Rufiji
Platinum Member
- Jun 18, 2006
- 1,855
- 884
Wanabodi nimesoma hii habari kuhusu mpango wa serikali kuwakopesha wanafunzi waliopata division one kwa wanaume na division one na two kwa wasichana tuu ! Mimi bado aiingii akilini kabisa inawezekana vipi kwa mtanzania wa kawaida kuweza kumsomesha mtoto wake pale chuo ?
Hivi ni taifa gani hawa viongozi wanategemea kulijenga? Hivi hawa viongozi hatambui ya kuwa kima cha chini cha mshahara ni shs 60,0000?
Tutashauri serikali itoe mikopo kwa wote
2006-08-16 08:35:15
Na Haji Mbaruku
Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo kwa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, Bw. Nimrod Mkono, amesema bodi yake inaendelea kuishauri serikali ili iweze kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaoihitaji.
Bw. Mkono ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, alisisitiza kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete, wakati akizindua shule mpya ya kisasa huko Musoma wiki iliyopita, kuwa serikali haina fedha za kusomesha wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu.
Serikali imesema kuwa haina fedha, tunaendelea kutafakari suala hili kwa vile linajadilika, alisema.
Alikuwa akiongea na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kuhusiana na malalamiko ya wanafunzi kuhusu utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Hivi karibuni Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, wakati ikiwasilisha makadirio na matumizi ya bajeti yake bungeni, ilisema kuwa mikopo ilitolewa kimakosa, hivyo kuanzia sasa, watakaopewa mikopo ni wale watakaofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kwa wanaume na kiwango cha daraja la kwanza na la pili kwa wanawake.
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na BBC walipinga kauli hiyo ya serikali, wakisema kuwa kusomesha wanafunzi kwa misingi hiyo, kutaua maendeleo ya elimu nchini.
Pia, wanafunzi wanadai kuwa kutoa mikopo kwa vigezo hivyo kunaweza kuleta ubaguzi na kwamba Taifa litashindwa kuwapata madaktari, wanasheria, wakandarasi, wahandisi na watafiti wa kutosha.
Mmoja wa wanafunzi wanaosoma mchepuo wa Sayansi katika shule moja ya sekondari, Said Jumanne, alisema kuwa mara nyingi wanafunzi wa masomo ya Sayansi, hufaulu kwa kiwango cha daraja la pili na kuendelea, hivyo wengi wao watashindwa kupata mikopo kwa vigezo vya serikali.
Kwa sababu wanafunzi wengi sasa watakimbilia kwenye masomo ya Sanaa, ambako wanaweza kupata daraja la kwanza na wanafunzi wa masomo ya sanaa hawawezi kusomea udaktari hata kidogo, alisema mwanafunzi huyo.
Aliiomba serikali ifikirie upya suala la utoaji wa mikopo.