APA CHICAGO
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 259
- 293
Kwa mara kadhaa katika jukwaa hili la watu tunaojiita "Great thinker" zimeletwa post hapa za kuonyesha maovu fulani kwenye jamii yetu ama yamefanya na kiongozi fulani majibu yetu yamekuwa ya ajabu kwa mfano Acha wivu wa kike wewe, mara acha Majungu au peleka TAKUKURU hiyo habari.
Huwa ninajiuliza hivi kweli? hatujui nguvu ya vyombo vya habari? Kama mitandao ya kijamii? Au hatujui umuhimu wa kupashana habari kwa njia mbalimbali kama vile facebook na twitter? Kama ni hivyo basi kwenye jukwaa hili tupo kwa bahati mbaya tu na kama tunajua umuhimu wa kupashana habari basi tupo hapa kusifia kitu chochote kile ili mradi kiko upande unao usapoti na kupinga kitu chochote ambacho kiko upande ambao wewe hausapoti,kama hili ni kweli basi naweza kusema hatupo hapa kwa masirahi ya Taifa,
Letu hivyo tusubiri kizazi kingine huenda chenyewe kitakuja na kitakuwa kwa masilahi ya taifa letu.
Nimesema haya kwa kuzingatia post kadhaa zimeletwa hapa kwa masilahi ya jamii yetu na taifa letu kwa ujumla lakini watu walianza kukoment bila kutaka kujua kwa undani zaidi. Kwa mfano kuna post moja ililetwa hapa jukwaani ikigusia mwenyekiti wa Halmashauri ya Geita mjini mhe. Bugomora kugawa fedha za wananchi kwa karibu zaidi ya asilimia hamsini kwa kikundi kimoja tu cha vijana.
Badala ya ma great thinker wa JamiiForums kuhoji na kutaka kujua fedha hizo katika halmashauri zetu zipo kwa ajili ya vikundi vya aina gani?. Mfano, akina mama na walemavu n.k. Watu walijikita katika kumshambulia mtoa post.
Mimi wakati mwingine nawaza huenda Watanzania tumeshazoea shida na imekuwa sehemu ya maisha yetu ya kawaida vikiwemo vitendo vya rushwa?.
Nitoe wito kwa wana Jamiiforums wenzangu tujitahidi kuisaidia jamii yetu kwa kusema ukweli kama mtu ameonewa ajitetee mwenyewe.