Watanzania tu waongo sana!!!!

Watanzania tu waongo sana!!!!

Quemu

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2007
Posts
984
Reaction score
137
Jana nilipanda basi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu sana. Safari yangu ilianzia Tegeta na kuishia Posta Mpya. Kilichonigusa katika safari hiyo, sio msongamano wa abiria, ukosefu wa utumiaji wa deodorant kwa watanzania wengi, ubovu wa basi nililopanda au mengineyo. La hasha! Kilichonigusa ni jinsi watanzania tulivyokuwa waongo.

Haya. Nilikamata basi la kwanza kutoka Tegeta kibaoni mpaka Mwenge. Tulipofika mitaa ya Mbezi Makonde, jirani yangu niliyekaa naye kwenye kiti akapigiwa simu. Inavyoonekana kuwa alikuwa na mihadi ya kukutana na mtu mjini. Basi bila ya hiyana, nikamsikia yule bwana akimwambia mtu wa upande wa pili wa simu kuwa ameshafika Mwenge, na kwamba sasa hivi yuko katika basi linaloelekea mjini.

Nikajikuta natoa mguno wa mbali!

Haya. Nikafika Mwenge, na kuchukua basi la Mwenge–Posta. Tulipofika mitaa ya Ubalozi wa Ufaransa, bwana mmoja (sio wa basi la mwanzo) akampigia simu mtu aliyekuwa ana ahadi naye mjini, na kumuuliza yuko wapi. Alipopewa jibu na kuulizwa yeye yuko wapi, nikamsikia akisema kuwa yuko maeneo ya Red Cross.

Nikatoa kiguno cha wastani!

Haya. Nikafika zangu mjini, nikafanya kilichonipeleka, na kutafuta usafiri wa kurudi zangu Tegeta. Nikatumbukiwa kwenye basi la Posta-Mwenge. Tulipofika maeneo ya Moroko, mama mmoja aliyekuwa amekaa kiti cha mbele yangu akapigiwa simu. Kutokana na mazungumzo yalivyokuwa yanakwenda, ni dhahiri kuwa yule mtu wa upande wa pili simu ulikuwa unauliza kama yule mama bado yuko mjini, na kwamba anatarajia kurudi nyumbani saa ngapi. Basi yule mama bila ya hiyana akasema kuwa bado yuko mjini anamalizia malizia shughuli.

Nikatoa mguno mkubwa mpaka nikajistukia !

Wazungu wana msemo mmoja unaenda hivi ‘You are what you eat.’ Sasa je kuna uwezekano kuwa kuta za Taifa letu limejengwa kwa misingi ya uongo uongo? Kwa hiyo je ni sahihi kusema kuwa uongo umekuwa ni sehemu ya hulka yetu watanzania? Je ni kweli kuwa bila ya kuongopa hatuwezi kuaminika?

Pengine huu uongo nilioshuhudia kwenye safari yangu unaweza kuwa hauna impact kubwa (debatable) katika maisha yetu ya kila siku. Lakini kwani si viongozi wetu ni reflection yetu sisi wananchi? Sasa je, kutokana na hulka hii tuliyokuwa nayo, unafikiri ni mangapi yanayosemwa na viongozi wetu ni ya kweli? Uchaguzi unakuja. Je kuna uwezekano kuwa kuna namba kubwa (kama sio wote) ya wataka ubunge wamejichimbia kambini wanasuka uongo kabambe wa kuombea kura ?

NB : hayo mazungumzo yote ya kwenye basi yalikuwa yanasikika wazi. Kwa hiyo sikutega masikio makusudi kutaka kusikiliza mazungumzo ya watu. Si mnajua masikio hayana mfuniko.
 
Si watanzania tu. Nimesikia kisa cha John Edwards (aliwahi kugombea urais wa marekani) na mpambe wake nikabaki nacheka tu!
 
Yale yale mtu kapigwa simu na baba watoto wake anamuuliza uko wapi anajibu niko nyumbani kumbe baba watoto ndio yuko nyumbani hapo chacha, kwa mtazamo wangu hizi simu zimeleta madhara makubwa sana kwa jamii nikianza kulist sitamaliza leo nafikiri most of you are aware.
 
