Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 19, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa inawezekana kabisa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe na watupu!, uwezo wa kufikiri kwa kina (deep thinking) hatuna!. Uwezo wa kufikiri kwa tafakuri, ("logical thinking"), ni mdogo!, wengi wetu ni sifuri kabisa, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe, au tufanywa mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunadanganyika kwa viahadi vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo. Badala ya kudeal na issue zenyewe ambazo ndicho chanzo, kilichopelekea haya yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi! Tunahangaika na matokeo.

  Hii ignorance ya Watanzania ina cut across section ya society yetu yote na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya bunge letu, serikali yetu na ndani ya cabinet yetu!, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ma ignorants ajabu ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma zenye dhamana kubwa na maisha ya Mtanzania ambao ni ma ignorants ajabu!, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ikiemo mihimili ambao pia ni ma ignotants, na wana jf wengi tuu pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, ninayeandika hapa, Paskali pia ni ignorant tuu!, ila tofauti yangu na wengi wa maignorants wenzetu, wao wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu, tunaionyesha hiyo ignorance yetu wazi wazi kwa ku speak out and expressing our minds, tatizo, ni, in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!. Sorry for this.

  Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura za ushindi, mwaka hadi mwaka, na October 25 tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.

  Hisia za kujiuliza, kama sisi ni ma ignorants au tumelogwa, ni kufuatia kuwa na mtazamo, ya kuwa haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu ajabu kama haya tunayofanyia na CCM lakini bado sisi wale wale tunaichagua tena CCM na kuichagua tena na tena!, na October 25, tutaichagua tena!.

  Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 54 baada ya uhuru, sio tuu, wale maadui wakuu watatu bado wapo, bali ujinga umeongezeka mara dufu, umasikini sasa ni uliotopea, kila siku ni afadhali ya jana!, na maradhi hadi mengine ni janga, vimeongezeka afadhali ya zamani na enzi za mkoloni, bali pia, tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, Escrow etc, etc.

  Tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulidharau capital kwa kudai "pesa sii msingi bali pesa ni matokeo!".

  Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

  Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa October 25, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

  Namalizia kwa kukumbushia hili swali, are we really this ignorant?!, kwa kuchagua tuu ili mradi ni kuchagua, or this time, around tutaonyesha tumeerevuka angalau kidogo, hivyo tutachagua kwa sababu ya kuchagua, yaani kufanya informed decision?!, na sio kujichagulia tuu alimradi tumechagua!.

  Nawatakia Jumamosi Njema.

  Paskali

   
 2. kababu

  kababu JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 14, 2013
  Messages: 1,535
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  YAAAAAANI
  [​IMG]
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2015
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Imekaa vizuri.

  Chagua Lowassa
  Jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 12,347
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  We threw MERIT out and installed SYCOPHANCY, unategemea nini?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Sep 19, 2015
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 77,846
  Likes Received: 39,867
  Trophy Points: 280
  Wacha wee!

  Kaka msomi wa sheria katika ubora wake wa kuchanganya lugha.

  Kama mtu si msomi kama huyu 'kaka msomi' basi huwezi kabisa kushuka lugha kama ashukavyo yeye.

  Asipochanganya Kiswahili na ung'eng'e sie wengine tutajuaje sasa kama kasoma sheria UDSM?
   
 6. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2015
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,231
  Likes Received: 5,992
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo ujanja na werevu na kutokuwa ignorant na zuzu ni kuikabidhi nchi kwa hilo genge la wapiga DEAL likiongozwa na MTEI na UKOO wake???!!CCM imechoka,YES!Lakini Tanzania bado hakuna chama mbadala wa CCM.Tatizo la afya ya akili Tanzania ni kubwa kuliko inavyodhaniwa.Kama mtu anaorodhesha matatizo yake then anaona hilo genge la wapiga deal na watu wenye tuhuma lukuki Lowassa,Rostam Aziz ,Ndessapesa,mtei ndio watatuzi wa matatizo yenu.UZENI NCHI YENU KWA KARATASI.
   
 7. Z

  Zanzibar-ASP JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 28, 2013
  Messages: 4,509
  Likes Received: 7,139
  Trophy Points: 280
  Ila mwaka huu, ignorants wameshaamua jambo moja tu, MABADILIKO tu. Hapa ni Lowassa na UKAWA tu.
   
