneasha mabadiliko makubwa na ya kushangaza yanayoweza kua tofauti na mtangulizi wake...
 
Mamalai angevunja floor nzima aweke vipaumbele vyake maana ukitazama vizuri kwasasa kumekua na ndimi 2 ndani ya taasisi 1.
 
Back
Top Bottom