HAHAHA UKWELI SIKU HIZI UMEKUWA ADIMU SANA. kila mtu anadanganya pale alipo, hilo la kwenye dala dala ndo usiseme, watu wanadanganya sana. kuna mtu alishawahi tamka niko Morogoro kumbe tupo mitaa ya maktaba twaelekea mwenge. Hata watoto nyumbani hudanganya sana wazazi wao (hasa wanafunzi wa secondary)
 
vijimambo tu vya simu za mkononi..
ila ukianza na hiyo mifano Quemu ynaona hata siasa zetu za kibongo za uongo uongo ndo madhara yake haya .
 
tatizo la tanzania nikwamba waasisi wetu awakuwa wa kweli tumedanganywa sana atujazoea kuambiwa ukweli hivyo wengi wamekuwa waongo ila ili ni tatizo la dunia lia kila sehemu inatofautiana
 
Uwongo ni sehemu ya maisha. Na pengine watu wanasema uwongo si kwa nia mbaya bali kwa nia ya kuepuka maswali na bughudha nyingi kutoka kwa wale wanaotka kujua kitu fulani kutoka kwako. Bila kuwa mwongo kidogo utateseka sana.
 
mbona hujasema watu ambao wasikia simu inaita na bado hawapokei? Huo nao ni uongo yaani kuogopa kusema uongo kwa kufanya uoungo. i.e kutosikia simu. Unaweza kuconclude kuwa watu wengi wenye simu ni waongo in one way or the other.
 
Maumivu ya kichwa huanza taratiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu!!!!!!!!!!!!
 
nilikuwa muongo wa kupigiwa mfano,yaani hata mtu akinisalimia naweza kumwambia sio mimi amenifananisha lol,lakini sasa hivi nimejifunza nadanganya pale inapobidi tu,maana nilishawahi kuface maswali baada ya kudanganya mahali,sitakuja kusahau kijasho kilinitoka
 
Hizo zote tisa, kumi mpigie mtu simu huku unamwona(labda amekaa mahali), utamsikia jinsi anavyokudanganya kwamba yuko sehemu ingine tofauti kabisa!
Tulikuwa tumepanda kwenye kifodi siku moja (eneo la Kijenge-Arusha)na rafiki yangu, mara tunaposhuka akagundua ameibiwa simu...akaniomba simu yangu ili tuipigie...jamaa(mwizi) akajibu..."UNASEMAJE...MIMI NIKO SIKONGE-TABORA"..! Tuliachwa hoi, na hatukuwa na la kujibu tena, ikawa ndo mwisho wa simu hiyo!
 
Mbaya zaidi ni kuwa mtu unapoongea UKWELI hakuna mtu atakayekuamini.Mpaka mtu adanganywe ndio anaridhika.
 
Lakini jana jamani maswali ya 'uko wapi' yalikuwa too much.......labda watanzania walichoka kujibu.

@Charity hiyo ni kweli kabisa, sasa sijui ni kwamba mtu anataka asikie tu kile yeye alichotarajia and not otherwise??!!
 
nilikuwa muongo wa kupigiwa mfano,yaani hata mtu akinisalimia naweza kumwambia sio mimi amenifananisha lol,lakini sasa hivi nimejifunza nadanganya pale inapobidi tu,maana nilishawahi kuface maswali baada ya kudanganya mahali,sitakuja kusahau kijasho kilinitoka

Ukweli unakuweka huru sana, ukiongopa bana mashaka kila saa unahisi kuumbuka.
 
Lakini jana jamani maswali ya 'uko wapi' yalikuwa too much.......labda watanzania walichoka kujibu.

@Charity hiyo ni kweli kabisa, sasa sijui ni kwamba mtu anataka asikie tu kile yeye alichotarajia and not otherwise??!!

He!...sijaelewa kitu..
BHT, uko kwenye mada kweli?
 
Back
Top Bottom