 8. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2015
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,586
  Likes Received: 12,067
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu tuna option moja tu.
  Hatuna budi kuichagua hiyo option.
   
 9. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,099
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  UJINGA wa watanzania ndio mtaji wa wanasiasa si UKAWA wala si CCM !...muhimu wenye mapenzi mema wenye uelewa sana wastani kidogo tusaidie ndugu zetu waliowengi kuwaelemisha ...
  ELIMU YA URAIA kuondoa UOGA...
   
 10. k

  kamagetac JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 25, 2014
  Messages: 2,472
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mabadiliko
   
 11. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  CCM imeinvest kwenye ujinga kwa 80%. CCM itashinda. Masikini Tanzania hawana elimu na hawaelewi. Utafiti wangu unaonesha hivo. Huu ni mtaji wa CCM
   
 12. Mhandisi Mzalendo

  Mhandisi Mzalendo JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2015
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 2,060
  Trophy Points: 280
  Ccm must go. Wanaotaka soft mabadiliko wananishangaza hakuna siku mtakayokua tayari kusema sasa ccm itoke maana Hawa watu ni walaghai Dr. Magufuli ni muongo sana anahaidi kila akionacho ahadi zake zinaweza zidi za kikwete mpaka sasa ameshaahidi mambo ya miaka 29 ijayo kuyatekeleza ndani ya miaka 5. Tumelogwa na aliyetuloga kafa
   
 13. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 9,256
  Likes Received: 35,594
  Trophy Points: 280
  Inaelekea Pasco amegundua Kuwa, hakuna mwanga mwishoni mwa tanuru!.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Ablessed

  Ablessed JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 4,625
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa lipo kwenye kujitambua. Hali tulionayo ktk maeneo yote uliyotaja tunahisi ni majaaliwa ya alietuumba yaani tumepangiwa kua hivyo. Hebu jiulize mama anaekosa hata sehemu nzuri ya kujifungulia hii October ataichagua ccm. Baba anaepeleka mwanae st kayumba ambako hakuna vifaa wala vitabu October ataichagua ccm .Nafikiri tatizo ni kubwa zadi ya tujuavyo
   
 15. pleo

  pleo JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2015
  Joined: Jun 20, 2013
  Messages: 2,609
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  mkuu utakua umesoma nje kila aya na kizungu kimoja angalau, haupo kundi la Watanzania wajinga. aisee!
  hivi kuna ubaya gani kumchagua kiongozi atakaye mwagilia mibuyu wakati wananchi hawana maji achilia mbali mahindi ya ugali.
   
 16. farajakwangu

  farajakwangu JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2015
  Joined: Jun 13, 2015
  Messages: 1,950
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Hakuna hata siku moja hicho chama chenye ubora unaotaka wewe utakiona hapa TZ, hata nyerere wakati anakabidhiwa nchi wazungu walikuwa na wasiwasi lakini walifika mahala wakatuamini wakatukabidhi nchi sasa tunasonga.
   
 17. m

  mkezwag JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  Asante Mkuu,,Mimi kwa upande wangu wakati Mwingine ninaposafiri huwa inanipa taabu sana kuonesha passport ya Tanzania.na form your information tunakoelekea ni kubaya zaidi kuliko tuliko toka kama tutaendelea na ccm.watu wetu sasa vyuoni na mashuleni wanatoka na vyeti tu badala ya cheti,maarifa na ujuzi.hatari sana
   
 18. M

  Mssassou JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2015
  Joined: Jun 17, 2015
  Messages: 1,540
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  hatuchagui wezi wa nembo wa chama kingine akienda ikulu ataiba zaidi
   
 19. Bejankabes

  Bejankabes Member

  #19
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 13, 2015
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mwaka huu mabadiliko hayaepukiki,tumejiondoa ujinga sasa
   
 20. m

  mkezwag JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  Mkuu tunaomba ccm mtusaidie na kwa Kuwa mnakiri mmechoka tusaidieni watanzania mnataka watu wa eneo gani ndio waanzishe chama ndo mkione kinafaa?nakumbuka mlianza na Nccr,mkaja kwa Cuf Leo mpo na chadema na ukawa na vyote hivi mliviita majina ya ajabu ajabu,mnataka nini hasa na nchi hii?au mnatulazimisha tutafute kuwangoa kwa Nguvu?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...